Nataka kujitolea kufundisha computer subjects | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka kujitolea kufundisha computer subjects

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by mashizo, Aug 15, 2011.

 1. m

  mashizo Member

  #1
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 43
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  wadau kuna plan nafikilia kuja kufundisha masomo ya computer hasa kwa vijana wetu wa shule za msingi,nitaanza mwakani nikiwa hai,nitafundisha bure bila ya malipo,na vilevile nina mpango wa kuzitengenezea baadhi ya shule za msingi websites ambazo maelezo muhimu kuhusu shule husika yatakuwepo hii ni kuendana na teknolojia ya karne ya ishirini na moja

  nawaomba wale watanzania wenzangu ambao mpo fiti kwenye suala zima la computer,mnishauri je huu mpango mzuri au wadau mnanishauri nn kuhusu ili suala?

  nakaribisha maoni yenu wakuu
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ushauri tena mkuu wakati umeshaamua na naona kama umedhamiria?

  Kwa kifupi kufanya any volunteer work (kind of pro bono publico) ni jambo zuri na la kuigwa.

  Nakutakia kila la kheri, ila usikimbili kwenye English Medium school anza na hizi za kina Kanumba hapo ndo utakuwa umesaidia kweli
   
 3. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Basically mpango ni mzuri, ila ungetoa details tungekushauri zaidi. Utaufanikisha vipi huo mpango? Machine, sehemu ya kufundishai utatoa wapi? Utaugharamia vipi huu mpango?
   
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mpango mzuri binafsi nilishajaribu kufanya hiki kitu nikashindwa Nilianzia kwa walimu binafsi wa shule chache za msingi hawakuelewa somo nikhamia kwa kwa diwani nikampa somo kuwa nataka niwapige shule za jirani na uswazik aribu na ninapokaa kila jumamosi niwapige shule Basi zoezi likawa gumu utadhani nilikuwa natafuta ufaya kazi kwamalipo malipo.

  Baada ya mwezi mzima kuonrnise mambo nikakata tamaa.....

  Sasa sijui wewe utaanzaje Sijui uende kwa walimu wakuu bina fsi wa shule za msingi au uende manispaa au....

  Yaaaani kwa kweli ha katika mazingira ya volunteering ni mgumu sana. But usikate tamaa jaribu mbinu utayofnnikisha utujulishe nasi labda inaweza kufanikisha .

  Ukienda kwa walimu binafsi watakumbia hilo suala hawawezi mpaka wizara au halmashauri. labda utafute kamati ya wazazi wa shule fulani uwaeleze.

  vile vile unaweza kuwalenga wanafuzi wa primary ukakuta hata walimu wao wako interested sijui itakuwaje. Maaana nilikutana na kesi hiyo.
   
 5. m

  mashizo Member

  #5
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 43
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  kiufupi ni kwamba nina laptop zangu mbili,nitanunua projector moja,na nitafundisha hizi shule za kata maana ndio tulipotokea huko nazijua shida zao,na kuhusu masomo nitawafundisha basic computer programs,kwa mfano vijana wajue windows aina zote,simple software kwa mfano microsoft office,photoshop ikiwezekana itategemea na uelewa wao wa masuala haya ya computer,ila tatizo lipo kwenye umeme sijui kama hizi shule madarasani kuna sockets za umeme au umeme wenyewe kama vikiwepo basi itakuwa kheri sana.naomba ushauri zaidi wakuu
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwa experince ndogo japo sikufanikiwa anza na walimu kwanza wa primry kwanza. Nadhani ukiwalenga walimu complication zitapungua. then utahami kwa waafunzi may be wa class six and seven. carriculum inayofaa usichague wewe. tafuta carricum wanazofundishwa age group husika kwa shule za majuu.

  Maana caricullum mtu amabye hajui computer aliyamaliza form four ni tofauti na mtu amabye hajui computer ambaye hajamaliza la saba. Na carriculm y mwalimu wa shule ambaye hajawai kugusa komyuta nayo ni tofauti na hao wawili niliowataja mwanzo.
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Kwa Mawazo yangu mimi nionavyo itabidi apate Wafadhili kwani huo mpango anaokusudia ni wa bure lakini una gharama sana sasa atakuwa akifundisha shule moja? au atakuwa akienda kila shule Kufundisha?Na tena mji gani aliokusudia kufundisha? hayo ndio maswali yangu ninauliza.......
   
