Nataka nichukue uamuzi wa kuachana na huyu mwanaume, naombeni ushauri

zenna

Member
Jan 15, 2012
33
7
Habari za mchana,

Mimi ni mama wa mtoto mmoja, nilianza kuishi na huyu baba baada ya kupata uja uzito. Nilikua kwenye mahusiano ya uchumba kwa miaka 3 na mtoto kwa sasa ana 2 years, ila bado hatujafunga ndoa, sisi sote ni waajiriwa na tunalala kitanda kimoja. Tatizo ni kuwa mume yeye anafanya tendo la ndoa pale anapojisikia yeye na kwa mwezi na mara 3 au 4 nayo ni ya kusua sua yaani dk3 kashamwaga na hawezi tena kwenda round ya pili, halafu mimi nikiwa nahitaji sipewi.

Nikimuuliza shida ni nini anasema hana shida ila tu hana feelings na wala hana hamu. Pia anasema mimi siko romantic. miezi michache iliyopita nikuta message za Fb za kutongoza akichati na mdada mmoja na kuna housgirl aliondoka kwa kusema kuwa mume wangu anamtaka. Sasa jamani mimi nimeongea nae anasema uamuzi ni wangu nikiamua niondoke na nikiamua nibaki na kama siridhiki nitafute wa kuniridhisha. Sio kwamba nimechokwa au maana sina mchepuko na sijawai kumsaliti ila kwa sasa najihisi tu niachane nae niondoke tu.


Nisaidieni wadau
 
achana naye asikusumbue akili, mungu atakupa aliye mwema kwako na mkatimiziana mahitaji ya familia.
 
Hizo ndio concequences za mapenzi,ngoja waje wataalamu wakupe ushauri.
 
Nashukuruni wapendwa ila sasa ndo anaongea kwa hisia kuwa moyo wake unamshuhudia kuwa hajawai kuacha kunipenda
 
Jamaa ana roho ngumu simsemei ila kusema tu kuwe we we zenna sio romantic ni kuwa hana mapenzi wala huruma kwenye feelings zako wewe ndie muamuzi wa mwisho, maisha yako yatasimama bila hata uwepo wake usikubali kunyanyasika kama umeshindwa kummiliki toka awali hapo huna jipya.
 
Last edited by a moderator:
Kama umeolewa kwaajili ya kumpikia na kumfulia( yaani kumlea kama mtoto) basi kaa?????

Ila kama umeolewa kwa ajiri ya kushare nae kila kitu, ikiwemo tendo la ndoa, ondoka kabla huzaa mtoto wa pili.

Raha ya mapenzi mtu akupende sio awe anapritend au anakutolea maneno makali.

ZINGATIA: wewe ni bora kuliko anavyokudhoofisha kihisia, yupo mwanaume atakae ona ubora wako hadi utastaajabu.
 
Pole my dear.
Haya huitwa majuto mjukuu. Sio mwisho wa maisha ila tazama mbele ukizingatia
- unataka kuishi nae hadi uzeeni akiwa hivyo bila kubadilika? Uko radhi kufunga mdomo wako na kupokea alivyo? Kero kudanganywa kukosa uaminifu kuwa mbinafsi
- muwazie mwanao je uko tayari kulea mtoto uliemtenganisha na baba yake? Au kumuacha alelewe na mtu mwingine? Fikiria uko tayari kwenda kwenye ndoa ingine na mtoto alie na baba tofauti na ndugu zake wengine utakaowapata huko? Uko tayari kuwa na mtoto mmoja tu kwa hiari sio mapenzi ya Mungu?
Yote haya ni kati ya mambo ambayo huwa bijana tunaambiwa tujitahidi tusijiingize katika mahusiano mazito bila kujua wenza wenyewe kama wameshakomaa.

Ila ni faraja kujua kuwa hauko peke yako wengi wameweza na kudanikiwa kuwa na maisha ya furaha kwa kuchagua chochote.kati ya kuondoka au kubaki.
Cha muhimu usijidanganye tena.
 
Ondoka Dada, huyo hajui thamani ya mwanamke. Umpikie, umfulie halafu akuletee nyodo? Huyo hakupendi, kuna wengi tu walio tayari kupata mwanamke kama wewe.
Tena ondoka haraka kabla hajakufukuza.
 
Umejaribu kuwashirikisha "wazee" wa familia zote mbili kwake na kwako ili kujua kama anaweza huyo Mtu wako kubadili tabia? Au tatizo lake ni nini hasa? Mwanzo wakati mnajuana alikuwa hivyo hivyo au alibadilika ghafla?

Usichukue maamuzi ya haraka,think twice
Mahusiano ya kimapenzi yana matatizo mengi sana na yanatofautiana kutegemea mtu na mtu

Pole sana
 
Zenna usichukue uamuzi wa haraka,fikiria kwa kina matokeo ya uamuzi wako,fikiria maisha ya mtoto wako,single parent ina hasara zake,muhimu kwa sasa usifikirie kuongeza mtoto mwingine,shirikisha familia yake katika kutafuta muafaka.
 
Zenna usichukue uamuzi wa haraka,fikiria kwa kina matokeo ya uamuzi wako,fikiria maisha ya mtoto wako,single parent ina hasara zake,muhimu kwa sasa usifikirie kuongeza mtoto mwingine,shirikisha familia yake katika kutafuta muafaka.
Huu ushauri hauna afya kabisa mapenzi ni ya wawili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom