Nataka kuacha kazi - Msaada wa kisheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka kuacha kazi - Msaada wa kisheria

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Ozzie, May 30, 2011.

 1. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Habari wakuu,

  Mimi nimekuwa nafanya kazi na wajerumani katika mradi fulani hapa Tanzania. Niliajiriwa nao pindi tu nilipomaliza degree ya kwanza, bahati nzuri baada ya kukaa nao kama miezi nane tu (2007) nikapata bahati ya kwenda kusomea degree ya pili kwa muda wa miaka mitatu (mambo ya Afya).

  Nilipata udhamini wa DAAD, ( ambapo huyu mwajiri anawafahamu watu wa DAAD (Wajerumani wenzake) hivyo alinikingia kifua; Na nikapata nafasi ya udhamini kirahisi sana).

  Kabla sijaondoka mwajiri aliniingiza kwenye mkataba wa kufanya nao kazi kwa miaka mitatu baada ya kumaliza masomo au kulipa kiasi kinacholingana na udhamini. Kwa kuwa nilikuwa desperate kwenda kusoma wala sikuhoji sana ule mkataba.

  Mdhamini niliyempata alinilipia kila kitu cha shule kwa miaka miwili, mwaka wa tatu huyu mwajiri wangu alinilipia ada (kama 12,000,000/=), lakini 50% ikakatwa kwenye mshahara wangu na 50% alichangia mwenyewe.

  Muda wote nikiwa masomoni, nilikuwa nikilipwa nusu mshahara na huyu mwajiri, akidai hiyo ndiyo policy yake ( lakini pale anapotaka kunibana kwa vitu vingine huwa anatumia policy za serikali.

  Nimerudi kazini mwaka jana mwezi wa tisa, tukaanza kushindana kuhusu mshahara baada ya kuniongezea pesa kiduchu. Amekataa kabisa kuniongezea mshahara, akidai ananilipa sawasawa na scale yangu, japo kuna vijana wenye degree moja ambao walikuja kazini baada ya mimi kuajiriwa wanalipwa mara mbili yangu (Sielewi hiyo scale ikoje, maana sijawahi iona).

  Wiki iliyopita nimemwambia ninataka ni resign, ambapo anaonesha kutokubali hata kidogo, japo mwisho wa siku itabidi iwe hivyo.

  Kwa sasa anapiga hesabu ya kiasi anachonidai ili kuni release.

  Kuna vitu kadhaa vinanipa utata:

  1. Ilikuwa haki kwa mimi kulipwa nusu mshahara kwa miaka yote mitatu?

  2. Ninaamini huyu jamaa atahesabia udhamini wa DAAD kwenye malipo anayotaka arudishiwe, je ni sahihi (naamini siyo sahihi) maana DAAD
  sikuingia nao mkataba wowote zaidi ya kuji commit kufanya kazi Africa kwa miaka mitatu.

  3. Hivi ninaweza daiwa hata huo nusu mshahara niliokuwa naupata kwa miaka mitatu nikiwa shule?


  Wasalaam
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Inategemea mkataba wako wa kazi unasemaje kuhusiana na ulipwaji wa mshahara kama ukienda kusoma. Umeshasoma mkataba wako na maandiko mengine yanasemaje?

  Hao ambao wanalipwa zaidi yako japokuwa wana degree moja, ni makubaliano yao. Lakini if they are doing exactly the same job you're are doing, then kunaweza kuwa na issue ya equal pay. Nakushauri soma mkataba wako kwa makini.

  Pia soma other correspondences between you and your employer tokea uanze kazi. Kabla ya ku-resign ningekushauri utafute ushauri wa kisheria toka kwa mtaalaamu wa mbambo ya sheria za ajira. Mtafute mwanasheria aliyebobea wenye mambo ya sheria za ajira na sio lawyer tuu wa kawaida.

  Au ukimpata mtu ambaye ana experience kubwa na mambo ya human resources anaweza kukupa mwangaza. Don't resign without getting legal advise on the implications resigning.

  Umeshapata kazi nyingine au unaresign ili ukatafute kazi? If that is the case huyu mwajiri yuko tayari kukupa reference nzuri?

  There is a lot of things to think.
   
 3. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  He, weye una bahati; sisi tunaofanya kwenye NGO za wazungu; ukienda kusoma muda Kama wako mshahara stop, kwani lazima wareplace nafasi yako!

  Pia ukirudi unaapply kazi upya! Wakikupeleka wenyewe, mshahara ni kama robo hivi! Inategemea maelewano, pia u must work at least 2 yrs! Ndio waweza acha!

  Hilo la mshahara; imekuwa kasumba ya mashirika mengi, wafanyakazi wapya kulipwa vizuri kuliko wenyeji!

  Soma policies zenu; then mshirikishe mwanasheria!
   
 4. Caren

  Caren JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2011
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Pal,
  First of all you are lucky ulifanya masomo for two years under nusu mshahara. Many cant. Ila pia huwezi jua mikataba mliyosaini inasemaje? For a small consultation fee you can easily get a lawyer who can advice you on the best approach to terminator/resign from your post.

  You can PM me if you so desire.
   
 5. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  asante mkuu.
   
 6. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  asante mkuu
   
 7. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  nashukuru kwa ushauri. Nitakutafuta
   
Loading...