Nataka kuacha kazi, ushauri unahitajika

Nataka kuacha kazi, ushauri unahitajika

doppla2

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
1,393
Reaction score
1,462
Direct to the point

Nataka kuacha kazi serikalini, niko kwenye process za ajira mpya, taasisi binafsi katika mkoa mwingine .

Ila nina mkopo unaondelea bank ya CRDB na makato mengine kama ya HESLB .

Sijamshirikisha HR wetu wala watumishi wenzangu coz sitaki wafahamu jambo hili wakaanza nichanganya.

Sasa ,wakuu naombeni kushirikishwa uzoefu wenu,katika maamuzi kama haya mambo yapi ya msingi kuzingatia?

Pili ni jinsi gani mabenki yanavyo handle madeni kwa mwajiriwa anayeacha kazi na kwenda kwenye kazi nyingine?

Karibuni sana wakuu

Natanguliza shukrani

Regards
 
CRDB wataendelea kukukata kwa maana lazima tu mwezi ukipita wakutafute, ila bodi ya mikopo sina uhakika maana mpaka waanze tena mchakato wa kukutafuta.
 
Lipa kwanza mkopo na wenzio wafaidikee Mkuu usikachee wajib wako
 
CRDB wataendelea kukukata kwa maana lazima tu mwezi ukipita wakutafute, ila bodi ya mikopo sina uhakika maana mpaka waanze tena mchakato wa kukutafuta.
So, huko ntakakokwenda itabidi nijisalimishe kwenye matawi yao au ntakua napeleka cash dirishani?
 
Unataka kuacha kazi serikalini na uko kwa process ya ajira nyingine. Kama bado ni process usikurupuke kuacha. Subiri hadi wakupe mkataba ndo uache serikalini. Vinginevyo lolote laweza tokea.
 
Hakuna kitu kizuri kama ajira ya kudumu inayokupa uhakika wa kula na kunywa maisha yako yote!
 
Huo mkopo umeufanyia nini mpk hutaki kulipa, pia nani kakuambia ukija private hutakatwa malipo ya HESLB, pia kumbuka unaakiba mfuko wa jamii ambayo itazuiwa.
Ushauri kama unataka kuja private basi makosa uliyofanya ya huko usiyarudie (mkopo usio na tija), pia ukumbuke huku contract term niya mda mchache so inabd uwe mjanja ukikopa unafanya cha maana ili siku ikibuma basi unaendeleza maisha.
 
Sikushauri sana kuacha kazi na kwenda sector binafsi huku ni kichomi ndugu yangu hata kama utavutiwa na dau nono ila hakufai hata,uliza kwanza tuliopo huku tunataman hata kesho tuondoke ila njaa ndo tatzo
 
Lipa deni kwanza, mwajiri wako hatokubali uache kazi (kama utafuata utaratibu wa kuacha) wakti una deni ambalo alikudhamini, pia itakupotezea uaminifu iwapo utahitaji kukopa tena.

Mie niko kwenye hatua za kuachana na ajira ili nisimamie vizuri mishe zangu,

lakini nasubiria kamkopo kaishe (ambako nilikachukua kukazia mishe zangu) pamoja na sababu nyinginezo

Pia usijerogwa ukaacha kazi bila ya kuwa na uhakika na kibarua kingine
 
Ukiacha utupe mrejesho mkuu nasi tu replace position hiyo
 
Huo mkopo umeufanyia nini mpk hutaki kulipa, pia nani kakuambia ukija private hutakatwa malipo ya HESLB, pia kumbuka unaakiba mfuko wa jamii ambayo itazuiwa.
Ushauri kama unataka kuja private basi makosa uliyofanya ya huko usiyarudie (mkopo usio na tija), pia ukumbuke huku contract term niya mda mchache so inabd uwe mjanja ukikopa unafanya cha maana ili siku ikibuma basi unaendeleza maisha.
sheria ya mifuko ya jamii inakataa,huwezi ukazuia mafa ya mtu kwa kuwa ana mkopo ktk taasisi ya fedha
 
Pata ajira mpya then contact benki kuwafahamisha kwa vile mwajiri wako ndo alikuwa guarantor wa mkopo,utaendelea kukatwa kupitia mwajiri mpya.Heslb ni kumfahamisha mwajiri wako mpya afanye makato.
 
Lipa deni kwanza, mwajiri wako hatokubali uache kazi (kama utafuata utaratibu wa kuacha) wakti una deni ambalo alikudhamini, pia itakupotezea uaminifu iwapo utahitaji kukopa tena.

Mie niko kwenye hatua za kuachana na ajira ili nisimamie vizuri mishe zangu,

lakini nasubiria kamkopo kaishe (ambako nilikachukua kukazia mishe zangu) pamoja na sababu nyinginezo

Pia usijerogwa ukaacha kazi bila ya kuwa na uhakika na kibarua kingine
mikopo ina riba
 
mkuu mtia mada hamna kinacho haribika zaidi ni kutoa taarifa makato yanahamishwa,vilevile bado unaweza endelea na mfuko wako wa hifadhi uliokuwa nao
 
Back
Top Bottom