Nataka kutembelea Zanzibar, Muongozo wenu Unahitajika

Mc cane

JF-Expert Member
May 18, 2018
5,570
10,506
Wakuu habari za majukumu ya utafutaji

Mimi sina mengi zaidi ya kuomba kufahamishwa kuhusu nini kinahitajika kwa mtu anayetaka kwenda kutembea Zanzibar

Naomba kujulishwa kuhusu aina ya Usafiri wa kwenda na gharama zake. Pia vipi kuhusu hoteli/lodge za Zanzibar na wigo wa gharama zake. Ningependa pia kujua utamaduni wa huko na jinsi unavyombana mgeni (mfano, je mtu anaweza kwenda na mwanamme ambaye hawana ndoa na wakalala hoteli/lodge moja n.k.)

Pia naomba kujulishwa, je wakati gani ni mzuri wa kutembelea huko, mfano kipindi ambacho hamna wageni wengi kutoka Ulaya/nje ya Afrika

Natanguliza shukurani zangu za dhati
 
Kitambulisho

Ticket ni kuanzia 35,000-70,000
Unachagua class

Kuna Kilimanjaro na Zanzibar Fast ferries (natumia hii hawakai baharini muda mrefu)

Kupata hotel nzuri na affordable book a day or few days before unaweza kulala stone town au shamba huko kuna kaumbali kidogo,

Unaweza kutumia tax kufika huko.



Hawana tabu na mtu, nenda na yoyote manake hata room zimespecify single
Double or family etc.
 
Asante, very helpful

Ningependa kujua zaidi kuhusu bei ya hotel ulizonishauri

Booking ya hotel ipoje, labda kuna link au majina ya hotel ili iwe rahisi

Thanks in advance
 
Dah.... Kama ni mpenzi wa vurugu....muziki wa taarabu mkubwa....kunywea pombe gizani....upepo wa bahari...na majani choma.....uliza kwa Kisasi 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nenda hotel na beach za shamba hapo mjini huwa Naona pamekaa kama Manzese au Tandale Tu.

Usisahau kitambulisho, narudia tena usisahau kitambulisho!

Ingia humu utaona bei tofauti tofauti za hotel za Kwenye fukwe.https://www.tripadvisor.com/SmartDeals-g482884-Zanzibar_Island_Zanzibar_Archipelago-Hotel-Deals.html


Nauli ni kuanzia 35,000



Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Asante, very helpful

Ningependa kujua zaidi kuhusu bei ya hotel ulizonishauri

Booking ya hotel ipoje, labda kuna link au majina ya hotel ili iwe rahisi

Thanks in advance

Tumia Airbnb
 
Back
Top Bottom