Nataka kuwa doctor naombeni ushauri

Nataka kuwa doctor naombeni ushauri

Mimi nimemaliza kidato cha nne nataka niende chuo kusomea diploma ya clinical officer naombeni ushauri kuhusu ajira na mshahara uko vip kwa sasa.

Thanks.
Soma ukifike kidato cha 6 tena mchepuo wa PCB kisha ufaulu vizuŕi hapo utakuwa na sifa za kujiunga na course ya udaktari katika chuo chochote cha afya
 
tatizo mentality yako ni hela tu sijui mshahara bei gani ......
kikubwa fanya juhudi na maarifa upate hiyo taaluma kwanza , mengine yatajipa tu....
Ajira zimekuwa kizungumkuti sana
 
Kwenye afya ajira bado zipo mshahara pia si mbaya ila uwe na chachu ya kujiendeleza baada ya kuanza kazi clinical officer bado ni cheo cha chini sana hvyo utafanya kazi kwa mipaka
 
Mimi nimemaliza kidato cha nne nataka niende chuo kusomea diploma ya clinical officer naombeni ushauri kuhusu ajira na mshahara uko vip kwa sasa.

Thanks.

Mshahara ni laki sita na themanini ukikatwa makato unachukua almost laki tano kushuka chini
 
Mimi nimemaliza kidato cha nne nataka niende chuo kusomea diploma ya clinical officer naombeni ushauri kuhusu ajira na mshahara uko vip kwa sasa.

Thanks.
Kuwa tu mkuuu kwan uamuzi ni wako mimi wala hayanihusu
 
Ni km mlinzi wa usiku tuu,clinical officer ni night na weekend Dr,
Utajuta Baadae
 
Haupo serious wewe.. kapige msuli mambo ya mshahara utajua badae
 
Mimi nimemaliza kidato cha nne nataka niende chuo kusomea diploma ya clinical officer naombeni ushauri kuhusu ajira na mshahara uko vip kwa sasa.

Thanks.
Ndugu, ni safari ndefu kidogo. Diploma tu ni miaka 3, kisha uje usome degree miaka 5 na mmoja was mafunzo kwa vitendo. Jumla Tisa ndio uwe doctor, sikuvunji moyo ila ni vema utambue hill mapema. Ila kama unapenda kwa dhati inawezekana kabisa. Hivyo ndio nijuavyo mm juu ya kuwa doctor kupitia clinical officer
 
Hivi kwanini huu mwaka wa internship huwa mnauhesabu wakati mtu anakua tayari anatibu na mapesa analipwa?Jumla minane bwana huo wa tisa mambo yanakuaga yameiva
 
Back
Top Bottom