Nataka kuacha kazi

Maamuzi sahihi kabisa, kwa kweli ukigonga 40 bado unategemea ajira majanga.
 
aisee mnanitamanisha na mimi niache kibarua changu! maaana malengo yanazidi chelewa
 


Mkuu Malila, mwaka huu nitakutafuta kwenye mambo ya shamba.
 
Si kazi kuacha kazi bali kazi kupata kazi, tunatafuta kazi wewe unaacha kazi,think twice,nyaka mil 500 ndo uache kazi

Hajasema anaacha kazi ili akakae nyumbani kwake bila kazi, nilivyomwelewa mimi ni kwamba, anabadirisha kazi, nijuavyo mimi, kazi anayokwenda kuifanya ni ngumu zaidi na inahitaji kujituma zaidi na tija yake ni kubwa, kazi ya sasa anayofanya, anajituma kwa kiwango cha kumridhisha bosi wake,ni ngumu kwa sababu inamnyima uhuru na tija yake kwake ni ndogo, kibaya zaidi umri unakwenda.

Kwa ufupi ni kwamba, mafanikio ya kazi anayofanya kwa sasa ni mali ya mtu mwingine, yy huambulia bonus. Mafanikio ya kazi anayokwenda kuifanya ni yake yeye kama yeye, na kinyume chake ni sahihi. Kajipima kaona bora akajitume.
 
Woga ni dhambi kubwa kuliko hata kuua, Endelea na mawazo yako mazuri.
 
Unasumbuliwa na woga.
Woga wako ndio umaskini wako.
 
do you have guts? if yes do.............otherwise it is petty talk.
 
Nimelelewa mazingira ya kujiajiri nakaza huko huko. Sema ikitoka opportunity ya UN aisee nitaacha private investment ziendeshwe na ndugu zangu ambao wapo kwenye bizness zetu na kupata exposure kidogo.
Tatizo la private bizness ni kutopata exposure hasa za kusafiri!
 
Ndugu yangu hongera kwanza kwa kufikiria hilo mm nilishaquit zamani nilifanya 4.5yrs na sasa niko pazuri sana. Ushauri wangu ni huu ulipotarget kupata mil300 ni mbali sana na unaweza usifike kirahisi. Ila mm nilitumia formula hii; km naweza zalisha pesa sawa na mshahara net nikiwa bado utumwani basi inanitosha sana kuondoka nikaemploy nguvu zangu zote. So inawezekana tu kaza buti. Halafu ukijiajiri utajua kuwa economy kwani ulichopata leo hutakitumia ovyo kwani hujui kesho kutakuwaje. Walioajiriwa huwa hata wanaoverspend kwani wanajua mshahara unakuja tar zile ishirini naaa... So kaza buti!

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
Kaka hilo wazo la msingi. Mimi pia nimespecialize kwenye mipango na miradi ila cha muhimu uangalie nini utakuwa unaingiza kwa siku katika private investment kiasi kwamba turnover yako isiwe chini ya matumiz yako pamoja na familia. Pamoja na wazo hilo mimi nakushaur uliendeleze zaid kwan ajira huru inakufanya uamue how much to produce in relation to market tofaut na kaz ya kuajiriwa ambayo mshahara unakuwa constant for long time and no room to add more. Kama vip tutaftane kaka
 

Mkuu wazo lako ni zuri saana na binafsi nadhani uzip huu ulipaswa kuuweka Jukwaa la ujasiriamali kule ungepata mawazo mazuri saana ya namna ya Kuchoma meli moto. Kwa mtazamo wangu naami sasa ni muda wa kufanya maamuzi hayo kuliko kuendelea kupoteza hiyo elfu 80 au 100,000 ambazo ni pesa ungeweza kuingiza katika miradi na wewe kuweza kuisimamia kwa umakin zaidi.
Ni hayo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…