Natafuta video clip ya Tangazo la Chai Jaba niwape wanangu kama cartoon

me natafuta lile la Coca au pepsi kombe la dunia 2006 au 2010 lipo kikatuni flan hivi kuna manzi aliingiza mchepuko sasa mme wake akaja ikabidi demu amfiche mchepuko kwenye kabati wakat huo huo mechi inaendelea kweny screen sebuleni goal likafungwa wakawa wanashangilia hadi ule mchepuko ukashindwa kuvumilia ukatoka kabatini ukaungana kishangilia
 
Lile la mhaya aliyekwenda kwenye duka la mangi akaanza kuulizia bei ya bidhaa mojamoja mwisho wasiku akaona kama anajisumbua akauliza kwan duka lote shilingi ngapi?
 
me natafuta lile la Coca au pepsi kombe la dunia 2006 au 2010 lipo kikatuni flan hivi kuna manzi aliingiza mchepuko sasa mme wake akaja ikabidi demu amfiche mchepuko kwenye kabati wakat huo huo mechi inaendelea kweny screen sebuleni goal likafungwa wakawa wanashangilia hadi ule mchepuko ukashindwa kuvumilia ukatoka kabatini ukaungana kishangilia
Ilikuwa kombe la Dunia 2006
 
Mie natafuta lile la salama condoms kama unampenda utamlinda.

Mdada alikua ametoka kazini, mvua ilikua ikinyesha, alikua akiwaza ni jinsi gani atarudi home, akatokea jamaa yake gentleman hivii akamfunika na mwamvuli.
Kamziki kana play on the back ground, then inaskika sauti

"Kama unampenda utamlinda"
Hata mie nalitafuta hili tangazo, lilitoka miaka ya 2004-2005, mziki wa kweny background n mzuri kweli..kuna jingine la hivyo hivyo na wimbo huo huo kwny background, lkn linaonyesha mwanamke na mwanaume, mwanaume anapanda juu ya meza kufunua sehemu ya celling board anatoa kimkoba cha mkononi anakiweka mezani halaf ndani yake kuna salama condom, kimziki cha background kinapigwa na kumalizia maneno haya "kama unampenda utamlinda".. sio siri tangazo hili lilinivutia sana hasa mziki kwny background sijui uliimbwa na nani
 
Mimi natafuta lile tangazo la ombaomba kakalia kiti cha dhahabu mwenye ile video ya tangazo apost humu nilikuwa nalipenda sana
 
Hata mimi natafuta lile tangazo la mafuta ya jambo,lile walikua wanaimba "mimi naitwa jambo katikati,na wewe je?,mimi naitwa jambo ndogondogo,na wewe je?...." hahahaa nmelimiss mno
 
Mimi natafuta Tangazo la zamani la Vipi lambo ? .....Pancha bwana ......Pancha wakati kuna OKO . DAH lile Tangazo lilitisha miaka ya 90
Dah we jamaa umenikumbusha enzi hizo niko primary na baridi lile la Himaya ya Mkwavinyika hapo ni kipindi cha Majira RTD
 
Umenikumbusha mbali sana, siku moja shangazi yangu alikuwa amekuja toka kijijini akaliona hilo tangazo pamoja na lile la cowbell, kwakuwa lilikuwa linachekesha nasi tukacheka, lakini yeye alisikitika sana, akatuonya tuache kabisa tabia ya kucheka walemavu, akasema hao hawakujipendea kuwa hivyo, hiyo ni kazi ya Mungu haina makosa.
Mkuu aliamini lile domo la Chai jaba ni live?
 
Da kitambo sana likiisha tangazo hilo tayari kengere ya namba saa moja kamili asubuhi inagongwa Mimi mbio kwenda kuhesabu namba
 
Salama Condom mpya bora kwa bei nafuu... Salama Chaguo la kisasa...

Tuelezee siri ya mafanikio yako... Sio siri ni revola tu hulainisha ngozi yangu na huniacha safi na salama mchana kutwa.... binti mrembo kuliko wote tz wakati ule akiongea
 
Back
Top Bottom