Nataka kumshitaki Rose Mhando kwa utapeli

Nataka kumshitaki Rose Mhando kwa utapeli

Nitafurahi pia ukinijulisha madhara yawezayo nipata baada ya kuchukua hizo hatua.
 
Kumekuwa na malalamiko meng km haya kumhusu huyu mama. Mwanzoni nilifikili anaonewa. Anajiharibia sana ajirekebishe kwakweli. Vingnevo ataendelea kuwa wahapahapa.
 
Ninataka kumshtaki Rose mhando kwa utapeli. Tafadhari naomba wabobezi Wa kisheria hapa Ndani. Mara ya kwanza niliandaa tukio tanga hakutokea sbb alipata ajali, nilimlipa nikasamehe. Mara ya pili niliandaa tamasha Morogoro.. Nikamlipa hakutokea kwa maelezo aliyojieleza.. Mara ya tatu nimeandaa tamasha Tanga hajatokea tena mara hii nikiwa nimeandikishana nae. Kilichoniuma zaidi ni pale aliponidanganya kwa kutaka pesa zaidi na kuniambia yuko njiani anakuja nimtumie pesa ya mafuta ya Gari.. Kumbe hata wazo la kuja Kwenye tamasha. Hana mpaka sasa ameshakula zaidi ya milioni nne kwa style. Tofauti je naweza fungua kesi mahakamani. Naomba msaada. Sasa hivi nilimpigia simu hapokei..
Kwa maelezo yako inaonyesha hii habari ni uzushi unataka kumchafua Mtu.Wewe unapesa gani ya kusamehe ovyoovyo acha hiz😵NYESHA MKATABA.
 
Hivi rose amegombana na nani jamani...

Maana tokea wameanza kumuita tapeli ni mwaka wa tatu sasa cha kushangaza hafikishwi polisi wala mahakamani...

Mfano kama huyu mtu kama umeshaandikishana nae kila kitu kwanini usiende polisi ukashtaki...au hujui????

Mi nahisi kuna plot behind
 
Kwa maelezo yako inaonyesha hii habari ni uzushi unataka kumchafua Mtu.Wewe unapesa gani ya kusamehe ovyoovyo acha hiz😵NYESHA MKATABA.

Ndugu semzei inawezekana unanifahamu vizuri kuwa sina pesa. Ila hiyo kidogo niloyotoa na namna nilivyoipata ndio inayonihangaisha kuona inapotea katika mazingira ambayo sikuyakusudia na kama nilivyosema hapo awali sio mara moja. Mimi ni miongoni mwa watu waliokuwa wakimtetea sana Rose. Na nafikiri miongoni mwa watu waliokuwa nae karibu sana mpaka nafikia hatua hii sio jambo ambalo nimekurupuka. Nimekuwa mstahimilivu sana.
 
Kwa maelezo yako inaonyesha hii habari ni uzushi unataka kumchafua Mtu.Wewe unapesa gani ya kusamehe ovyoovyo acha hiz😵NYESHA MKATABA.
Fedha zenyewe Wanalipa ndogo million moja, mbili . Rose ni mwanamziki mkubwa watampaje fedha kidogo kiasi hicho?
 
Halafu watu wanampendea nini huyu mama? Make mimi huwa naamini Rose hana kipai cha kuimba zaidi ya kulazimisha kwa kurukaruka na kupiga gwaride, Na ishu ya kutapeli nisha isikia mahali kwingi sana wewe ni mtu wa tatu nasikia analalimika katapeliwa na Rose Muhando,

Ila mimi hata Bure siwezi mualika

Ukisikia mtu anakuambia ameokoka mfuatilie,lazima anamatatizo,kuna anayoyafanya anaficha kwenye wokovu,au uchumi umeyumba vibaya,au kaumwa sanaaaaaa.
 
Nimejitahidi mno kuwa mstahimilivu nimeenda kila mahali panapostahili. Nimejitahidi kumtafuta ana kwa ana bado ananikwepa simu zangu hapokei tena kinachokera sio mkweli ni muongo mpaka inatisha...sio Mimi peke yangu wengi sana wamelia lakini tumekuwa tukiishia kunung'unika tu kiroho kuwa tunamuachia Mungu bt ilipofika nadhani hata Mungu mwenyewe anatuona wapuuzi.!! Huyu kama kweli bado yupo kiroho basi so kwa walio karibu sana nae.!! Naomba unishauri mpendwa namna niwezavyochukua hatua.

Mtafute Alex Msama,anamsikiza Sana na ameshawahi hats kumlipia madeni yake
 
Fedha zenyewe Wanalipa ndogo million moja, mbili . Rose ni mwanamziki mkubwa watampaje fedha kidogo kiasi hicho?

Kwanini anazipokea kama ni ndogo? Hakuna pesa ndogo bwana! Wewe unamiliki sh ngapi hadi useme eti milioni moja au milioni mbili ni ndogo? Acheni ulimbukeni wa maisha.
 
Sheria zipo Panda mahakamani.
Na wengi mnamlalamikia uyu na sioni mkienda mahakamani kuna namna mnamalizana nae nini?
 
Lakini nimeshawahi kumsikia mara nyingi akilalamikiwa..tatizo nini???? Kafulia au?
Nanyi wapendwa wenzake kama mnahitaji mziki wake kiasi hicho kwanini msitafute njia ya kumsaidia aenende kwa misingi ya imani yenu??? Naona inakua TOO MUCH..... ROSE ROSE ROSE doooh
 
Wewe mwenyewe tapeli. Rose c ana meneja wake Alex msama nenda kamwone msiharibiane kwenye mitandao ok
 
Acha ukabila nyama we kwani wagogo unawaonaje ukome kuzalau kabila za watu
 
sasa unatushitakia huku jamiiforum c ufanye uende mahakamani
 
Wewe mwenyewe tapeli. Rose c ana meneja wake Alex msama nenda kamwone msiharibiane kwenye mitandao ok

Ahsante kwa kunijulisha kuwa ni tapeli wakati Fulani huwezi jua vile watu wakuitavyo.. Kwa taarifa tu hata msama aliisha mkataa Rose kuwa sio meneja wake.
 
sasa unatushitakia huku jamiiforum c ufanye uende mahakamani

Kabla sijaenda nilitaka kujua watu wenye taaluma hiyo watanishauri vip naamini hapa ndani wapo na wananelewa.
 
Sheria zipo Panda mahakamani.
Na wengi mnamlalamikia uyu na sioni mkienda mahakamani kuna namna mnamalizana nae nini?

Hekima ya kimungu imekuwa ikitumika mara nyingi. Zaidi ya ile ya kibinadamu.
 
Back
Top Bottom