Natafuta shule | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta shule

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Tiger, Jan 24, 2010.

 1. T

  Tiger JF-Expert Member

  #1
  Jan 24, 2010
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,750
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Ndugu wana jf nina ndugu yangu(msichana (21)) aliyehitimu kidato cha nne upande wa arts .
  Kwenye mtihani wake alipata D 3 na F 4.
  Ninachoonba toka kwenu ni ushuri wa kwamba je?

  1) anaweza kufanya nini ili aendelee na masomo hasa kwa mtoto wa kikekama yeye?
  2) anaweza kusoma kozi gani ambayo akimaliza anaweza kujiajiri/kuajairiwa au kijaendeleza zaidi?
  3) kunachuo gani anachoweza kusoma kulingana na sifa zake hasa katika mikoa ya Dar, Arusha au Tanga?

  Nina uhakika sana kwamba nitapata ushauri mzuri toka kwenu maana hii ni ndiyo jamii forum.
  Natanguliza sukruni zangu kwenu.
   
 2. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  kama nafasi ya malipo ipo kaka mpeleke akasomee kozi za nursing
   
 3. T

  Tiger JF-Expert Member

  #3
  Jan 24, 2010
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,750
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Nashukuru mkuu najua hii ndiyo jf.
  Pamoja sana mkuu.
   
 4. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2010
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Todays nursing is not our grandparents nursing. It has evolved and very scientific, you need a strong background in biology,microbiology, math, chemistry and some sociology and psychology. not to forget maths and pharmacology. What makes you think a form four failure can do that?

  On the constructive side, find the young woman's interests and cultivate them. We tend to forget vocational training, one of my regrets in life is that I did not learn any trade. Jifunze kuchonga mtumbwi, kutengeneza matofari, kutengeneza furniture, kusuka ukili, virago etc. people always buy matofali , mikeka na maandazi.
   
 5. b

  bnhai JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Huyo ndugu yako anaamini kuwa bado anamuda wa kusoma? Maana kuna watu wengine wanaamini wamechelewa. Km anajiona anamuda na anaweza formal training areseat masomo yake ambayo itamchukua mwaka mmoja, then aendelee na kidato cha tano au cha sita (2 years), then University of which atakuwa bado mdogo. Ila tu km uwezo wake wa kipesa, utayari na akili yake inamuwezesha kufanya hivyo.
  Option ya 2 ni kufanya vocational training. Kuna ufundi km cherehani ambao mtu akiufanya kisasa utamlipa. Hii ni pamoja kuwa na ofisi ya kueleweka na appointment nk.
  Km hayo ni marefu kwake ajifunze hata ualimu wa chekechea. Akiu-modenise utamlipa na maisha yatakwenda.
   
 6. T

  Tiger JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,750
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Nimependa sana mawazo yako,
  mi mwenyewe baba yangu ni Doc. na mama ni nurse lakini sijapata hamasa ya kushuri aende huko.
  To be honesty she is not that much confident to face such subject as advance maths, i know her.
  Niliwahi kumwambia akajifunze kutengeneza mikate(bakery) ambayo ukiwanayo makini unauwezo wakuajiri na watu wengine.
  Shida ya watu wengi ni kwamba bado tunapenda sana kuajiriwa hata kama hatuoni manufaa.
  Hata hivyo bado naomba msaada wenu kwakuwa naamini kuna wazo au chuo ambacho mkinishauri nimwambie ili afanye apendacho.
   
 7. T

  Tiger JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,750
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Nashukuru ndugu kwa mawazo yako tafadhari ukipata wazo jingine usisite kunishauri.
  Asante sana. Nawapenda sana jamani.
   
 8. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  1) anaweza kufanya nini ili aendelee na masomo hasa kwa mtoto wa kikekama yeye?

  *** Hapo ndipo watu wengi huwa wanakosea sana! Nini chakufanya hupaswi kumchaguliwa kwani ni ngumu sana kujua uwezo wake na interest yake! Kaa naye uongee naye na akwambie nini anaweza kufanya/kusoma! Epuka lawama kama: 'wewe ndiyo ulinishawishi kusoma Biology'

  2) anaweza kusoma kozi gani ambayo akimaliza anaweza kujiajiri/kuajairiwa au kijaendeleza zaidi?

  *** kwa maisha ya sasa kidato cha 4 bado ni elimu ndogo sana. Mshauri arudie mtihani wa kidato cha nne kwanza ili apate credit walau CCC kisha ajikongoje na kidato cha 5/6. Baada ya hapo yeye ndiyo achague nini cha kufanya na sio wewe au sisi kumchagulia!

  3) kunachuo gani anachoweza kusoma kulingana na sifa zake hasa katika mikoa ya Dar, Arusha au Tanga?

  *** Vyuo vipo vingi ni pesa yako tu lakini simshauri aendelee na vyuo kwani katika elimu kadri unavyosonga mbele ndivyo mamabo yanapanuka. kumbuka tunaishi katika dunia ya utandawazi ambayo ili uwe ngangari kitaaluma basi walau unatakiwa usome hii kitu wanayoita 'formal education'. Ni vyema binti yako ajenge msingi imara kwanza! Ninauhakika miaka ya baadae itakuwa ni ngumu sana kupata kazi kwa cheti cha kidato cha 4.
   
 9. T

  Tiger JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 30, 2007
  Messages: 1,750
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Asante kwa ushauri ila usisahau kuna GENERAL na SPECIALIZED KNOWLEDGE. Tuko pamoja sana.
   
 10. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  haya nimekusoma! mimi mwenyewe shule imenipiga kushoto, karibu kijiweni ni kelele na draft kucha kutwa....
   
 11. TingTing

  TingTing Member

  #11
  Jan 25, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  ni vyema akaangaliwa ni nini anataka kuja kuwa ama "interests" zake ziko wapi. Mimi siamini kuwa bila kidato cha nne bado hujakomaa kiakili. Kuna watu wengi sana wanaoishia hapo na kwenda chuo na kufanya vyema. Kinachotakiwa ni mhusika kujua anapendelea nini haswa na kisha kuingia shule iwapo hela inaruhusu. Shule si lazima iwe "university" kuna njia mbadala za kufika huko hata kama mtu hujafanya vyema O' au A level kama vocational training center, polytechnic colleges na community colleges mbali na hapo pia kuna vyuo binfasi vyenye hadhi zao pia. Muhimu ni kujua chuo gani, gharama zake na ubora wa elimu yake ikiwa ni pamoja na "pass rate yake". Watu wengi udharau kusomea professional qualifications kama ABE, CIM, City & Guilds, CIM, CAM n.k zinazotolewa na vyuo kadha wa kadha ambavyo vimesajiliwa na vinatoa huduma hii kwa niaba ya Center husika. Hizi zinajulikana na kutambulika popote pale nchini na nje ya nchi. Kama mhusika yuko tayari kujitoa muanga kwa kujitudnika katika mojawapo ya hizi kozi basi afanye utafiti wa vyuo/colleges na kisha ajiunge.
   
 12. mabuba

  mabuba Senior Member

  #12
  Jan 25, 2010
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 133
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Habari mwanajf.

  Nakushauri huyo kijana wako upeleke chuo cha Kumbukumbu ya mwalimu Nyerere. Akasome programme inaitwa kazi za vijana (Youth Work). Hii ni programme ambayo imesaidia vijana wengi amabo hawakufanya vizuri kidato cha nne. Mara amalizapo kozi hiyo, kama amefanya vizuri ataendelea na stashahada miaka miwili na baadae shahada. J
   
Loading...