Nataka kuwa bilionea ifikapo 2025 msaada please

Nataka kuwa bilionea ifikapo 2025 msaada please

Mkuu sina chochote kwa sasa zaidi ya mshahara na ndio maana nataka ushauri wenu Great thinkers
Sikiliza, mabenki mengi yanatoa mikopo unaweza kukopo walau kuwa na mtaji wa kuanzia, kwa mshahara wa Tshs. 1.2m, take home yako itakuwa Tshs. 900,000/- hivi hivyo unaweza kopa Tshs.15m kwa miaka mitano na ukalipa about Tshs.400000/- a month for five years, na ukabakia na 500000/- ya kukuendeshea maisha kila mwezi, halafu anza biashara.
 
Hakuna bilionea yeyote ambaye huwa anapanga kuwa anataka kuwa bilionea.Mabilionea wote duniani ni watu wanaopenda kuhudumia jamii kwa kile wafanyacho.Mfano BAKHERESA anahudumia jamii kupitia meli zake,vyakula lengo lake ni kuisaidia jamii kupata huduma bora kwa bei nafuu na katika kufanya hivyo amejikuta jamii imependa huduma zake na akawa bilionea.Bill gate yeye anapenda sana kuhudumia jamii anafurahi kuona watu wa kila lugha na rangi wakubwa na wadogo maskini kwa matajiri wanatumia microsoft products inampa raha kila apitapo kwamba kahudumia jamii ya ulimwengu vizuri na kajikuta bilionea.

Ukiwa mroho tu wa hela huwezi kuwa bilionea hata siku moja.Unatakiwa ukae chini uwaze unataka jamii uifanyie nini au kitu gani kizuri ambacho jamii itakukumbuka?

Mengi anahudumia vizuri jamii kupitia vyombo vyake vya habari amepitia milima na mabonde lakini hajaondoka huko pia anahudumia jamii nadhani kupitia kinywaji cha kokakola na maji mazuri ya kilimanjaro n.k na ubora wake umebaki vizuri jamii za makabila yote wanapenda vinywaji hivyo na hivyo kumfanya bilionea.

Utajiri huja kwa kuiangalia jamii na kujipanga unataka uisaidie nini kwa kupitia kitu gani na udhamirie hasa kuwa jibu la tatizo fulani la jamii na utafute ufumbuzi wake utakuwa bilionea.

Bilionea wa magari ya TATA kule india ni mtu rahisi sana anasafiri kwenye madaladala na treni walimuuliza utajiri wote alionao una kazi gani akajibu nafurahi kuona jamii ya watu wanafaidika kwa kusafiri na magari ya TATA inanipa raha kuwa na mimi nimechangia kutatua tatizo la usafiri la watu.Lenga kutatua tatizo ubilionea utakuja wenyewe si tu wa kukesha na kuomba uwe tu bilionea.Mabilionea wote duniani wana kazi ya kufanya kwa jamii duniani.Na ubilionea ni mshahara anaolipwa mtu na jamii baada ya kuitumikia vizuri jamii iwe kwa bidhaa,huduma n.k Ndio maana mabilionea wako kila fani wafanyabiashara,wafanyakazi,masheikh,mapadre,masista,wachungaji,wakulima,wanamuziki,waganga wa kienyeji, Waigizaji,wachekeshaji,waandishi wa habari n.k Kila mtu kutegemea na ukubwa wa uwezo na ubora wake wa kuihudumia jamii ikamkubali.

Cha kwanza kaa chini fikiria (Meditate) Unataka uifanyie nini jamii hapo ndio unatakiwa uanzie usianzie kufikiria unmechoka kuajiriwa unataka pesa nyingi kwa hasira ya kimshahara kidogo.Pili usimwonee wivu mtu yeyote safari ya ubilionea ni safari binafsi kila mtu ana yake.Ndio maana Hata kikwete alipoulizwa kwa nini watanzania ni maskini alisema sijui.Sababu safari ya utajiri kila mtu ana yake.
Unachosema ni kweli kwa kuwa kinaendana na kanuni ya kimungu, kwamba tuko kwa ajili ya watu wengine, Mimi huwa nasikitika sana nikiona tajiri asiyeiangalia jamii, nachukia sana ubinafsi.
 