 8. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Wafadhili wa kazi gani tena mkuu, hii low self-esteem inatoka wapi tena?
   
 9. Kijuche

  Kijuche JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 419
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Endelelea na wito wako kama unaona upo ndani ya uwezo wako mkuu. Kila la kheri.
   
 10. wende

  wende JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kwa hao wa primary hakuna haja ya kwenda majuu kutafuta hiyo mitala ya computer,watafute wadau wa elimu wa hapa bongo watakupa mitala ya kibongo.....kama sijakosea watoto hao wanasoma maswala ya CTI!
   
 11. L

  Lepapalongo Member

  #11
  Aug 17, 2011
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Hili suala jana usiku nilipita mezani nikakutana kajomba kangu anasoma darasa la sita mara nakagua vitabu vyake nakutana na kitabu kimeandikwa TEHAMA nikamuuliza nini hii akasema anko computer.Baada ya kufunua ndani nikakutana programu andishi sasa hapo kuanzia word,excel na masuala ya printa yamechambuliwa hapo ila lugha imebadilishwa kiswahili ya kuna maneno mageni sana kama chatazi,pau n.k kwa hiyo mdau nakushauri tafuta kwanza mitaala hii kwanza then kamua ndo uende huko la sivyo utabaki kusema highlight word badala ya kuumbiza neno {lol!!}.
   
 12. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #12
  Aug 17, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kichakata matini, puku, programu endeshi, wavu wa walimwengu (www) KISARA (kioneshi sanifu rasilimali - url hiyo), mwambaa kazi, rambaza, teua, kitambazo, kisuduru, kichakata mikro, diski tepe, n.k
   
 13. Millah

  Millah JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kaka kwanza nikupongeze kwa kufikiria jambo kama hili, kwa ushauri wangu ungeanza na kuandika plan kamili ya project kuanzia unapotaka kuanza hadi unapokusudia kufika hata kama ni baada ya miaka mitano, hii itakusaidia kuwa na vision na malengo, badala ya kuanza shagahala baghala halafu ndio baada ya mwezi unaacha kwa vile hujui wapi unataka kufikia.

  Baada ya hapo ungetafuta jinsi ya ku-finance "mradi wako" baada ya kutoka kwenye phase ya "laptop mbili" kwenda phase ya pili. Pia kama ungependa uwe ni mradi wa kuendelea fikiria kuwa utahitaji watu kwani huwezi kufundisha shule 10 peke yako, ni vipi utaweza kuwapata sahihi wakushirikiana nao huku wakitambua lengo nini.

  Nisingependa kukuchosha kuandika sana, ila fikiria sana kufanya contact na walimu wa mashuleni, wafanyakazi wa wizara ya elimu na sehemu nyingine husika ili ujue nafasi ya jambo kama hili, waliokushauri masuala ya nini utafundisha wametoa ushauri wa msingi sana badala ya kufikiria kufundisha "basic programmes" kama ulivyosema mwenyewe.

  Mwisho kabisa naomba nikusisitize kuhusu Plan, kuna msemo kwamba "if you fain to plan you are planning to fail". kwa hiyo jitahidi sana plan yako iwe viable na iyenye kuweza kutekelezeka bila ya kutaka mambo makubwa yasiyowezekana, plan ni muhimu na huenda ikawa sababu ya kuvutia wafadhili na watu wakujitolea kuendeleza wazo lako. Nakutakia kila la kheri.
   
 14. mazd

  mazd Senior Member

  #14
  Aug 18, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Computer inahitaji mazoezi so hao wanafunzi ukisha wasomesha na laptop zako then ukachomoka nazo, itakuaje na shule hamna PC-u must me sponsored i thnk-GOOD WORK BY THE WAY
   
 15. HT

  HT JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  jamani mkusanyieni hiyo misamiati na tafsiri yake ili aanza kuzizoea.... Hiyo tafsiri ya URL nimeipenda!
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Very good thread
   
 17. ChelseaBlue

  ChelseaBlue Senior Member

  #17
  Aug 18, 2011
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kuna Mzee mmoja wa Arusha namfahamu nae ana wazo zuri kama lako mkuu, endeleeni na moyo huo huo mtazidishiwa na Mola...
   
 18. SHAROBALO

  SHAROBALO JF-Expert Member

  #18
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Ni wazo zuri sana
   
Loading...