Natafuta software ya kuratibu mahesabu ya dukani

Natafuta software ya kuratibu mahesabu ya dukani

Mimi ni professional software developer. Natengeneza specific solutions for business needs. Karibu tupige stori tuangalie ni namna gani utacontrol biashara yako ipasavyo mkuu.
mkuu, bei zako zipoje? Je software zako unatengeza ni Online au ni Offline pia?? Nahitaji dabase ya kutunzia hesabu zangu za biashara. Kwasasa natumia Excel lkn kutokana kuongezeka kwa data naona changamoto nyingi za kuendelea kutumia excel
 
mkuu, bei zako zipoje? Je software zako unatengeza ni Online au ni Offline pia??
Bei itategemea na requirements, muda nitakaotumia, uharaka wa mteja na thamani ya software husika kwa mteja.

Requirements/mazingira ndio zitadictate iwe online, offline au somewhere in between. I have done both.
 
Wadau mbona mnaweka namba zenu hazipatikan..?
 
Msaada wadau,

Nina depo ya bia na soda kubwa tu sasa kuna vijana nimewaajiri wa nne naona vitambi vinawatoka, mashavu dodo na mmoja kanunuaa gari aina ya crown week iliyopita mwingine alinunua gari aina ya volts december wao ni kula bata tu ni ndugu so nimewaweka shop tusaidiane maisha.

Wakati biashara napata loss karibia kila mwezi faida ikipatikana ni kidogo sana. So kama kuna mdau anajua software ya shop stock profit anisaidie maana nakaribia kufunga depo coz sioni faida wakati naona mzunguko upo.

Naamini humu kuna wataalamu watanisaidia.
Pole sana Mkuu , jaribu kuajiri mtu mwingine mwaminifu, coz hata hizo software wataweza kucheza nazo
 
Bro hupigi stock?Kama unapiga Ina balance au haibalance?unaweza ukawa unawalaumu vijana kumbe WW sio mfuatiliaji.kama unauza pombe Na duka kubwa ma Ni sehem yenye mzunguko Na vinywaji vya jumla uwezekano wa hao vijana kupiga cha huu Ni Mkubwa Sana.control stock yako mkuu
 
Chief mzunguko upo n mkubwa sana.. tatizo n faida mkuu sipati.... hilo ndo tatizo.
 
Mkuu, tatizo kama lako haliwezi kuwa solved kwa ku acquire tu software.

Kwanza, unatakiwa ukae na mtaalam umuelezee biashara yako, processes zote kuanzia mzigo kuingia, kuwa stored, kununuliwa, kutolewa na kulipiwa. Kila kitu kiwekwe wazi. Katika kila sub-process lazima muangalie taarifa (data) gani zinaingia, kuhifadhiwa, kubadilishwa na kutoka, mhusika ni nani na anafanya vitu gani katika hatua hiyo.

Kisha muangalie kwa makini sana faida yako inatakiwa itoke wapi na ni gharama zipi unazoingia ukiachana na za kununua mzigo. Tumia rekodi zako zilizopita katika hili.

Sasa muanze kukagua kila hatua, angalia ni vitu gani waajiriwa wako wanaweza kufanya vikaua faida yako. Angalia movement yote ya bidhaa pamoja na movement yote ya data na jinsi gani inaweza kuchezewa. Assume the worst katika kila hatua. Angalieni mianya yote.

Baada ya kuona nyufa zilizopo, mtadesign system mpya ya processes na control ambayo inaweka nia ya kuzuia mianya hiyo. Sio lazima iwe software per se - just an established system ambayo lazima ifuatwe katika kils hatua na isipofuatwa basi hatua husika haiwezi kufanyika.

Yani mfano kwa mfumo huo, kama nataka kuuza kreti lazima nifanye A,B,C kwa usahihi, na nisipofanya hivyo nishindwe kabisa kuuza kreti hilo, au nikilitoa kwenye stock lisiingie kwenye rekodi ya mauzo - liwe kama limeibiwa as far as data is concerned. Inaweza kuwa purely hardware based, inaweza kuwa combination ya software na hardware au ikawa purely software based, lakini principles za security, integrity and control ziwe enforced.

Kabla hujakimbilia kununua software, fanya analysis kwanza. Unaweza kujikuta kumbe vijana wanaagiza mzigo wao na wanauza huo badala ya stock yako na wanapata faida to the extent ya kutokukuogopa na kununua Crown wakijua fika huwezi kuwakamata kimahesabu kwasababu hawajakuibia fedha bali wamekuibia wateja, na market space.

Find the root of the problem, THEN sove it.
Umetoa ushauri wa msingi sana mkuu. Ulichoainisha ni baadhi tu ya madudu ambayo yanamaliza na kufilisi biashara nyingi sana hapa Bongo. Haswa Kama mmiliki anakuwa busy muda wote na shughuli tofauti tofauti bila kuwa na uangalizi wa karibu.

