Leo Msasani amefika Mzee mmoja kutoka Kilimanjaro anasema kwamba amejadiliana na wazee fulani kule,na wanauliza kwa nini watoto wa Nyerere hawataki kugombea Urais,kwa hiyo ameleta ujumbe,anauliza kama yupo mmoja wetu anataka kugombea Urais.
Anasema mwezi wa nane alisoma kwenye gazeti kwamba Madaraka Nyerere anataka kugombea Urais,Je Madaraka bado anataka kugombea Urais? Kama anataka kugombea Urais,basi wazee kule mkoa wa Kilimanjaroa watamuunga mkono. Akaambiwa kweli iliandika katika gazeti kwamba Madaraka anataka kugombea Urais,lakini siyo yeye aliyeandika,yupo mtu mwingine aliandika,na huyu mtu hakutumwa na Madaraka.
Akaniambia hili swala amejadiliana kwa kina na Mama Maria,na Makongoro,na kwamba Makongoro amemuahidi kwamba ataitisha mkutano wa familia kulijadili hili swala. Baada ya kusikia hivyo,yule mzee akaridhika na kuondoka.
Sasa sijui niseme nini. Sidhani kama tutafanya mkutano wowote kujadiliana kama kuna kuna mtu hapa anataka kugombea Urais.
Watu wengi wantaka kuleta mabadiliko katika Nchi. Labda wanataka kuleta education reform,au financial reforms,au kuleta utaratibu wa school lunches,au fair labour relations,au whatever,au kujenga zahanati,au reform katika utendaji kazi wa hospitali;I hope watu wote wanaweza kupata nafasi ya kuleta mabadiliko katika Nchi bila kulazimika kugombea Urais.