Waungwana nawasilisha kwenu hoja yangu naomba nipatiwe mwongozo niufuate,
Mimi ni kijana wa kitanzania nina miaka 30 kipato changu kwa kazi ninayofanya ni 1200000 per month, nina mke na watoto wawili wa miaka 5 na mwingine mwaka 1.
Nawaonea wivu sana Bakharesa na Mengi na mimi nataka niwe kama wao au zaidi,
Hivyo naomba ushauri nifanye nini ili nifanikiwe malengo yangu.
Nawasilisha
Hakuna bilionea yeyote ambaye huwa anapanga kuwa anataka kuwa bilionea.Mabilionea wote duniani ni watu wanaopenda kuhudumia jamii kwa kile wafanyacho.Mfano BAKHERESA anahudumia jamii kupitia meli zake,vyakula lengo lake ni kuisaidia jamii kupata huduma bora kwa bei nafuu na katika kufanya hivyo amejikuta jamii imependa huduma zake na akawa bilionea.Bill gate yeye anapenda sana kuhudumia jamii anafurahi kuona watu wa kila lugha na rangi wakubwa na wadogo maskini kwa matajiri wanatumia microsoft products inampa raha kila apitapo kwamba kahudumia jamii ya ulimwengu vizuri na kajikuta bilionea.
Ukiwa mroho tu wa hela huwezi kuwa bilionea hata siku moja.Unatakiwa ukae chini uwaze unataka jamii uifanyie nini au kitu gani kizuri ambacho jamii itakukumbuka?
Mengi anahudumia vizuri jamii kupitia vyombo vyake vya habari amepitia milima na mabonde lakini hajaondoka huko pia anahudumia jamii nadhani kupitia kinywaji cha kokakola na maji mazuri ya kilimanjaro n.k na ubora wake umebaki vizuri jamii za makabila yote wanapenda vinywaji hivyo na hivyo kumfanya bilionea.
Utajiri huja kwa kuiangalia jamii na kujipanga unataka uisaidie nini kwa kupitia kitu gani na udhamirie hasa kuwa jibu la tatizo fulani la jamii na utafute ufumbuzi wake utakuwa bilionea.
Bilionea wa magari ya TATA kule india ni mtu rahisi sana anasafiri kwenye madaladala na treni walimuuliza utajiri wote alionao una kazi gani akajibu nafurahi kuona jamii ya watu wanafaidika kwa kusafiri na magari ya TATA inanipa raha kuwa na mimi nimechangia kutatua tatizo la usafiri la watu.Lenga kutatua tatizo ubilionea utakuja wenyewe si tu wa kukesha na kuomba uwe tu bilionea.Mabilionea wote duniani wana kazi ya kufanya kwa jamii duniani.Na ubilionea ni mshahara anaolipwa mtu na jamii baada ya kuitumikia vizuri jamii iwe kwa bidhaa,huduma n.k Ndio maana mabilionea wako kila fani wafanyabiashara,wafanyakazi,masheikh,mapadre,masista,wachungaji,wakulima,wanamuziki,waganga wa kienyeji, Waigizaji,wachekeshaji,waandishi wa habari n.k Kila mtu kutegemea na ukubwa wa uwezo na ubora wake wa kuihudumia jamii ikamkubali.
Cha kwanza kaa chini fikiria (Meditate) Unataka uifanyie nini jamii hapo ndio unatakiwa uanzie usianzie kufikiria unmechoka kuajiriwa unataka pesa nyingi kwa hasira ya kimshahara kidogo.Pili usimwonee wivu mtu yeyote safari ya ubilionea ni safari binafsi kila mtu ana yake.Ndio maana Hata kikwete alipoulizwa kwa nini watanzania ni maskini alisema sijui.Sababu safari ya utajiri kila mtu ana yake.