Nataka kujenga kisima cha ardhini cha maji

Nataka kujenga kisima cha ardhini cha maji

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,869
Reaction score
5,170
Wandugu naonaga uchungu sana kuyaacha maji ya mvua ya mapaa yapotee.
Nina mpango wa kujenga kisima cha kukusanya lita laki moja kiwe chini ya ardhi gutters ndio zitakuwa zinakusanya.
Swali je cha umbo gani kinafaa mstatili au mviringo.
Naomba wataalamu wa dams na visima wanipe ushauri mbali mbali je kuna adhari kuwa na kisima cha aina hiyo kwa nyumba za karibu na mengineyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jenga cha round mkuu ndio kiko imara
 
Ahsante kwa ushauri ila ningepata ushauri wa kiinjinia pia maana lita laki moja ni load ya uzito wa tani 100 chini ya ardhi je unene wa ukuta uweje na nitumue mawe au tofali?je nondo najua kwa juu lazima ziwepo je kwa pembeni je?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tumia tofali au zege lenye ratio ya uhakika. Hakikisha unachanganya na water proof cement ili kuzuia maji yasipotelee ardhini. Na hiyo underground tank iwe ya round. Ukishafunika waweza kufunga nira pump kwa juu ili kuchota maji hayo. Au ukaweka submissible pump yenye HP ndogo na ukayapandisha maji kwenye tanki lingine la juu(simtank) la hata lita 5000 au 2000 na kisha haya maji ukayasambaza ndani ya nyumba yako kwa matumizi anuai.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante kwa ushauri ila ningepata ushauri wa kiinjinia pia maana lita laki moja ni load ya uzito wa tani 100 chini ya ardhi je unene wa ukuta uweje na nitumue mawe au tofali?je nondo najua kwa juu lazima ziwepo je kwa pembeni je?

Sent using Jamii Forums mobile app
Pia lita laki moja ni tank kubwa so hakikisha linakuwa na nguzo katikati za Ku support slab yako, otherwise litakuja kushuka
 
Kisima cha chini kilichofunikwa.Bwawa ni changamoto litahitaji area kubwa.Pia litakuwa kama dam ni hatari kwa usalama wa viumbe wengine hasa watoto pia lisije kuwa mazalia ya mbu changamoto ingine evaporation.Changamoto ingine kuchafuka maji
Unataka kuchimba kisima au bwawa?

Sent from my SM-J200F using JamiiForums mobile app
 
Naomba msada wa vipimo vya tank la chini lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita laki moja.
 
Back
Top Bottom