Nataka Kujenga kaghorofa ka ushkaji hivi eneo halijapimwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka Kujenga kaghorofa ka ushkaji hivi eneo halijapimwa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Karhumanzira, Jan 11, 2012.

 1. Karhumanzira

  Karhumanzira Member

  #1
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Habari wadau,
  Ninataka kujenga kaghorofa kadogo tu na kiwanja hakijapimwa,kipo bunju,je utaratibu ukoje? Nijenge tu bila kupima? Je nikaombe kibali cha ujenzi hata kama kiwanja hakijapimwa? Au hairuhusiwi kujenga kama kiwanja hakijapimwa? Au unaweza kujenga tu hata kama kiwanja hakijapimwa sema tu uwe na kibali?

  Ufafanuzi please wadau wa sheria
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu Bunju nafikiri ukienda kwenye ramani za City Master Plan iko kwenye ramani hiyo
  Sawa inawezekana eneo lako halijapimwa ila liko katika mipango ya jiji ya kuendelezwa
  What you can do ni kwamba wasiliana na watu wa Jiji au manispaa uwaambie wazi eneo lako lilipo na unachotaka kujenga na waombe kama inawezekana wakupe ramani ya manispaa ya kinondoni ile master plan uone eneo lako linaangukia wapi
  Usije kujenga wakati kwenye master plan wamesema eneo hilo ni eneo la shule au wazi au wana mpango wa kujenga hospital
  Ukishaona master plan sasa unaweza kuongea nao uwaambie mpango wako na wakupe ushauri cha kufanya maana wanajua namna ya kudeal na viwanja ambavyo havijapimwa
  Kaushauri kidogo pima eneo lako na uwe na hati mkuu maana kujenga nyumba wakati hata hati huna ni hatari nyingine
  Wakija wao wenye manguvu yao wakichukua ardhi yako na huna hata cha kuitetea utapata balaa jingine
   
 3. Karhumanzira

  Karhumanzira Member

  #3
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Asante kwa taarifa mkuu nitafanya hivyo
   
 4. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Karibu mkuu na zingatia ushauri wangu
   
Loading...