Natafuta Nyimbo za zamani za Taarab

Natafuta Nyimbo za zamani za Taarab

Umenikumbusha mbali sana. Nikiwa na umri was miaka 11 nliwahi msindikiza mama sehemu inaitwa Mtupie, Chumbageni basi wee huo wimbo ulikua ukiimba redioni na msusi anaimba kwa hisia nikajikuta naupenda.
Mkuu nilikua nausikiliza zamani RTD kipindi cha mziki wa mwambao, nilishawai kuwa na tape yake ilinipotea hata hivyo bado nautafuta.!
 
Ahsante sana mkuu.
ila kila nikijaribu kui download inafeli na sijajua kwanini.
Labda kama unaweza kunisaidia kwa watsaap nikupm mkuu.

Mkuu sio hii taarab hile ni ya mid2000
 
Kuna wimbo wa zamani ulikuwa unaitwa zumbukuku mambo ipo huku,usinishike bega mke wangu yupo hapa hapa,panda juu nenda ukazibe.
 
Umenikumbusha mbali sana. Nikiwa na umri was miaka 11 nliwahi msindikiza mama sehemu inaitwa Mtupie, Chumbageni basi wee huo wimbo ulikua ukiimba redioni na msusi anaimba kwa hisia nikajikuta naupenda.

Mwenye hii atuwekee pia nakumbuka walikuwa na igizo la huu wimbo
 
Jamani mie atafuta ule wimbo wa
TX mpezi doctor wangu zamaniii,
anayo degree kapasi Ujerumaniii,
ananipasua tezi siku nyingi tumboni,
TX nipasue, Taja vyote sikunyimiiiii. Na kuendelea.

Kiitikio: Nipasue Tx nipasue mie ninapenda operation we nipasueeeeeee
 
Mpende bado yupo hai pendo alipokee

Ukimpenda yupo kaburini utalitupa pendo lako hewani.

Nilivipanda viazi, matuta yakajazana
Viazi vya kinyamwezi chakula cha kiungwana.
Vikaingiliwa na wezi hata sina la kunena mie, naapa silimi tena nawachia walimao.

Mambo ya zuhra wa mombasa
 
Dah,sijaona mtu akitaja "mlango wa mungu u-wazi" au walau japo "fimbo ya mungu" ujue nn kinamshikisha mtu adabu....hizi zinanipeleka mbaliiiii kilwa kisiwani kwenye majahazi haswaa na sio lile la mzee yusuph...
 
Wakuu kuna ile moja ya moyo......moyo eeeh ondoa machungu,hayo yalokuufika mwachie Mungu.
nakuasa moyo wangu,tafadhali nisikize........huu ulipigwa sana ile cku ya uchaguzi wa kwanza vyama vingi wakichuana chenkapa,cheyo mapesa na lyatonga.Halafu ile ya manahodha wa ngalawa
Nahodha akae mbele,abiria tuwe nyuma
tuvikwepe vipengele,tupate fika salama salama
manahodha wa ngalawa,kwa nini wakae nyuma
 
Dah! Mmang'ati na taarab!

JF is never boring - The Boss
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom