Natafuta TV receiver

Natafuta TV receiver

WABALLA Inc

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2014
Posts
2,711
Reaction score
1,018
Habari ya weekend wakuu?
Yoyote anayejua sehemu zenye kuuza receiver ambazo zinazoonyesha station free bila malipo mfano kuna mtu kaniambia kuwa star life wanazo
 
Habari ya weekend wakuu?
Yoyote anayejua sehemu zenye kuuza receiver ambazo zinazoonyesha station free bila malipo mfano kuna mtu kaniambia kuwa star life wanazo

Inategemea unataka receiver gani.
Mie nauza aina mbali mbali za receivers za FTA (ambazo kwa maelezo yako ndizo unazohitaji). Zipo Strong 4930 (laki moja na kumi), Mediacom 940+ (laki moja), Ibox (laki moja na kumi). Hizo zote ni High Definition, zina blind Scan na zinaapokea BISS keys (kama wewe ni mtaalamu wa mambo hayo. Kama kuna swali niulize. Nipo Dar.
 
Hebu nieleze zaidi kuhusu hizo BISS keys sio mtaalam sana kwenye hii fani
 
Pia nitafurahi ukinipa Maelekezo ya ofisi yako
 
Hebu nieleze zaidi kuhusu hizo BISS keys sio mtaalam sana kwenye hii fani
Soory kwa ukimya. Kila kampuni ina utaratibu wake wa kufunga channels ili zionekana kwa wahusika tu (waliolipia tu). Mfano, DTSv wanafunga channels zao kwa kutumia mifumo ya Irdeto 2, Azam wanatumia Nagravision 3, Zuku wanatumia verimatrix na Startimes wanatumia Conax na videoguard. BISS keys ni aina ya encryption (mfumo wa kufunga channels ili zinekane kwa mhusika tu). Ila keys hizi aghalabu huwa ni bure na zinapatikana kirahisi mitandaoni.
Sasa basi, sio decoder zote zina uwezo wa kuweka hizo BISS keys. Ni somo refu kidogo, ila itoshe kusema kwamba decoder tajwa hapo juu zina uwezo wa kufungua channels zilizofungwa kwa mfumo huo wa BISS.
Pia nitafurahi ukinipa Maelekezo ya ofisi yako
Nina ofisi kadhaa. Moja iko mtaa wa Magila na Msimbazi kariakoo, inauza electronics mbalimbali. Nyingine iko Kitunda na yenyewe ina deal na masuala hayohayo. Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuni-PM namba yako.
Karibu sana mkuu
 
Back
Top Bottom