Nataka kadi ya CCM rasmi

fanya haraka kama unaona ndio kupigana nao au kuwapongeze, maana unaweza ukawa huko na ukajiona unaitwa kila wakati kutokana na maneno yako kwa CHAMA CHA chao mwenyewe, lakini sio wewe mwezangu na mimi, mwenyewe ni wakina Malecela, mwenye nacho sio wewe unajidanganya wewe
 
Mpeni chama mbadala basi kama hamtaki ajiunge na CCM. Kwa ambao hawataki ajiunge na CCM mnamshauri ajiunge na chama gani? Mimi binafsi so far sijaona chama chochote ambacho I'm willing to commit to. Labda watu mnaweza kutusaidia hata na sisi wengine kujua wapi pa kwenda.
 
bwana burn ni wewe ndo mheshimiwa Lwakatare au? maana tuliambiwa ataingi ukumbini.. karibu.. lkn la kushangaza nahisi tayari jamaa washakubadilisha kabla ya wewe kuwabadilisha maana tumezowea kuona kina Tambwe,Salum msabah,Kabouru,Lamwai wakibadilishwa halafu ndo wanajiunga na CCM RASMI.. wakowapi? hongera Kwa mafisadi kukunua..

Mkuu mimi ni Burn wala si huyo unayedhani na nikukumbushe wakulu hapa hawaruhusu ku speculate identity za members. Du hiyo ya kununuliwa nayo ni kali sana, hivi ndugu zangu hadi lini mtaendelea kuwapa nguvu hawa mafisadi?mnadhani wana uwezo wa kumnunua kila mtu? kwa taarifa yako mimi sio target yao na hata wale ambao ni target yao wengi tu wamewashindwa na nakuapia kwa mungu wapo watanzania ambao hawanunuliwi kwa fedha za mafisadi.
 
Burn at least wewe unaelekea maan wengi wetu tumebaki kukinyooshea kidole khuku tumesimama mbali CCM wako hivh CCM iko vile but no one dares to do anything.

Wengi wetu pamoja na kuyaanika makosa, maovu na uozo wa CCM bado tumekiri kuwa hatuna Chama pinzani chenye uwezo wa kupambana na Chama hiki cha mafisadi. Matokeo yake tunaishia tu kulalamikia wananchi na upofu wao katika kukichagua chama CCM.

Bora yako ambaye umeamua kuitumia haki yako ya msingi ipasavyo. Ni matumaini yangu kuwa ukishajiunga na CCM hutaungana nao katika UFISADI na uozo wote unaotajwa bali utasaidia, utapigana katika kukibadilisha kwani umeshajua ugonjwa wake.

wewe ni shujaa miongoni mwa mashujaa wapigao kelele bila vitendo.

Kila la heri, ukihitaji msaada usisite kluwa wazi.
 
Need I say more? you nailed it to the wall
 
Umejidhatiti vipi kuyakabili mapapa ya CCM?

Umejidhatiti vipi kuyashinda waliyoshindwa waasisi wa CCM?

Umejidhatiti vipi kuhakikisha hulali kama wanasiasa machachari wa CCM (waliojitokeza/ wanaojitokeza/wakafanya waliyofanya, watajitokeza baadae kama ulivyojitokeza wewe) na bado wakaanguka chali aidha kwa tamaa mbali mbali au mfumo wa CCM?

Umejidhatiti vipi kuhakikisha hutatuchosha kwa kuwafadhili wapinzani kama ulivyodai hapo juu ukiwa ndani ya CCM?

Umejidhatiti vipi hurudi (ukinyonga) huku utokako kisa uendako ukakukuta ni kubaya au kuzuri zaidi? (Tutakupokeaje? Kwa makofi au kutuandikia humu mkekani kwamba unatafuta pa kuingia tena?)

All in all umejidhatiti vipi kuhakikisha mizani ya UWILI wako na CCM hautalilia kwako?

Nani kakudanganya kiumbe wewe mabadiliko na maendeleo huletwa ukiwa TU ndani ya chombo cha kilicho madarakani? (Mbona kwa miaka zaidi ya 40 ya uhuru hatujayaona?

Nani kakudanganya kiumbe wewe ukiwa kigeu geu/ kutokua na msimamo na kutojua ufanyalo ndio njia ya mabadiliko?

