Natafuta paka Dar kukamata panya

Natafuta paka Dar kukamata panya

CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2010
Posts
571
Reaction score
157
Habari zenu wadau?
Naomba msaada.
Natafuta paka (domestic cats) wawili - dume na jike.
Wasio na mabaka kama ya chui.
Wenye mabaka kama ya chui wana asili ya kuwa deviant (paka mwitu)- huwa na tabia ya kukamata vifaranga na hata kuku.
Nawahitaji sana, panya wananisumbua.
Sipendi kutumia sumu au mitego - ni kinyume na taratibu za mazingira, pia hazimalizi tatizo - hupunguza tatizo tu.
Njia sahihi ni kufanya mazingira yasiwe rafiki kwa panya (i.e kutoacha mabaki ya vyakula hovyo au kutohifadhi vibaya vyakula) na biological control (kwa kutumia paka).

Natanguliza shukrani.
 
nyau wangu ana vitoto tele njoo uvichukue maana nawaza pa kuvipeleka aiseeh
 
Huyu atazaa siku si nyingi nitakupatia wote kama utakua bado hujapata.
 
mkuu upo wapi kama upo dar mm nikuletee free kabisa. garama mpaka za kufika kwako juu yangu mkuu.
 
Haaa jamani mpaka namuonea huruma maana inapoelekea ataanzisha NYAU DAY CARW CENTRE
 
Kuna nyau anasumbua sana hapa sijui nikukamatie!
 
Hapa naona utani/ mzaha mwingi.
Waliosema wana paka/ nyau nawaomba contacts hawatoi.
Kama mko serious nitawachukuaje sasa wakati contacts hamtaki kutoa?
 
kuna chama cha wanyama wa home tanzania sjui knaitwaje.. wacheki hao jamaa utajipatia nyau.
 
Habari zenu wadau?
Naomba msaada.
Natafuta paka (domestic cats) wawili - dume na jike.
Wasio na mabaka kama ya chui.
Wenye mabaka kama ya chui wana asili ya kuwa deviant (paka mwitu)- huwa na tabia ya kukamata vifaranga na hata kuku.
Nawahitaji sana, panya wananisumbua.
Sipendi kutumia sumu au mitego - ni kinyume na taratibu za mazingira, pia hazimalizi tatizo - hupunguza tatizo tu.
Njia sahihi ni kufanya mazingira yasiwe rafiki kwa panya (i.e kutoacha mabaki ya vyakula hovyo au kutohifadhi vibaya vyakula) na biological control (kwa kutumia paka).

Natanguliza shukrani.

Mara unafuta PAKA,
Mara unatoa mongozo wa njia sahihi za kudhibiti PANYA,
Muda sio mrefu utaanza kutafuta MBWA na baadaye utatafuta PANYA.

Mimi nikushauri: Paka sio mnyama wa kufuga ikiwa huna hela kama wengi wetu tunavyodhani. Leo hii wewe unatafuta JIKE na DUME, style anayokujanayo mtu anayetaka kufuga ng'ombe au mbuzi akiwa na lengo wazaliane na kuongzeka. Je, hiyo ndio nia yako?

Ikiwa huna hela za kuwafunga kizazi hao PAKA wako, basi naomba uwe na huruma kwa jirani zako. Nyau anazaa mara 2 kwa mwaka na huzaa watoto kadhaa, cha kuzingtia ni kwamba, hutakuwa na wa kumuuzia.Jirani yangu alipoanza na nyau mmoja JIKE, hakuyazingatia haya. Tena yeye hakuwa na super strategy kama wewe uliyeamua kutafuta DUME na JIKE sasa hajuti peke yake, bali mtaa mzima tunajuta.

Sumu ya PANYA ipo hadi ya 500.
 
  • Thanks
Reactions: amu

"Do not argue with a fool because people may not recognise the difference"
Unajuaje kama jike hatifungwa kizazi lkn jike na dume waendelee kufurahia nature?

Si kila mada lazima udandie, waliokaa kimya wao wajinga lkn wewe mwerevu?

"The more the person speaks, the more (s)he exposes his/her ignorance"
 
Nenda pale open university of Tz kinondoni biafra, kuna nyau wengi sana. Yaani wametapakaa kila kona. Idadi ya pusi pale inalingana ya wanafunzi.
 
Back
Top Bottom