Nataka kumshitaki Rose Mhando kwa utapeli

getrusa

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
2,150
1,821
Ninataka kumshtaki Rose Mhando kwa utapeli. Tafadhali naomba wabobezi wa kisheria hapa ndani.

Mara ya kwanza niliandaa tukio Tanga hakutokea sababu alipata ajali, nilimlipa nikasamehe.

Mara ya pili niliandaa tamasha Morogoro.. Nikamlipa hakutokea kwa maelezo aliyojieleza..

Mara ya tatu nimeandaa tamasha Tanga hajatokea tena mara hii nikiwa nimeandikishana nae. Kilichoniuma zaidi ni pale aliponidanganya kwa kutaka pesa zaidi na kuniambia yuko njiani anakuja nimtumie pesa ya mafuta ya Gari.. Kumbe hata wazo la kuja Kwenye tamasha hana mpaka sasa ameshakula zaidi ya milioni nne kwa style tofauti.

Je, naweza fungua kesi mahakamani?

Naomba msaada. Sasa hivi nilimpigia simu hapokei..
 
Halafu watu wanampendea nini huyu mama? Make mimi huwa naamini Rose hana kipai cha kuimba zaidi ya kulazimisha kwa kurukaruka na kupiga gwaride, Na ishu ya kutapeli nisha isikia mahali kwingi sana wewe ni mtu wa tatu nasikia analalimika katapeliwa na Rose Muhando,

Ila mimi hata Bure siwezi mualika
 
Pole mkuu nenda mahakamani. Watu wako after money. Taste the money test the money!!!
 
Huyu Muhando hamnazo kwanza anatuaibisha Wakagulu bora aseme amezaliwa huko huko ugogoni Kweli masikini akipata...
 
Ninataka kumshtaki Rose mhando kwa utapeli. Tafadhari naomba wabobezi Wa kisheria hapa Ndani. Mara ya kwanza niliandaa tukio tanga hakutokea sbb alipata ajali, nilimlipa nikasamehe. Mara ya pili niliandaa tamasha Morogoro.. Nikamlipa hakutokea kwa maelezo aliyojieleza.. Mara ya tatu nimeandaa tamasha Tanga hajatokea tena mara hii nikiwa nimeandikishana nae. Kilichoniuma zaidi ni pale aliponidanganya kwa kutaka pesa zaidi na kuniambia yuko njiani anakuja nimtumie pesa ya mafuta ya Gari.. Kumbe hata wazo la kuja Kwenye tamasha. Hana mpaka sasa ameshakula zaidi ya milioni nne kwa style. Tofauti je naweza fungua kesi mahakamani. Naomba msaada. Sasa hivi nilimpigia simu hapokei..
hapo ndipo mtakapojua mnawahitaji sana wanasheria, wawasaidie namna ya kuandika mikataba yenu hiyo. mimi ni mwanasheria, lakini kwasababu wewe uliyeandika hapa ninakufahamu, ni mimi nimpendwa mwenzako, hakushauri achana na kupelekana mahakamani,nenda kaongee naye uso kwa uso, asipokuelewa nenda kwa mzee wake wa kanisa, asipokuelewa tafuta rafikir zake/waimbaji wenzake kadhaa waombe mwende mkasuluhishane, ....akigoma maeneo yote haya jua ni tapeli hivyo nenda mahakamani, lakini kabla haujafanya hayo usiende mahakamani kwasababu atakachokipata mahakamani (madhara) na wewe yatakuathiri. najua ninachokisema.
 
Huyu Muhando hamnazo kwanza anatuaibisha Wakagulu bora aseme amezaliwa huko huko ugogoni Kweli masikini akipata...
awaaibishe wakaguru, kwani rose muhango ni mkagulu au asili yake mtu wa Tanga, sema basi tu alizaliwa huko wilaya ya kilosa? au nimekosea, nikosoeni.
 
ubaya wa kesi Kama yako yani analipa hela ulompa na analipa hadi gharama nzima ulotumia kuandaa tukio simply tuuu
 
baada ya kupiga hela zenu wapenda faida, asha tangaza kurudi alikotoka. islam
 
Duhhh!!! Pole sana embu anzia kwa viongozi wake wa kiroho ikishindikana nenda Mahakamani.
 
sasa anaandaa video ya album ya Mama mkwe. Atakuambia yupo busy sana, kwani kashajifungua? au zile tuhuma zilikuwa sio sahihi?
 
hapo ndipo mtakapojua mnawahitaji sana wanasheria, wawasaidie namna ya kuandika mikataba yenu hiyo. mimi ni mwanasheria, lakini kwasababu wewe uliyeandika hapa ninakufahamu, ni mimi nimpendwa mwenzako, hakushauri achana na kupelekana mahakamani,nenda kaongee naye uso kwa uso, asipokuelewa nenda kwa mzee wake wa kanisa, asipokuelewa tafuta rafikir zake/waimbaji wenzake kadhaa waombe mwende mkasuluhishane, ....akigoma maeneo yote haya jua ni tapeli hivyo nenda mahakamani, lakini kabla haujafanya hayo usiende mahakamani kwasababu atakachokipata mahakamani (madhara) na wewe yatakuathiri. najua ninachokisema.

Nimejitahidi mno kuwa mstahimilivu nimeenda kila mahali panapostahili. Nimejitahidi kumtafuta ana kwa ana bado ananikwepa simu zangu hapokei tena kinachokera sio mkweli ni muongo mpaka inatisha...sio Mimi peke yangu wengi sana wamelia lakini tumekuwa tukiishia kunung'unika tu kiroho kuwa tunamuachia Mungu bt ilipofika nadhani hata Mungu mwenyewe anatuona wapuuzi.!! Huyu kama kweli bado yupo kiroho basi so kwa walio karibu sana nae.!! Naomba unishauri mpendwa namna niwezavyochukua hatua.
 
Mkataba wenu ulikuwa unasema nini kama mtu asipotimiza makubaliano ?
 
Back
Top Bottom