Natafuta tani 50 za Mianzi (Bamboo)

jajcom

Senior Member
Jan 4, 2013
125
250
Habari wadau,
Natafuta zaidi ya tani 50 za mianzi (Bamboo) kutoka sehemu yoyote Tanzania Bara. Kwa mwenye kujua mianzi inapatikana wapi kwa wingi niko tayari kuifata hasa kwa maeneo ya Dar es salaam, Pwani, Tanga, Morogoro na maeneo jirani.

Nahitaji kwa matumizi yangu binafsi na niko tayari kusafirisha mwenyewe na kuomba vibali kutoka maliasili.

IMG-20161223-WA0050.jpg

Mwenye kufahamu inapopatikana naomba anijuze.
 
bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,335
2,000
Hivyo vijiji vinapatikana wilaya gan?
Wilaya ya iringa vijijini, kuanzia Kitwiru, Tanangozi, Ihemi, ifunda hadi Mufindi pale. Tafuta contact za watu kule. Maana nahisi wenye mianzi huwa wanahangaika sana pa kupeleka, mara waichome moto. Ni vurugu tupu. Inatafuna sana rutuba ingawa kwao faida ni ile pombe.
 
jajcom

Senior Member
Jan 4, 2013
125
250
Wilaya ya iringa vijijini, kuanzia Kitwiru, Tanangozi, Ihemi, ifunda hadi Mufindi pale. Tafuta contact za watu kule. Maana nahisi wenye mianzi huwa wanahangaika sana pa kupeleka, mara waichome moto. Ni vurugu tupu. Inatafuna sana rutuba ingawa kwao faida ni ile pombe.
Mkuu nashukuru sana, Naweza kupata mawasiliano ya mkazi wa hayo maeneo?
 
Bashatu

JF-Expert Member
Nov 8, 2015
841
1,000
Mkuu tani unanuaje. Mi nipo iringa wilaya ya kilolo. Mianzi ipo mingi ila ni si ndefu kama kwenye picha. Nijuavyo mimi kuna aina zaidi ya 2000 za mianzi. Je mianzi ya iringa itakufaa?
 
jajcom

Senior Member
Jan 4, 2013
125
250
Mkuu tani unanuaje. Mi nipo iringa wilaya ya kilolo. Mianzi ipo mingi ila ni si ndefu kama kwenye picha. Nijuavyo mimi kuna aina zaidi ya 2000 za mianzi. Je mianzi ya iringa itakufaa?
Nahitaji mianzi kama inayoonekana hapo juu kwenye picha. Unaweza kuipiga picha unitumie niione.
Kuhusu gharama inategemea na eneo inapopatikana na urahisi wa usafiri
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom