Nataka kuagiza Toyota Allex ya mwaka 2003, nimekwama kwenye kipengele cha Diesel or Petrol

Mlolongo

Senior Member
Jul 4, 2019
144
225
Nimejaribu kufuatilia ubishano wa gari ipi nzuri kibongo bongo kwa mtu wa kipato cha chini, kati ya Diesel na Petrol. Nimekuta watu wanabishana tu.

Wengine wanasema Diesel inatumia fuel kidogo kuliko Petrol.

Wengine wanasema gari za Diesel zina gharama sana kwenye maintenance.

Wengine wanasema Petrol ipo juu sana (gharama za wese zinafilisi)

Wakuu, kwani wabongo wengi wa kipato cha chini wanatumia magari ya Diesel au Petrol.
Naperuzi website ya Befoward hapa nimekwama hicho kipengele.
 
ilonga

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
1,018
2,000
Kwa Toyota Allex, sidhani kama utapata ya kutumia diesel. Hata hivyo, gari za 1500cc kushuka chini si za kuumiza vichwa kuhusu consumption. Kama upo tayari kuagiza gari toka Japan kwa milioni 12, sidhani kama utashindwa kuligharamia mafuta kwa kiasi cha sh laki 1 hadi 1.5 kwa mwezi kwenye mafuta.
 
Glenn

JF-Expert Member
May 22, 2018
9,196
2,000
1. Hakuna gari ya Allex inayotumia diesel
2. Kwa uzoefu wangu ninatumia gari ya diesel na petrol pia
TOFAUTI ZAO..diesel
a) Gari ya diesel ni gari ngumu, nyingi zina 4w hivyo utaenda popote majira yote
B) wese ni kawaida mengi yanaenda 10km /lita.
C) spare ni ghali japo inategemea aina ya gari lakini zinadumu hasa org hivyo ni ghali lakini ukichunguza vizuri sio ghali kwani zinadumu.
Mfano mimi tangu 2017 sijawahi nunua shock absorber wakati mtu wa Allex huenda amenunua zaidi ya mara 4
D) Gari ya diesel haichsnganyi mwendo kwa haraka lakini ikikolea ni tamu kwani nzito haiyumbi

Gari za petrol
1. Zafaa zaidi mijini hazina 4w, kwa watu wa masafa na pori kama mimi hazifai kwani hazimudu
2. Nyingi zinatumia lita 1 kwa 12km
3. Zinachanya mwendi haraka
5. Nyingi spare ni fake sana hasa toyota, inahitaji uzoefu kukwepa hili vinginevyo maduka ya spare yatakuwa sawa na nyumbani.

USHAURI WANGU
Nunua gari ya ndoto yako, uishi maisha yako.
Wabongo tumejaa ujuaji tena wa kuambia sio kuwa tunajua au tu wazoefu.
 
Nzi

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
13,830
2,000
D) Gari ya diesel haichsnganyi mwendo kwa haraka lakini ikikolea ni tamu kwani nzito haiyumbi
Mzee,unazungumzia diesel engines za kizamani! Siku hizi diesel cars zina vavavooom kwa haraka tu.
 
Brodre

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,267
2,000
1. Hakuna gari ya Allex inayotumia diesel
2. Kwa uzoefu wangu ninatumia gari ya diesel na petrol pia
TOFAUTI ZAO..diesel
a) Gari ya diesel ni gari ngumu, nyingi zina 4w hivyo utaenda popote majira yote
B) wese ni kawaida mengi yanaenda 10km /lita.
C) spare ni ghali japo inategemea aina ya gari lakini zinadumu hasa org hivyo ni ghali lakini ukichunguza vizuri sio ghali kwani zinadumu.
Mfano mimi tangu 2017 sijawahi nunua shock absorber wakati mtu wa Allex huenda amenunua zaidi ya mara 4
D) Gari ya diesel haichsnganyi mwendo kwa haraka lakini ikikolea ni tamu kwani nzito haiyumbi

Gari za petrol
1. Zafaa zaidi mijini hazina 4w, kwa watu wa masafa na pori kama mimi hazifai kwani hazimudu
2. Nyingi zinatumia lita 1 kwa 12km
3. Zinachanya mwendi haraka
5. Nyingi spare ni fake sana hasa toyota, inahitaji uzoefu kukwepa hili vinginevyo maduka ya spare yatakuwa sawa na nyumbani.

USHAURI WANGU
Nunua gari ya ndoto yako, uishi maisha yako.
Wabongo tumejaa ujuaji tena wa kuambia sio kuwa tunajua au tu wazoefu.
zipo mkuu mimi nishaiona moja hapa mlimani city nyeusi labda kama jamaa alifanyia manjonjo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom