Nataka kuoa wifi wa shangazi yangu

Nataka kuoa wifi wa shangazi yangu

Blessed Son

Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
34
Reaction score
23
Wakuu,

Je, inafaa kumuoa wifi wa shangazi yangu, yani namaanisha shangazi yangu ana mume na mume wa shangazi ana dada yake ambae tunapendana na naona ananifaa sana "wife material"

Ushauri tafadhali
 
Hakuna shida kabisa. Hamna undugu wowote hapo wa damu au kikoo. Hapo kuna ukaribu tu wa kijamii ulioletwa na ndoa ya shangazi yako.
 
Oa hapo, hakuna shida kabisa.
 
Sasa huyo si ni shangaz yako mkuu..? mme wa shangaz yako ni mjomba af dada wa mjomba ako huyo ni shangazi
 
Sasa huyo si ni shangaz yako mkuu..? mme wa shangaz yako ni mjomba af dada wa mjomba ako huyo ni shangazi

Achana na hizo...kule shangazi kaolewa tu ndoa ikivunjika na urafiki unaisha...wacha jamaa achukue chombo...
 
Ruksa kuoa kijana, ila cjui sasa mke wako na Shangazi yako wataitanaje???
 
Hakuna undugu hapo, oa haraka iwezekanavyo....
 
kama ni mkristo nyie ndugu achaa kabisa.

hakuna undugu hapo. hata wifi wa dada yako unaoa tu.
sisi kwetu unazuiwa kuoa kizazi kilichoambatana na baba yako au mama yako tu.

wengine wote unaruhusiwa kuwabeba tu.
 
Hakuna undugu hapo complication itakuwa kwenye kuitana Hasa Shangazi Yako. Maana atakuwa Wifi-Mkwe Hivi.
 
Madada wameisha?Kuuliza humu jf ni wewe kuwa na wasiwasi tu japo ukweli unaujua
:wink2:
 
Hakuna shida kabisa. Hamna undugu wowote hapo wa damu au kikoo. Hapo kuna ukaribu tu wa kijamii ulioletwa na ndoa ya shangazi yako.

Kula like. ......"ukaribu wa kijamii ulioletwa na ndoa"
 
Ushagegeda vya kutosha unataka kuhalalisha mkuu? kama ni dhambi tayari unayo we endelea tu
 
Wakuu,

Je, inafaa kumuoa wifi wa shangazi yangu, yani namaanisha shangazi yangu ana mume na mume wa shangazi ana dada yake ambae tunapendana na naona ananifaa sana "wife material"

Ushauri tafadhali

Umeshakaba hadi penalti halafu unakuja kuhuliza wewe halalisha na ubwabwa usisahau kutualika mme wa shangazi yako endelea kumuita mjomba
 
Back
Top Bottom