Mkuu mbona wewe ni bilionea tayari, mitaa ya Arusha kwa kipato chako hicho wewe tayari ni bilionea...
 
Ahsante mkuu je kwa maisha ya sasa yalivyo magumu kwa mshahara wa milion 1.2 utatosha nijenge na hatimae kuwa bilionea ndani ya miaka 11 from now?

Asikudanganye mtu kujenga ni kazi ya taratibu, kigumu kidogo ni kupata kiwanja kwasababu lazima utoe hela kamili. Mimi binafsi niliweza kujenga kwa mshahara wa laki tano, ndani ya miaka 6 na sasa nina na nyumba ndogo ya pili ya kupangisha. Mimi naamini nyumba ndiyo mwanzo wa maisha ya mtu yeyote, kupanga kunalemaza, kurudisha maendeleo na kudharaulika hata kama umewekeza kwa kiasi gani. Uwe kwanza na nyumbani kwako pa kudumu na familia mambo mengine yatafuata.
 
Sikiliza, mabenki mengi yanatoa mikopo unaweza kukopo walau kuwa na mtaji wa kuanzia, kwa mshahara wa Tshs. 1.2m, take home yako itakuwa Tshs. 900,000/- hivi hivyo unaweza kopa Tshs.15m kwa miaka mitano na ukalipa about Tshs.400000/- a month for five years, na ukabakia na 500000/- ya kukuendeshea maisha kila mwezi, halafu anza biashara.

Mtu ambaye hajawahi kufanya biashara unawezaje kumshauri akachukue mkopo ndo akaanzishie biashara? Acha kumpoteza mwenzio.
 
Mtu ambaye hajawahi kufanya biashara unawezaje kumshauri akachukue mkopo ndo akaanzishie biashara? Acha kumpoteza mwenzio.
Kwa hiyo ulitegemea nimwambie achukue mkopo akanunue gari kama wengine wanavyofanya?
 
Kipato cha 1.2M kwa mwezi, kwahiyo nimshahara. Kama ndicho kipato chako no way ukawa bilionea. Chukua maamuzi magumu, fanya biashara. Anza kama walivyoanza mzee Mengi, Bakheresa, kwa ufupi jifunze kutoka kwa mabilionea unaowafahamu kama Stive Job, Bill Gates, Warren Buffet n.k. mwisho soma Rich dad Poor dad by Robert Kyosaki itakusaidia.
 
Waungwana nawasilisha kwenu hoja yangu naomba nipatiwe mwongozo niufuate,
Mimi ni kijana wa kitanzania nina miaka 30 kipato changu kwa kazi ninayofanya ni 1200000 per month, nina mke na watoto wawili wa miaka 5 na mwingine mwaka 1.
Nawaonea wivu sana Bakharesa na Mengi na mimi nataka niwe kama wao au zaidi,
Hivyo naomba ushauri nifanye nini ili nifanikiwe malengo yangu.
Nawasilisha

Maisha ya biashara si lelemama kama unavyoyafikiria... wengi wa wanaokupa ushauri hawajawahi kuuza hata maji ya kufunga kwenye mfuko, ukitegemea mawazo yao naamini utaangukia pua.

Ni vigumu kupata mafanikio makubwa mno kama unayoyataka wakati huo ukiwa mtumishi.

Maelezo yako yana kila dalili za kufeli kwasababu unachokitaka kimejengeka kwenye misingi ya tamaa ya fedha ilihali hujui hata namna ya kuitafuta fedha yenyewe.

Lakini ukitaka kwenda unakotaka huko huna budi kuifata njia ya mateso na misoto iliyopo kwenye biashara.

Jikusanye kwa kile unachoona kinakutosha kisha acha kaz ukaribie kwenye ulimwengu wa wajasiliamali.
Nako si lazima ufanikiwe make ni kama karata 3, ukicheza vizuri na ukawa na disprine ya matumizi mi naamini utatoka tu.
 
Ndetirima,

Wengi wanaosema kujenga ni kufukia hela ni bachelors waliokataa kufikiri kesho, hivi unapangaje na familia ya watoto 2? Achilia mbali ndugu mambo ya Afrika na extended family

Ni watu waliokataa kuwa realistic kuwa kujenga ni kidogo kidogo kama ulivyoeleza. Nyumba ya thamani ya 35 milion haitolewi hela at per hivyo hakuna uwezekano wa kui alternate kufanya biashara ya 35 milion
 
Last edited by a moderator:
Wengine kwa mwezi wanapata laki 3 tena kwa shidaaa
 
Mbuyu ulianza kama mchicha....kwa kipato chako si haba jipangie bajet, mfano chukua 500000 kwa matumizi ya nyumbani, inayobaki wekeza sehemu yoyote utakayoiweza kufuatilia.
 
Kwa hiyo ulitegemea nimwambie achukue mkopo akanunue gari kama wengine wanavyofanya?

Huo sio ushauri mzuri hata kidogo. Mikopo inachukuliwa kwa biashara ilokwisha simama. Mwenzio hata wazo la ni biashara ipi anataka kufanya hana alafu wewe unamuongezea ujinga eti akakope? Acha utani kwenye mambo mazito.
 
Ahsante mkuu je kwa maisha ya sasa yalivyo magumu kwa mshahara wa milion 1.2 utatosha nijenge na hatimae kuwa bilionea ndani ya miaka 11 from now?

huo mshahara ni mkubwa sana kama una taka ku-invest ili baadaye uwe bilionea! achana na wazo la kujenga nyumba ya kukaa wekeza kwanza kwenye majengo ya biashara!
 
Karibu CCM gombea ubunge 2015. halafu tutakupa uwaziri wa Nishati na madini au mali asili
 
Huo sio ushauri mzuri hata kidogo. Mikopo inachukuliwa kwa biashara ilokwisha simama. Mwenzio hata wazo la ni biashara ipi anataka kufanya hana alafu wewe unamuongezea ujinga eti akakope? Acha utani kwenye mambo mazito.
Mkuu kwa mtu kama yeye anahitaji mahali pa kuanzia na hana, hivi unategemea lini atakuwa na mtaji asipoanza? Lakini pia yeye anayo security ya kupata mkopo ambayo ni kazi yake, anachohitaji kufanya ni kuwa na mahali pa kuanzia hata baada ya miaka walau 5 atakuwa na kitu, wakati huo anaendelea kufanya kazi yake huku akijisimamisha kwa Biashara, Na biashara ikishasimama anawezakuacha kazi na akajikita kwenye Biashara,
Mfano: akiweza kufuga kuku , kwa kila kuku 100 anaweza kupata shilingi 120000/- kila baada ya wiki 6, akianza na kuku 500 sio mbaya. Lakini anahitaji kuwa na miundo mbinu, na yeye hana pesa zaidi ya mshahara wake.
 
Sasa humu kwenyewe sidhani kama kuna billionea haswaaa wa level ya bakhresa et. al. Ukiachana na ubillionea kwa njia zisizo halali ushauri wa East African Eagle ndio uko makini nahisi. Utajiri wa kihalali ni kuangalia mahita ya wananchi wengi. Ukiweza kuja na product itakayovutia poplulation kubwa basi huo ndio ubillionea. Industry kubwa duniani na ambazo hazina dalili ya kufeli ni Chakula, Afya, na infrastructure (i.e. ujenzi na technologia!) Mimi pia nina target kama yako ila mimi target ni kuwa na business yeney turnaround ya billion 30 by 2018. Na my areas of focus ni hayo hapo juu.
Nakutakia kila la heri ndugu. Cha muhimu penda kuchakarika na vizuizi vione kama kuni ya kuchochea jitihada zako!
 
Karibu CCM gombea ubunge 2015. halafu tutakupa uwaziri wa Nishati na madini au mali asili

Mkiwa kwenye hedhi msiwe mnakurupuka kuleta ujinga hapa... nenda kwenye siasa au mmu ndo kuna mbulumunda kama wewe.
 
Nadhani wangekuja hao akina Bagharesa na Mengi ndio wangekupa jibu sahihi..Hapa ni sawa wote tuko ndani ya chumba cha mahabusu tunasikia mtu anapita kwa nje, wewe unatuuliza..NI AFANDE GANI HUYO ANAPITA? au unadhani sisi hatutaki kuwa mabilionea? hahaha mkuu, weka mipango tu na uifuate utafanikiwa.
 
Back
Top Bottom