Kuna jamaa yangu alikuwa na Duka la Hardware. Yeye kutwa alikuwa analia hasara na kuishia kulipa gharama ya pango, umeme, ulinzi n.k.
Kumbe wale Vijana pale dukani walikuwa wanauza mzigo wao badala ya ule wa Boss uliokuwa dukani. Au kwa vitu kimoja kimoja wakiuza walikuwa wana replace. Maana Boss kwa mwezi anaonekana mara mbili au tatu dukani. Hao Vijana walipiga hela sana, mpaka Boss anakuja kushtuka tayari walikuwa mbali na miradi yao binafsi maeneo mengine. Na alikuja gundua sababu kuna jamaa yetu mmoja alienda kununua Tiles mzigo wa kutosha dukani kwake. Siku ya siku katika maongezi mshikaji ndio akamwambia "Chief Nilipita dukani kuchukua tiles na Gypsum boards" ...jamaa ndio akashtuka Eeeeeeeh! Wakati aliambiwa mwezi huo ulikuwa mgumu sanaaa, na vilivyouzwa vilikuwa havizidi laki 6 jumla ya mauzo ya mwezi. Wakati mshikaji pekee alichukua mzigo almost wa 4.2mil. Jamaa alitaka kuanguka na Duka aliliuza kwa hasira akaachana na hiyo makitu.
 
Du Sana Bro Proffessor, hizo ndizo changamoto za biashara ila cha msingi ningeweza kukushauri ufanye vitu viwili
1.Weka CCTV camera
2.Funga software
Changamoto nyingine kwenye software je itakidhi yale mahitaji ya biashara yako sababu software nyingi utazokumbana nazo ni za kudownload then mwisho wa siku inaexpire na kukosa support ya kutosha pindi utapokumbana na changamoto katika matumizi na isitoshe ukosefu wa elimu ya kutosha kwa watomiaji wa hizo software.

Nini cha kufanya ili upate software itakayokidhi mahitaji ya biashara yako na watumiaji kwa ujumla?

--Hakikisha software inakuwa user friend na iwe flexible yaan can be customized according to business requirements[Hapa ndipo kwenye shida kwa upande wa software za kudownload kwa sababu the source codes are protected na unapata uhakika wa support pindi unapopata matatizo.

NOTE:
Tafadhali hebu check hiyo ambayo ni best in Pharmacy(PeMS),shops and can be customized to meet your busines requirements.
1.Login
2.Login
Hi software nimefunga zaid ya pharmacy/shops 20 tanzania nzima

Kazi zangu zingine ni pmoja na

1.<img src="images/amis.png" width="100%" alt="AMIS PORTAL"><link rel="icon" type="image/gif/png" href="images/amis.png">
2.CCoHAS

Please text me on 0758 818117 to get username and passoword for test.
Mkuu, kwenye pharmacy moja ipo posta jengo la mkapa hio software ndo hii au unaweza kunitengenezea kama hio
 
Umetoa ushauri wa msingi sana mkuu. Ulichoainisha ni baadhi tu ya madudu ambayo yanamaliza na kufilisi biashara nyingi sana hapa Bongo. Haswa Kama mmiliki anakuwa busy muda wote na shughuli tofauti tofauti bila kuwa na uangalizi wa karibu.

Kuna jamaa yangu alikuwa na Duka la Hardware. Yeye kutwa alikuwa analia hasara na kuishia kulipa gharama ya pango, umeme, ulinzi n.k.
Kumbe wale Vijana pale dukani walikuwa wanauza mzigo wao badala ya ule wa Boss uliokuwa dukani. Au kwa vitu kimoja kimoja wakiuza walikuwa wana replace. Maana Boss kwa mwezi anaonekana mara mbili au tatu dukani. Hao Vijana walipiga hela sana, mpaka Boss anakuja kushtuka tayari walikuwa mbali na miradi yao binafsi maeneo mengine. Na alikuja gundua sababu kuna jamaa yetu mmoja alienda kununua Tiles mzigo wa kutosha dukani kwake. Siku ya siku katika maongezi mshikaji ndio akamwambia "Chief Nilipita dukani kuchukua tiles na Gypsum boards" ...jamaa ndio akashtuka Eeeeeeeh! Wakati aliambiwa mwezi huo ulikuwa mgumu sanaaa, na vilivyouzwa vilikuwa havizidi laki 6 jumla ya mauzo ya mwezi. Wakati mshikaji pekee alichukua mzigo almost wa 4.2mil. Jamaa alitaka kuanguka na Duka aliliuza kwa hasira akaachana na hiyo makitu.
Huyu mkurugenzi inabidi atulie afanye research atafute chimbuko la tatizo
 
Acha kbsaa mkuu vijana wanarudisha maendeleo nyuma sana... me naaamin software makin ndo suluhisho
 
Acha kbsaa mkuu vijana wanarudisha maendeleo nyuma sana... me naaamin software makin ndo suluhisho
Kabisa mkuu. Miaka ya nyuma wakati nilikuwa nasoma huko ughaibuni, nilikuwa nafanya kazi sehemu moja ambayo tulikuwa tunatumia SAP system. Hii ilikuwa intergrated na department zote mpaka kwa Managing Director. Kuanzia Receiving Dock (Mzigo unapoingia kiwandani) Mali inapoingia inaonekana kwenye system ni nani ameipokea, pieces ngapi, location ya mzigo ulipohifadhiwa kiwandani, utambulisho wa mtu anayechukua mzigo tayari kuupeleka Shipping Dept, Shipping Clerk anaingiza info kwenye system tayari kwa mzigo kuondoka kiwandani. Na hizo taarifa zote ulikuwa unaweza kuziona ukiwa na access kwenye SAP ya kampuni. Ni njia bora sana ya kudhibiti wizi na upotevu wa Mali kiholela. Pia barcodes system ilisaidia sana.

