Natafuta picha za mzee Jongo

sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
7,566
11,484
Alikuwa akiitwa Ibrahim Raha maarufu kama mzee Jongo, alikuwa mzee wa makamo na msanii wa viwango vikubwa katika upande wa ucheshi. Kwa wanaokumbuka alianzia redio Tanzania na badae akahamia kwenye runinga ya ITV.

Usingeweza kuchoka kumtazama kwa vituko na maigizo ambayo yangeweza kukutoa kwenye kuigiza na kudhania ukweli.

Nimekuwa nikitafuta picha za huyu mzee ambaye kwa sasa ni marehemu bila mafanikio. Kwa mwenye picha au video clip za huyu mzee naomba tafadhali.

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
 
Picha sina....ila umenikumbusha mbali sana miaka ya 90 mwanzoni kulikuwa na igizo lake RTD kama sijakaosea likuwa linaanza saa tatu..siku sikumbuki..hapo familia nzima haiendi kulala inasubiri kipindi...kikianza ole wako upige kelele.,..
 
1697224758962.png

1697224786746.png

Nami naomba za juma na uledi mchezo maarufu niliusikiliza kupitia kanda za kaseti?
 
View attachment 2781265
View attachment 2781267

Nami naomba za juma na uledi mchezo maarufu niliusikiliza kupitia kanda za kaseti?
Marehemu mzee Said Fundi al'maarufu mzee Kipara,alianza uigizaji mwaka wa 64.

Nakumbuka siku za mwisho za uhai wake alikuwa akilalamika sanaa yake kutomsaidia chochote kiasi cha kukosa makazi hadi wasanii wenzake wa Kaole kujichanga na kumpangishia nyumba maeneo ya Kigogo Mburahati.
 
Asee Kuna kazi ni hazina faida zaidi kukupa umaarufu , kupanga ni kuchagua sometimes haina namna lazima usifanye kwasababu hakuna plan B lakini ishi nayo kwa mpango.
 
Alikuwa akiitwa Ibrahim Raha maarufu kama mzee Jongo, alikuwa mzee wa makamo na msanii wa viwango vikubwa katika upande wa ucheshi. Kwa wanaokumbuka alianzia redio Tanzania na badae akahamia kwenye runinga ya ITV.

Usingeweza kuchoka kumtazama kwa vituko na maigizo ambayo yangeweza kukutoa kwenye kuigiza na kudhania ukweli.

Nimekuwa nikitafuta picha za huyu mzee ambaye kwa sasa ni marehemu bila mafanikio. Kwa mwenye picha au video clip za huyu mzee naomba tafadhali.

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
Muulize Jiwe akutupie kutoka kuzimu huko.
 
Back
Top Bottom