Nataka kuchukua fomu kugombea Urais,CCM

Ganesh,

Huoni kwamba Tanzania inakuwa kama ya kisultani sasa? Nasikia wengine wanamuandaa mtoto wa Mwinyi kuwa rais Zanzibar, huyu rais wa sasa wa Zanzibar ni mtoto wa rais wa zamani wa Zanzibar, kweli hakuna wengine wenye uwezo? Au ni usultani tu?

Rais Nyerere mmoja anatosha. Ingawa una haki kikatiba, kung'ang'ania rais lazima awe Nyerere ni kama kutukana watu wengine hawana uwezo.

ukweli ni kuwa watoto wa nyerere tunawapongeza..kwa kutotumia madaraka ya mzee vibaya..hata mama hilo ni jambo la kupongeza!!!...

ambao hamjamuelewa Garnesh...hapa anachochea mada tu...HAPO JUU MKIMSOMA VEMA AMESEMA WAZI KUWA INTEREST YAO...ni kila mtu afanye juhudi kufanya tanzania iwe sehemu nzuri[literally]...its like alivosema kenedy ...dont ask what america can do for you ..ask what you can do for america....ameweka wazi kuwa sio lengo lau kugombea ....zaidi ya kuchochea maendeleo ..

Nataka pia kwa hili tuelewe kuwa hata siku ikitokea katika kizazi cha mwalimu ...iwe mjukuu au kitukuu amekuwa rais nchi hii[kumbukeni hili linaweza kuja kutokea ]...itakuwa ni kwa uwezo wake mwenyewe....na wala si kubebwa...tofauti na sasa hao mliotaja wote wamebebwa na baba zao.....karume alipomaliza form six ....temporary employment aliyoifanya ni kuwa KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA....waziri akiwa baba yake...
HUSSEIN mwinyi....pia amesaidiwa sana na influence ya BABA yake ni vema sasa akasimama mwenyewe kama HUSSEIN.....ili hata siku akifanikiwa mafanikio yake yasiusishwe na kubebwa....
Mliona hata kenya KENYETTA UHURU alibebwa na MOI.kama shukrani kwa mzee wake kwa kumpa urais na kuwaacha wakikuyu.....Lakini wananchi wakamkataa ...wakamuambia kama aanataka urais ajipange agombee kwa uwezo wake...na for sure he will become president next time maana sasa anasimama mwenyewe.....
 
Ndugu Mchukua fomu, Hebu kamilisha basi unachotaka kusema. Je wewe unataka kuchukua fomu tu au lengo lako ni kugombea u-Rais ?. Kama kuchukua fomu sioni tatizo, si uta-file kama kubukumbu na wewe uliwahi kuchukua fomu.
Lakini kama unataka kugombea kuwa Rais, nina hakika hujajiandaa kabisaaaaa-huna matayarisho yeyote kwa hii 2010, labda jaribu 2015 na uanze matayarisho sasa. Uchaguzi huu wa 2010 uwe darasa lako la kuanzia matayarisho.
 
Nimefikiria kuchukua fomu kugombea Urasi kwa tiketi ya CCM. Nimeuliza tayari,naambiwa kadi lazima uwe nayo miaka mitano kabla ya kugombea uongozi katika Chama.

you hav to be out of your mind - gombea udiwani kwanza.
 
Nimefikiria kuchukua fomu kugombea Urais kwa tiketi ya CCM.

Nimeuliza tayari,naambiwa kadi lazima uwe nayo miaka mitano kabla ya kugombea uongozi katika Chama.

Mkuu Andrew Nyerere, kwanza nikupongeze kwa uamuzi huu. Naona kama unasita na kama umekutana na kikwazo cha kadi. Kwani kadi yako ina umri gani?Pia kama utagombea kwa tikiti ya CCM utafanyaje kukihuisha chama?Maana mimi naamini kuwa CCM njema na bora ilishapotea baada tu ya kifo cha baba yetu mwl Nyerere. Pia ukiweza hapo naamini kuwa spirit ya Unyerere itarudi kwa kasi ajabu. Umejipangaje kuhuisha roho ya uzalendo?
 
Last edited by a moderator:
Kumbe nini,unatoa maoni kuhusu vitu usivyofahamu. Unadhani tutaogopa kuchukua fomu kwa sababu Mnajimu amesema kuna majini yatatushambulia,kwa sababu Mnajimu amesema,''kama huniamini kachukue fomu.''

Safi sana mkuu. Miongoni mwa mambo yaliyomweka Mwl Nyerere salama ni kumuamini Mungu. Nami mchungaji wako nakuombea.
 
Back
Top Bottom