Nani kakudanganya kiumbe wewe CCM atatawala milele Tanzania hii?

Nani kakudanganya kiumbe wewe CCM itang'olewa na mtu kama wewe usie na msimamo?

(Samahani kama kuna tusi au lugha inayoweza mkwaza mtuhapo juu) " We dare to talk openly"
 
Mpeni chama mbadala basi kama hamtaki ajiunge na CCM. Kwa ambao hawataki ajiunge na CCM mnamshauri ajiunge na chama gani? Mimi binafsi so far sijaona chama chochote ambacho I'm willing to commit to. Labda watu mnaweza kutusaidia hata na sisi wengine kujua wapi pa kwenda.

Hapo ndipo point yangu ilipo MwanaFA kwani mara zote nilipokuwa nikianzisha mjadala wa chama mbadala wengi waliniita msaliti. Nadhani kungekuwa na mbadala nisinge ishia huku ila nimeamua na kwa kujua kuwa wapo wengi wenye nia kama yangu nitakwenda kufight from within.
 
Watu wengine wanaogopa kuisupport CCM simply because wanaogopa kuonekana wana tetea mafisadi. Sasa kama mtu anapinga CCM ni lazima aseme mimi naona chama hiki ndiyo bora kwa sababu hizi. Sasa simply kusema CCM haifai ina saidia nini? Siasa zetu bado zina tegemea vyama. Bado wananchi wanabidi wapinge kura kuchagua chama kimoja ama kingine kiingie madarakani na kuongoza, hiyo haikwepeki. Sasa kumuambia tu mtu usichague CCM wakati hauja muambia asupport chama gani au kwanini ndiyo yale yale watu kujaa kwenye mikutano ya hadhara ya upinzani na bado kuishia kuchagua CCM. Fine CCM is not the right party, which one is? Bora Burn kasema ana kiunga chama gani na katoa sababu zake na wengine semeni basi vyama gani mnaviunga na kwanini.
 
(Samahani kama kuna tusi au lugha inayoweza mkwaza mtuhapo juu) " We dare to talk openly"

Hakuna haja ya kuomba samahani mkuu maneno yako yamenyooka sawia na siamini kama kuna mtu atakwazika nayo. Ila tu huwa sipendi kurudia rudia maneno yangu nakuomba tu rudi soma vizuri post ukielewa ndio rudi omba radhi kwa kukurupuka kujibu hoja zenye majibu tayari.
N:B
Surprise!!!mimi natamani kuona chama kingine kikichukua uongozi wa nchi hii kwani naamini hiyo ndiyo mbegu ya kujenga CCM imara na safi.
 
No wonder this country is where it is today, auhitaji toba to act responsibly, vote retrospectively and be a man who changes stuff!
 
Najua mtanishangaa lakini nimepata ufunuo kuwa mabadiliko ya haraka yatawezekana iwapo tu nguvu hiyo inatoka CCM(sijasema hayawezekani ila nimesema ya haraka). Kwa wanaofuatilia muelekeo wa siasa za nchi hii nguvu hii ya mabadiliko imekwisha anza kujidhihirisha, matukio ndani ya chama na kwenye serikali yanatoa taswira ya mafanikio muda si mrefu cha msingi ni kuongeza nguvu ndio maana nimekata shauri nachukua kadi. Siri za vyama vya upinzani zilizo mezani(za kufadhiriwa na CCM) na zilizo gizani ni dalili ya kuendelea kuchoshana tu huku watu wetu wanaendelea kuteseka kwa njaa,umasikini, kukosa elimu bora, huduma bora za afya na mateso yanayotokana na CCM hovyo, siwezi kusubiri vyama vya upinzani vibadilike huku nikishuhudia hayo nawafuata akina NAPE,JERRY na vijana wengine machachari tuinyoroshe CCM.
Nani yupo pamoja nami???????
Mkuu nimeona mantiki yako. nadhani ni rahisi kuwadhoofisha hawa kutokea ndani, nakuunga mkono
 
Umejidhatiti vipi kuyakabili mapapa ya CCM?

Umejidhatiti vipi kuyashinda waliyoshindwa waasisi wa CCM?

Umejidhatiti vipi kuhakikisha hulali kama wanasiasa machachari wa CCM (waliojitokeza/ wanaojitokeza/wakafanya waliyofanya, watajitokeza baadae kama ulivyojitokeza wewe) na bado wakaanguka chali aidha kwa tamaa mbali mbali au mfumo wa CCM?

Umejidhatiti vipi kuhakikisha hutatuchosha kwa kuwafadhili wapinzani kama ulivyodai hapo juu ukiwa ndani ya CCM?

Umejidhatiti vipi hurudi (ukinyonga) huku utokako kisa uendako ukakukuta ni kubaya au kuzuri zaidi? (Tutakupokeaje? Kwa makofi au kutuandikia humu mkekani kwamba unatafuta pa kuingia tena?)

All in all umejidhatiti vipi kuhakikisha mizani ya UWILI wako na CCM hautalilia kwako?

Nani kakudanganya kiumbe wewe mabadiliko na maendeleo huletwa ukiwa TU ndani ya chombo cha kilicho madarakani? (Mbona kwa miaka zaidi ya 40 ya uhuru hatujayaona?

Nani kakudanganya kiumbe wewe ukiwa kigeu geu/ kutokua na msimamo na kutojua ufanyalo ndio njia ya mabadiliko?

Nani kakudanganya kiumbe wewe CCM atatawala milele Tanzania hii?

Nani kakudanganya kiumbe wewe CCM itang'olewa na mtu kama wewe usie na msimamo?

(Samahani kama kuna tusi au lugha inayoweza mkwaza mtuhapo juu) " We dare to talk openly"

Duh wewe unamkatisha tamaa mwenzio ila kumbuka hata Mwalimu Nyerere kipindi kile cha Ukombozi wa Taifa alikuwa akikashifiwa kwa kuonekana kuwa hawezi lakini alikaza buti.

Tunakubali kuwa CCM haitatawala milele but kwa sasa hatuoni chama chochote cha upinzani kinachotuma matumaini ya kuiona hatma ya CCM kesho!! wote tunakiri kuwa upinzani Tanzania bado mchanga!

Simtetei ila unaposema Burn hana msimamo una maanisha nini? Pengine ndio kaupata msimamo sasa hivi au!
(Joke)
 
Najua mtanishangaa lakini nimepata ufunuo

Unajuaje tutashangaa ? Kwanza, CCM ndio kimbilio la wanafiki na mafisadi na huko ndiko wanakopata hifadhi. Pili, maadamu umepata ufunuo wahi ukate hiyo kadi maanake huku nje muda si mrefu hutabaki salama.

kuwa mabadiliko ya haraka yatawezekana iwapo tu nguvu hiyo inatoka CCM (sijasema hayawezekani ila nimesema ya haraka).

Kama hayo mabadiliko hayakuweza kupatikana katika kipindi cha miaka karibia hamsini, kwa nini Burn leo hii aweze lililoshindikana - una nguvu gani ? Hivi sasa ni miaka miwili toka orodha ya mafisadi imetajwa na wote bado wamejaa tele kwenye uongozi ndani ya CCM na wewe uko nje - hicho hicho unachokikimbilia huko ndicho kinachowafanya wazidi kukumbatiwa huko.

Kwa wanaofuatilia muelekeo wa siasa za nchi hii nguvu hii ya mabadiliko imekwisha anza kujidhihirisha, matukio ndani ya chama na kwenye serikali yanatoa taswira ya mafanikio muda si mrefu cha msingi ni kuongeza nguvu ndio maana nimekata shauri nachukua kadi.

Kwetu wengine tunaofuatilia muelekeo wa siasa za nchi hii hayo unayoita nguvu ya mabadiliko ya kuridhisha hatuyaoni zaidi ya usanii. Hebu tueleze hayo matukio ndani ya chama na serikali yanayotoa taswira ya mafanikio. Serikali iliwekwa madarakani na asilimia 80% ya wapiga kura, ni nguvu gani zaidi yahitajika kuongezwa - ya Burn kwa kutaka kadi ya CCM rasmi ?

Siri za vyama vya upinzani zilizo mezani(za kufadhiriwa na CCM) na zilizo gizani ni dalili ya kuendelea kuchoshana tu huku watu wetu wanaendelea kuteseka kwa njaa,umasikini, kukosa elimu bora, huduma bora za afya na mateso yanayotokana na CCM hovyo,

Je, vyama vya sasa kufadhiliwa na CCM, huku wananchi wakiendelea kuteseka kwa njaa, umasikini, kukosa elimu bora, huduma bora za afya na mateso yanayotokana na CCM hovyo, ni sababu tosha ya kutufanya kujiunga na CCM ? Kama CCM inaweza kubaki ovyo pamoja na kelele za wachache upinzani, itakuwaje wote tukijiunga CCM ?

siwezi kusubiri vyama vya upinzani vibadilike huku nikishuhudia hayo nawafuata akina NAPE,JERRY na vijana wengine machachari tuinyoroshe CCM.

Kwa nini usubiri vibadilike na usiungane nao kuwabadilisha na badala yake unajiunga na CCM unayoita ovyo kuibadilisha. Unasema unawafuata NAPE, JERRY na vijana wengine machachari - hawa wamefanikiwa nini cha kujivunia ndani ya CCM.

Nani yupo pamoja nami???????

Wewe na yeyote aliye pamoja nawe ni watu wa kuogopwa kama ukoma. Kinachowavutia huko ndicho wengi tunachokipigia kelele - uozo ndani ya CCM.
Manyang'au hujikusanya kwenye mzoga, ole wao mzoga ukiisha.
 
Burn tunakuunga mkono. Endeleza mapambano mzee. Ila jihadhari huko kwenye uwanja mpya. Siyo wote watakaokupigia makofi watakuwa upande wako. Wengine watakuwa wanakuwinda kama kwale msituni. Jichunge! Safari njema!
 
Ndio demokrasi hiyo umefanya uamuzi sahihi kabisa. Hata Mwalimu RIP alisema " Bila ya CCM imara nchi itayumba"
 
Kadi ya sisi M? sijui niliitupa ch***i vile mwaka 84/85 sijui nije nende nikutafutie vile?
After all sitaki kukisikia hata harufu yake, achilia mbali sauti yake na jina lake.
Sasa hiv Chadema ndio chama pekee kinaweza mkomboa mtanzania.
Forget about other parties!
 
Najua mtanishangaa lakini nimepata ufunuo kuwa mabadiliko ya haraka yatawezekana iwapo tu nguvu hiyo inatoka CCM(sijasema hayawezekani ila nimesema ya haraka). Kwa wanaofuatilia muelekeo wa siasa za nchi hii nguvu hii ya mabadiliko imekwisha anza kujidhihirisha, matukio ndani ya chama na kwenye serikali yanatoa taswira ya mafanikio muda si mrefu cha msingi ni kuongeza nguvu ndio maana nimekata shauri nachukua kadi. Siri za vyama vya upinzani zilizo mezani(za kufadhiriwa na CCM) na zilizo gizani ni dalili ya kuendelea kuchoshana tu huku watu wetu wanaendelea kuteseka kwa njaa,umasikini, kukosa elimu bora, huduma bora za afya na mateso yanayotokana na CCM hovyo, siwezi kusubiri vyama vya upinzani vibadilike huku nikishuhudia hayo nawafuata akina NAPE,JERRY na vijana wengine machachari tuinyoroshe CCM.
Nani yupo pamoja nami???????

Mabadiliko ya haraka CCM? labda kama neno haraka ni msamiati mpya! Hata hivyo nenda ukawaambie kuwa ndio ulikuwa unawasumbua hapa JF, watakuweka karibu ili kutwa ukae kupangua hoja zinazokwenda kinyume nao hapa!! Tuna tatizo kubwa kuliko tunavyodhani. The country has gone to the dogs!!
 
Wewe na yeyote aliye pamoja nawe ni watu wa kuogopwa kama ukoma. Kinachowavutia huko ndicho wengi tunachokipigia kelele - uozo ndani ya CCM.
Manyang'au hujikusanya kwenye mzoga, ole wao mzoga ukiisha.

Ahsante ndugu kwa yote uliyoyasema pamoja na jazba ila nimepata hapo mawili matatu ya kunipeleka huko niendako. Ushauri wangu unapochagua misemo uwe makini...kwani hujui ilhali viumbe vyenye roho vitaendelea kuwepo duniani mizoga ni guarantee itaendelea kuwepo?.
 
Back
Top Bottom