Nataka kumpeleka mwanangu hapa

Nataka kumpeleka mwanangu hapa

nina maana ya value for money,$ 16000 for a year hakuna jipya hapo .usitete umashuhuri wa kijinga ina maana watoto wa hiyo shule wapo bright au wanapata cha ziada ukkilinganisha na other private schools? hiyo shule ni kwa diplomatic families and the fees is paid by the office not a parent alone ,hii ni kwa 90 % of all children

Kwanza, IST siyo kwa ajili ya watoto wa mabalozi tu.

Wanafunzi wa Kitanzania ni karibu nusu ya wanafunzi wote.

Kama mwanafunzi wa IST, certificate zake ni za Kimataifa. Na ni juzi tu, shule binafsi zikaanza kuiga kutoa GCSE certificates. Sijui kama zinatoa international baccalaureate diploma kama IST.

Kama umehitimu hapa VIZURI katika masomo yako, pamoja na barua ya guidance counsellor wako, na sifa nyingine, ni rahisi kupata scholarship kuliko shule za Kitanzania, private au public.

Kuna shule Tanzania unapelekwa Model United Nations na kupewa kazi ya kuiwakilisha nchi fulani kama Balozi Mwanafunzi?

Kuna shule Tanzania zinapeleka wanafunzi kusoma bure (full scholarship) Marekani na UK zaidi ya IST baada ya kuhitimu vizuri?

Kuna shule unafundishwa kutoa muda wako bure kwa jamii kama requirement ya kupata diploma?

Kuna shule unafundishwa kuogelea na kuokoa kwa kufundishwa CPR na mouth to mouth resuscitation?

Bora niishie hapa.
 
Safi sana kijana.

Sasa sijui uko wapi. Umeshajiunga na mafisadi au unawatumikia raia wa hii jamhuri kwa uadilifu.

Mimi nampongeza mzazi/mlezi wako kama aliona mbali na kukupeleka shule nzuri kama hiyo.

Payback to your country and its people by doing what is good for humanity!

Elewa vizuri.

Kwanza ni kujitumikia mpaka unaridhika na quality ya maisha yako popote duniani.

Watanzania wengi wanalitumia neno "uzalendo" kama kuweka nchi kwanza kuliko maisha yako. Au kuonyesha upendo kwa kufanya kazi nyumbani siyo nje.

Huo ni ujinga. Unatokana na exposure ndogo ya mambo ya dunia.

Huwezi kuiweka nchi kwanza kabla ya kujiridhisha kwa kila kitu wewe mwenyewe kwanza.

Kuna makampuni ya Kimarekani, Japan na nchi nyingine Asia na nchi nyingine kupunguza gharama ya uzalishaji na kuzidisha soko la bidhaa zao.

Hawa pengine utawaita wasaliti siyo "Wazalendo" kwa kuwa wamewekeza nje na kuwapa ajira raia wa nje badala ya kukaa nyumbani.

Dunia ya leo ni kijiji kidogo. Haina mipaka wala uzalendo.

Na siyo kila mtu aliotajirika ni fisadi.
Kuna wengi wamechuma kwa jasho lao Tanzania.

I work for the success of myself and my family. I don't work for a nation.
Neither do most people.

The paramount importance for me is to live happily. I found my happiness in Tokyo, Japan.
 
mhhh! halafu hawatumii syllabus ya Tanzania. si mchezo Ila wenye nazo wanawapeleka watoto huko
 
sasa mkuu yote hayo yametoka wapi? Yes you found your happiness in Tokyo. I respect that. That's why nimesema ukisoma shule nzuri Kama IST uwezekano wa kufanikiwa ni mkubwa. But it doesn't mean tuliosoma kayumba wote ni wajinga wajinga........kuna ambao hizo Harvard na LSE tumezisoma vile vile...so....my brother..don't go there.

Saying that I meant well it was just a brotherly challenge.

Asante.
 
Kuna watoto wa mabalozi kama wa Yemen, Korea na Japan. Wanakuja hata maneno matatu ya Kiingereza hawajui.

Wanapelekwa Intensive English Class, baada ya miezi sita, anaongea vizuri kabisa.

Tunapelekwa Model United Nations, Nairobi, kujifunza debating.

