Nataka kusoma Diploma niache degree

mishie_allie

New Member
Aug 3, 2021
4
1
wadau wa elimu,

Nina swali. nataka kuacha degree nikasome diploma je inawezekana au natakiwa niende kwanza tcu kusema kama nimeacha au utaratibu upoke, msaada please.
 
Malizia hiyo degree unayosoma kwanza kama upo ukingoni yaani mwaka au miaka 2 kabla ya kumaliza then baadae ndio ufanye unachotaka kufanya huwezi kujua hiyo degree unayotaka kuiacha kwa sasa yawezekana ndio ikakupa deal siku za hivi karibuni.

Komaa nayo kwanza haya mambo hayatabiriki unaweza kudrop hiyo degree ukaikimbilia hiyo diploma ukidhania kuwa itakusaidia kwa kiasi fulani ukashangaa baadae unajuta kuwa bora ungeendelea ukamaliza hiyo degree kwanza then ungefanya maamuzi sahihi advantage ni kuwa tayari utakuwa na taaluma wakati unawaza kutafuta taaluma nyingine.
 
Ahirisha mwaka, then nenda kapige diploma yako (nadhani itachukua miaka miwili kama utaanzia NTA level 5 &6)
then kama utaona inafaa utairudia degree yako baadae.
Ila tuambie unasoma degree ya kitu gani na unataka kusoma diploma ya kitu gani?
 
Swali LA mwisho no LA msingi , unasoma degree ya nini na unataka kwenda kusoma diploma ya nn
 
  • Thanks
Reactions: snn
wadau wa elimu,

Nina swali. nataka kuacha degree nikasome diploma je inawezekana au natakiwa niende kwanza tcu kusema kama nimeacha au utaratibu upoke, msaada please.
Sema tyuuu ushadisco unakuja kutuchora hapa.... mnajifanyaga mabingwa wa kukesha club wadogo zetu
 
Ahirisha mwaka, then nenda kapige diploma yako (nadhani itachukua miaka miwili kama utaanzia NTA level 5 &6)
then kama utaona inafaa utairudia degree yako baadae.
Ila tuambie unasoma degree ya kitu gani na unataka kusoma diploma ya kitu gani?
agronomy sua
 
Sema tyuuu ushadisco unakuja kutuchora hapa.... mnajifanyaga mabingwa wa kukesha club wadogo zetu
Haki sijadisco sema ni kilimo na sielewi nahisi kama agronomy inawafaa sana CBG kuliko mimi PCB nachanganyikiwa natumia nguvu kibao kusoma na kuelewa.
 
Swali LA mwisho no LA msingi , unasoma degree ya nini na unataka kwenda kusoma diploma ya nn
nasoma agronomy, first year yan tukifungua ndo naingia second! nataka nikasome nursing sasa wazee walinambia nijarib hiyo agronomy lkn hata wao wameona kama hainifai kdg
 
Back
Top Bottom