Nataka kufungua biashara ya saluni lakini nahofia kuanza kutokana na Corona. Naomba mawazo yenu

palesh pizoo

Senior Member
Apr 14, 2018
131
223
Habari za kazi wapambanaji mimi ni mkazi wa Dodoma mjini nilipoanza mwaka 2020 nliandaa mpango wa kufungua saloon ya kusuka ifikapo mwezi March mwaka huu lakin ilipofika huo mwezi ikawa kumeingiliana na mambo ya Corona hali ikawa sio nzuri nikahofia sananhasa kwa biashara ambayo inaanza nilipata hofu kidogo kutokana na ile hali maana hata walioanza kufanya biashara muda mrefu kwa kipindi hiki walisikika wakilalamikia kuyumba kwa biashara zao na miongoni mwa wafanyabiashara wengi humu wamo.

Ombi langu kwenu naona muda unazidi kuenda na tangu huo muda sijafanya biashara yoyote mpaka sasa natamani kuianzisha maana serikali inatupa imani kuwa corona imepungua.

Je, hali mnaionaje wafanya biashara ambao tayar mpo kwenye biashara muda mrefu na mmepitia kipindi cha korona vip hali ya biashara bado ni ngumu au ahueni? Na je naweza kuanzisha tu biashara yangu kwa sasa?

NAOMBA KUWASILISHA
 
Anzisha biashara,unavyoanza na changamoto ndio unakomaa kwenye biashara husika Covid19 ikiisha utakuwa ume master vizuri na utaona faida yake.
 
palesh pizoo,
Nikujibu kifupi...woga wako ndio anguko lako!

Hii kauli imenipa moyo sana.ubarikiwe mkuu.mimi kuna ka officn kangu kananiingizia kwa siku sikosi elfu 20 lakini nimeitiwa fursa sehemu nyingine ambayo kwa mahesabu ya haraka haraka naweza piga hela hata mara mbili au tatu ya hii ninayopiga huku.

Na hii ya huku sina mtu wa kuweza kuisimimamia ila nina hofu sana je nikienda huko ikibuma?japo sina mpango wa kuifuta kabisa hii ya huku nataka nii suspend tu ila ndo ivo nina hofu sana ya kwenda huko
 
Back
Top Bottom