Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,578
- 28,699
Wakuu natafuta shamba la kununua lenye ukubwa usiopungua hekari 30, kwa ajili ya project yangu ya kilimo mwaka ujao ninayotegemea kuifanya nje kidogo ya jiji la Dar es Salam, shamba hilo naomba liwe na sifa zifuataazo:
Kwa mwenye kuwa nalo au yeyote mwenye kuuza naomba tuwasiliane hapa au kwa PM hususani kwa mambo kama bei, vibali na location.
Natanguliza shukrani
- Liwe na ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo hususani mahindi
- Liwe eneo lenye water-table iliyo karibu, eneo ambalo nikichimmba kisima cha ku-drill nitapata uhakika wa maji kuanzia lita 5,000 kwa siku, na iwe ni kwa mwaka mzima.
- Liwe pembezoni mwa mji lakini umbali usizidi km 50 kutoka Dar es Salaam.
- Liwe linafikika kwa urahisi kwa gari kwa ajili ya kusafirisha mazao yangu kutoka shambani
- Uwepo wa umeme japo si muhimu sana
Kwa mwenye kuwa nalo au yeyote mwenye kuuza naomba tuwasiliane hapa au kwa PM hususani kwa mambo kama bei, vibali na location.
Natanguliza shukrani