Nataka kuokoka lakini sitaki niache pombe

Mkuu nakupongeza sana kwa kutaka kubadili maisha yako,okoka tu na endelea kugonga njimbo kama kawa,ila usiwatamani mabaamedi wala kuwapapasa,maana hata Yesu alitengeneza hiyo kitu kwenye arusi ya kana,KUNYWA SI DHAMBI ila unywe kwa manufaa ya mwili wako.
 
Jamani naombeni ushaur wa kiroho.mimi natamani kuokoka lakini kila nikitafakir kuacha pombe naona kama nakosa kitu kikibwa sana ktk maisha yangu ambacho ndicho kinachonipaga kujiskia mtu hapa duniani.wht shal i do?
Huwezi kutaka kuoka huku bado unatamani pombe.changua moja kuoka na uingie katika raha ya Mungu ya milele na utajisikia amani na furaha tele.Mwamini Kristo naye atakufungua kutoka kwenye kifungo cha pombe.
 
mnavyolichangamkia kanisa hilo mnanipa na mimi tamaa ya kuanzisha dhehebu langu halafu hizi mambo zote ruhusa kabisa.
Kanisa ni wewe mwili wako ni hekalu la Mungu na ukishamwamini Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako haijalishi upo kanisa gani Yesu atatenda miujiza katika maisha yako.Neno la Mungu linasema Mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka pamoja na nyumba yako
 
Jamani naombeni ushaur wa kiroho.mimi natamani kuokoka lakini kila nikitafakir kuacha pombe naona kama nakosa kitu kikibwa sana ktk maisha yangu ambacho ndicho kinachonipaga kujiskia mtu hapa duniani.wht shal i do?
<br />
Uzuri wako umeshamjua adui yako, pombe! Nusu ya tatizo lako limeshatatuliwa mpaka sasa! Second step, acha pombe, Okoka sasa maana saa ya wokovu ni sasa! Third step, achana na marafiki waliokuwa mnakunywa pamoja na kuwatangazia kwamba umeokoka (difficult but not impossible) maana Biblia inasema kwamba watu 2 hawaendi njia moja wasipopatana, ingia kwenye maombi ya kufunga, soma Biblia mara kwa mara, hudhuria Ibada Jumapili na siku nyinginezo za katikati ya wiki! Mungu ni mwema, baada ya muda utaiona pombe kama kinyesi! Mimi sasa hivi ukiniuliza bei ya bia hata sijui! Ubarikiwe!
 
Jamani naombeni ushaur wa kiroho.mimi natamani kuokoka lakini kila nikitafakir kuacha pombe naona kama nakosa kitu kikibwa sana ktk maisha yangu ambacho ndicho kinachonipaga kujiskia mtu hapa duniani.wht shal i do?
Kwani pombe inakuzuia nini kuokoka? Pekua kwenye biblia kuna sehemu imeandikwa... kunyweni mvinyo kidogo kwa ajili ya afya... tatizo ni matendo, kunywa lakini hakikisha hutendi dhambi... anyway, hata muujiza wa kwanz wa Yesu ilikuwa ni kugeuza maji kuwa divai
 
Kanisa ni wewe mwili wako ni hekalu la Mungu na ukishamwamini Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako haijalishi upo kanisa gani Yesu atatenda miujiza katika maisha yako.Neno la Mungu linasema Mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka pamoja na nyumba yako

kwa hiyo wanatuchangisha hela za kujenga makanisa tuwatoe mkuku
 
wewe okoka tu ..then endelea kunywa pombe ..huku ukiendelea kushuhudia washikaji zako mkikutana club na ukiendelea kujifunza mafundisho ya kukulia wokou..baada ya miezi kama 2 utajikuta umeacha mwenyewe bila ya mtu yoyote kukwambia..
mtu akiokoka anabadili hata fikira na mfumo wa maisha hawezi tena kuendelea kutumikia ulevi wa pombe.Acha kumpotosha
 
kwa hiyo wanatuchangisha hela za kujenga makanisa tuwatoe mkuku
Mkuu elewa kuwa kanisa ni mwili wa Kristo.Kama wewe unaishi na kulala kwenye nyumba nzuri kwanini usimjenge Mungu wako nyumba yakukusanyika pamoja na wakristo wenzako?Changa na mtumikie Mungu kwa uwezo wako wote maana mali na vitu vyote ni mali yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom