Nataka nichukue uamuzi wa kuachana na huyu mwanaume, naombeni ushauri

zenna

aapo anasposema haupo romantic ndio tatizo so kabla haujafanya uamuzi wowote hebu jitathimini we mwenyewe ili ata ukiamua kuacha usijekurudia makosa
 
Last edited by a moderator:
Wanawake mna uvumilivu, mtu kakwambia sina feelings na wewe bado upo tu?

Halafu utakuja kusema mme wangu kazidi michepuko!
 
Kama huwezi kukibadili kitu au mtu, basi badilika we mwenyewe. Ikishindikana nyoosha mikono, yaani ondoka hapo, tafuta mbadala.
 
Jaman wote humu tunashuri ondoka ondoka sawa lakinn tujiulize

mleta mda utataka tena kuolewa? ama kuwa na mpenzi? sasa je utakaye mpata ni malaika?

ivi unaonaje ukatengeenza ulipo ili uwe romantic?

nichek PM nikupe ujanja wa mstuni ila shhhhhhhhhhhhhh
asije skia cacico manake atanitoa roho wallah navujisha siri za ndani

ushauri wangu ni rahisi sana kutengeneza ulipo ili pawe bora kuliko kwenda kujenga pengine ambapo hujui patakuwa bora ama laa
mekumiss bae! mekumiss haswaaaaaa uje tucheke!
 
Kwa kua bado hamjaoana unaweza kwenda tu, Mungu atakujaalia mbele ya safari maana hayo maisha ni hatarii
 
Movie za kimahaba ni Sinema tu zile acheni kumuongopea,wengi huwa wanataka sex kam wanavyoona kwenye hizo movie na wasipopata kama walivyoona ndio huanza kulalama hawaridhishwi,

Zile ni sinema kama za Holywood tu zina editing kibaoo
Sawa mkuu usemavyo, lakini ajifunze kuremba na kupamba, weka manukato ktk maisha ya nyumbani kwake, Dada zenna chukuwa ushauri huu;- ukiwa nymbani kwako mbele ya Boss valia mavazi maridadi acha mtambara yako pembeni.... zungumza lugha taamu ya kimahaba... Bwana atalewa huba zako!!!! zenna
 
Last edited by a moderator:
tembea uone dada try to found another way wengne wanashida zaidi akoo
 
Tena anasubiri tu uondoke afanye sherehe! Kifupi hakutaki kakuchoka.

Na ndio maana amekaa naye miaka 3 bila kufunga ndoa...jibu lipo wazi huyu dada sio chaguo lake...yuko mtu ambaye anatamani kumuoa...na ndio anayempa penzi huko nje
 
Wana great thinkers nashukuruni sana mmenipa ushirikiano, mmenishauri na mmenitia moyo pia. Ngoja nitawaletea mrejesho kwa nitakachokiamua. Mniombee jaman maana ni pagumu sana aisee.
 
Huu ushauri hauna afya kabisa mapenzi ni ya wawili.


Kuna watu wanaona kama ndoa nikulea watoto tu, hata kama unapigania kumlelea mtoto kwenye ndoa kama ndoa aina amani, imekuwa uwanja wa masumbwi na matusi ni wazi huyo mtoto ataathirika kisaikolojia tu, ni bora mtu mmoja akaa nsa mtoto kwa amani na ustawi mzuri, mambo yakung'ang'ania ndoa kisa tu kulea ni ujinga, ndoa ni zaidi ya kulea.
 
duh mbona kashakuchana live sasa hapo....hakuna swali tena.....af hata hamjaoana...
 
Me honestly sipendi watu waachane. Halafu hakuna mtu ambaye ni mkamilifu, hata utakayempata tena atakuwa tu na mapungufu yake.

Tatizo linakuja pale ambapo kuna mapungufu fulani kati yenu, Halafu mwenzako hakuelezi kwa utulivu tatizo liko wapi na inaonekana yeye ashafanya maamuzi yake. Hivi kwa mfano angemwambia tu, zenna mke wangu kuna A B C. Siku hizi haupo romantic, kwa nini na tutalitatuaje tatizo hili.
Lakini mtu anakwambia tu "sina feelings" mara sijui "sina hamu" au utaamua mwenyewe uondoke au ubaki? Kuna mapenzi tena hapo?

Mtu ambaye bado anakuhitaji si atakuita chini, mtazungumza tatizo ni nini na nini kifanyike jamani. Huyo kakuchoka ndo maana anakwambia utaamua mwenyewe kukaa or kuondoka. Kwa hiyo kuondoka ndo solution yake? Ukiondoka ndo utakuwa romantic?? Wanandoa/wapenzi hawaishi hivyo kabisa. Na pia tuwe makini na maneno ya kutumia kwa wenzi wetu
 
Kwa kua bado hamjaoana unaweza kwenda tu, Mungu atakujaalia mbele ya safari maana hayo maisha ni hatarii

Hawajaoana wakati wameishi pamoja na kulala kitanda kimoja miaka mitatu!!????????
 
Hawajaoana wakati wameishi pamoja na kulala kitanda kimoja miaka mitatu!!????????

Sasa kama mwanaume hajaona hiyo thamani ya miaka 3 ndani ya kitanda kimoja??? ukweli ni huo bado hajawa na hati miliki mkononi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom