Natafuta video clip ya Tangazo la Chai Jaba niwape wanangu kama cartoon

me natafuta lile la Coca au pepsi kombe la dunia 2006 au 2010 lipo kikatuni flan hivi kuna manzi aliingiza mchepuko sasa mme wake akaja ikabidi demu amfiche mchepuko kwenye kabati wakat huo huo mechi inaendelea kweny screen sebuleni goal likafungwa wakawa wanashangilia hadi ule mchepuko ukashindwa kuvumilia ukatoka kabatini ukaungana kishangilia
:D aisee
 
na lile la Sharo milionea na Mzee Majuto....
SHARO MILIONEA:Unatoa wapi Meen
Mzee Majuto:Airtel
SHARO MILIONEA:Umebugi meen
 
Dah, mwenye tangazo la shiva jerojero...shivaa..jerojero.. alitupie hapa, hata picha tu ya ile vocha
 
Mie natafuta la salama condom la je unaweza ku ila barabara ukiwa una cheza mziki? Badae wanasema tumia salama condom sasa tulikuwa tunaliita tangazo la uncle J
 
Kuna lile. La unajua kutumia Dawa ya penzi(Kondomu),Una tembo Master card ?
,Tukacheki sinema Bila fantaaa
 
Wapendwa mwenye hiyo video clip anisaidie kuitupia hapa JF kwenye huu uzi.
Natanguliza shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app


Umenikumbusha mbali sana, siku moja shangazi yangu alikuwa amekuja toka kijijini akaliona hilo tangazo pamoja na lile la cowbell, kwakuwa lilikuwa linachekesha nasi tukacheka, lakini yeye alisikitika sana, akatuonya tuache kabisa tabia ya kucheka walemavu, akasema hao hawakujipendea kuwa hivyo, hiyo ni kazi ya Mungu haina makosa.
 
Back
Top Bottom