Nina hakika kwa sasa kutakuwa na softwares bora zaidi.
 
Karibu mkuu ipo systems nzuri ya kisasa unatumia mpaka kwenye simu yako. Ni check 0715812160
 
Pole sana ndugu, nathan kuna mahali una kosea hasa hasa kwenye internal control zako za biashara. Muhim ni kuangalia sehemu yenye risk kubwa na yenye ushawishi na kuithibiti vingine vitafuata mkondo.
Mfano. Wanapoweka oda na zinapolipwa je zinalandana? mzigo uliopo store na unaotoka na kinachopatikana kinaendana.
Jaribu kuweka watu wawili lakini independent na kila mtu umpe job description yake na ajue mipaka yake ya kazi.

Kuhusu software zipo nyingi sana zinazoweza tatua matatizo yako eg. QuickBooks au Tally ni nzuri na zinazotumika sana hapa kwetu kwenye SME & Individual.
QuickBooks.
Faida:

-Ni raisi sana kutumia hata kwa mtu asiye mwasibu
-Ina report nzuri sana, kwa maana unachokiitaji cha aina yeyote waweza kipata kwa muda wowote.
-Management ya Store na Accounts zipo well arranged naweza kusema,kiasi kwamba mpaka mtu aje kukuibia inaitaji utaalum wa ziada.
-Waweza kuweka credentials(mipaka) kulingana na watumiaji ulio nao na wakazifuata bila wao kujua.

Hasara
-
Ni garama kidogo kama unaitaji orginal version na hii pia utaweza pata access ya mobile phone access kwamba mtu akiuza au mzigo ukitoka store utajua na utaweza jua store kimebaki kiasi gani.

Tally ERP
-
Sio rahisi kutumia, inaitaji muda kuizoea na kuweza kufanya posting na uyamkini wa kukosea post ni mkubwa usipo kuwa makini au kutojua nn unafanya.
-Uzuri ina both Accounts & Payroll kwa wakati mmoja.

Excel
Hii ni nyepesi kwa kutunzia data zako na kupata taarifa kila unapo ziitaji. Ina changamoto lkn nayo inatumika sana.

Note: Hivi vyote ni vizuri na vinasaidia kulinda na kugundua uhai wa biashara yako. Lakini vinaitaji uwekezaji na utayari wa wahusika. Kwa maana, lazima watu wako hao uwapeleke training wajue kutumia, wanaweza wasiwe wote lkn wale kwenye sehemu nyeti ni lazima.

Tunauza na kutrain izi software, tucheki tushauriane na tuone ni kwa jinsi gani unaweza okoa biashara yako.
Tupigie: 0717 71 85 19 | 022 270 1320
Tuandikie: training@comskills.co.tz
Karibu sana
 
Watu wanaleta habari za quickbook na madude magumu magumu? Hatuhitaji hizo. Hata hizi kompyuta tunazotumia kuna watu waliumiza vichwa kubadili Command usser interface ambayo iliwashinda watu wengi hadi kwenye Graphical user interface ambayo kila mtu anaitumia. Sasa mtu anaomba msaada wa haraka mtu anamjibu akasome ama accounting package? Hakuna watu humu waliosoma kutengeneza software rahisi ambao inaweza kukidhi matakwa ya muuliza swali akaweza kuitumia kama tunavyotumia simu ngumu bila kuisomea? Nadhani wapo, tena waweke wazi na sii kuweka namba ya simu ili umpigie ama kwa nyia ya PM. Huu ndio muda wa wanafunzi na maprofesa wa IT kukunyua makucha yao.
Ni hivi ndugu, hiyo ni biashara na biashara ina mengi ikiwemo utunzaji wa taarifa muhimu za miamala, mali, madeni, hapo hakuna suala la njia ya mkato, accounting packages ndio suluhisho la uhakika vinginevyo atakwenda akwame hukombele ya safari, na asitishike na hizo program kwani akipata mtaalam mzuri atamtengenezea mfumo atamuelekeza kiasi cha wiki 2 mpk 3 baada hayo kazi zinaenda, zingatia ni account package ndizo zinazoweza kuandaa taarifa zilizokamilika ktk masuala ya ukaguzi wa mahesabu na pia zinaendana na kila aina ya biashara, kinyume na hapo mnampotosha
 
Back
Top Bottom