Huwezi kumaliza IB2 (form 6) mpaka ufanye masaa 80 ya volunteer work, hapo Salvation Army, kwa Mama Theresa au Katika hospitali yetu ya Kijiji cha Kinduitwi.

Pia, tumepiga rangi wodi za Ocean Road Hospital.

Tunafundishwa kuogelea na kuokoa.

Maktaba haina tofauti na Maktaba ya nchi tajiri. Kuna kila aina ya vitabu na magazines.

Kwa elimu, IST haina mshindani Tanzania.

Ila kwa majengo mazuri IST imepitwa vibaya sana na LOYOLA HIGH SCHOOL.
 
I beg to differ. Again nimekupa mfano..kuna akina Masanja tumesoma shule za UPE za shs. 20..Lakini Mungu ametuongoza tukatoboa kwenye maisha. Lakini I can guarantee you in reality akina Masanja tunaotoboa notwithstanding our background ni wachache mno..ndo maana umasikini hauwezi kuisha.

Ukisoma shule kama hiyo hata exposure unayoipata ni zaidi ya University. Mf. Mimi kwa mara ya kwanza nimemiliki laptop nilipokwenda kufanya masters nje ya nchi!! Nimetumia internet..(Imean kuitumia..siyo hizi za facebok na IG) nimemaliza Form six.. Ila mtoto wa hizo shule anafanya niliyofanya akiwa darasa la kwanza na kunizid!!!

lets face it ni umasikni tuu ila shule kama hizo zinasaidia sana vijana wetu....

IST pengine ni shule ya kwanza kutumia MS-DOS miaka ya 80. Mimi nimefundishwa 1985 mara ya kwanza na IBM wameitoa hii program 1981.

Ni kweli kuhusu Exposure Mkuu.
Unasoma na wanafunzi wa nchi 80 ( wakati huo, sijui sasa).

Imagine upo darasani mnafundishwa namna ya watu wa Lapland (Sami people- wamasai wa Kizungu) wanavyoishi halafu kuna wanafunzi wawili wa Kisami waliozaliwa Sweden na Finland wanatupa live example jinsi wanavyoishi katika misitu yao.

Ilikuwa mara yangu ya kwanza kujua kuna Wasami wapo Sweden, Finland, Norway na Urusi na ni kabila tofauti na wazungu wa nchi zao kitamaduni na kilugha.

They are indigenous people, like Native Americans (USA) au First Nation ( Canada ) au Ainu (Japan).
 
sasa mkuu yote hayo yametoka wapi? Yes you found your happiness in Tokyo. I respect that. That's why nimesema ukisoma shule nzuri Kama IST uwezekano wa kufanikiwa ni mkubwa. But it doesn't mean tuliosoma kayumba wote ni wajinga wajinga........kuna ambao hizo Harvard na LSE tumezisoma vile vile...so....my brother..don't go there.

Saying that I meant well it was just a brotherly challenge.

Asante.

Mkuu,

Sijadharau waliosoma shule za kawaida.

Uliniuluza maswali, nikakujibu.

Naomba usome maswali yako.

Nimekutana na Watanzania wengi nje wamesoma Aga Khan, Shabaan Robert na shule za serikali nje na wana maisha mazuri tu. Wengi wamerudi na kuendelea na maisha yao nyumbani pia.

Kila mmoja na mahesabu yake.

Nia yangu ilikuwa ni kujibu maswali yako tu.

I meant well.
 
Nimefurahi kama inaendelea. Kuna wakati ilisimamishwa nilipokuwa huko.

Graduates wa sekondary niliyosoma karibu kila mwaka wanapata scholarship hapo. Baadae wanaenda marekani kwa degree.
 
Kuna watoto wa mabalozi kama wa Yemen, Korea na Japan. Wanakuja hata maneno matatu ya Kiingereza hawajui.

Wanapelekwa Intensive English Class, baada ya miezi sita, anaongea vizuri kabisa.

Tunapelekwa Model United Nations, Nairobi, kujifunza debating.

Huwezi kumaliza IB2 (form 6) mpaka ufanye masaa 80 ya volunteer work, hapo Salvation Army, kwa Mama Theresa au Katika hospitali yetu ya Kijiji cha Kinduitwi.

Pia, tumepiga rangi wodi za Ocean Road Hospital.

Tunafundishwa kuogelea na kuokoa.

Maktaba haina tofauti na Maktaba ya nchi tajiri. Kuna kila aina ya vitabu na magazines.

Kwa elimu, IST haina mshindani Tanzania.

Naona elimu yao ipo too practical related to the existing global current affairs. Haipo theoretical kama ya bongo.

Vitu unavyopata kule vinakujenga kwenye maisha yako ya kila siku.

Wakati tunasoma secondary hatukuwa na mwanga wa vitu kama hivi, tunakuja kushtuka wenzetu tuliomaliza nao wanaitwa kwa usaili na wanapata scholarship sisi tunarudi kwenye mtaala wa serikali.

Kwasasa najitahidi kwa gharama yeyote mdogo wangu aingie hapo. Na nikiwa na hela nzuri wanangu wote watasoma hapo kuanzia nursery hadi PHD.
 
hiyo fees ya mwaka mmoja kwa nursery unajenga simple house,,,,,,its extremely high

donbeny;
Nyumba huungua moto ikabaki majivu. Msingi mzuri wa elim ya mwanao itamuwezesha kuipoke hiyo ijayo akawa kichwa. Mwanao akisoma vizuri, ni mtaji wa nyumba yako bora baadaye.
Swali la kizushi tu; Jaribu fikiri, una jumba la kifahari lakini mtoto pekee uliye naye akiwa kibaka hapo kitaa, utaifurahia nyumba?? Usilinganishe elim ya mwanao na chochote
 
[h=2]Notable Alumni[edit][/h]
  • Mohammed Dewji - Member of the Tanzanian Parliament
  • Usman Ally - Actor
  • Shamima Bhalloo - President of IST Alumni Association
  • Mariam Naficy - Founder and CEO of Minted, attended IST Elementary
  • Saurabh Khetrapal - entrepreneur
  • Gwamaka Kifukwe - researcher at UONGOZI Institute
  • Walter Kitundu - music composer
  • Mark Latham - music director at The New Hampshire Philharmonic, attended IST Elementary
  • Sue Stolberger - artist
  • Kali Ongala - footballer and coach Azam FC
  • Magdalena Moshi - swimmer
 
Naona elimu yao ipo too practical related to the existing global current affairs. Haipo theoretical kama ya bongo.

Vitu unavyopata kule vinakujenga kwenye maisha yako ya kila siku.

Wakati tunasoma secondary hatukuwa na mwanga wa vitu kama hivi, tunakuja kushtuka wenzetu tuliomaliza nao wanaitwa kwa usaili na wanapata scholarship sisi tunarudi kwenye mtaala wa serikali.

Kwasasa najitahidi kwa gharama yeyote mdogo wangu aingie hapo. Na nikiwa na hela nzuri wanangu wote watasoma hapo kuanzia nursery hadi PHD.

Kila la heri Mkuu.

When there is a will, there is a way!

Best of luck.
 
Graduates wa sekondary niliyosoma karibu kila mwaka wanapata scholarship hapo. Baadae wanaenda marekani kwa degree.

Miaka imepita ila nawakumbuka wawili wa div1 scholarship.

Mmoja alikuwa student president, best orator I've ever met. Alipomaliza, akapata full scholarship Minnesota, USA. Akaja kujiharibia na mambo ya kijinga na kupata deportation. Huyu, hata Raisi angekuwa. He was very gifted.

Mwingine kapata full scholarship, Norway alipomaliza.
 
Hapo ni mwisho wa mchezo.

Nimebahatika kusoma hapo miaka ya 80.

Siku hizi bei yake kubwa mno kama ya kwenda chuo kikuu.

Miaka hiyo ya 80 malipo yake yalikuwaje? Kwa hapa Tanzania, hata gharama za kusoma PhD hazijafikia hapo...
Wanafunzi wanaotoka hapo wanaendelea hatua inayofuata katika shule na vyuo vipi? Kama ni shule na vyuo hivi hivi tulivyosoma sisi akina Kayumba nahisi ni kufuru ya pesa tu...
 
Kaloleni primary school halafu Arusha Sec wakati huo Mkuu ni Mrs Materu halafu Ilboru sec Mkuu akiwa Mr Mushi na gari yake 404...then JKT oljoro and after that UDSM.Chakula kizuri..malazi safi...wakufunzi wazuri.
 
Back
Top Bottom