Hongera Mkuu!
Hapo umepata mradi wa kukutoa. Lakini uwe "serious" siyo utupiga ma-green tu humu JF! Ila mbona itakuwa kazi sana kuwaweka ng'ombe 120 kwenye zero grazing? Labda ungeniambia unataka kuanzisha small scale ranch hapo ningekuelewa. Hao Ankole mkuu ukiwachanganya na Boran wanatoka bomba sana maana utapata ng'ombe wazuri sana wa nyama.
Wazo lako na mimi ninalo Mkuu, napingana sana na ufugaji wa kuweka mamia ya ng'ombe wenye tija hafifu. Kwetu Wasukuma hiyo ndo fahari yetu, ng'ombe 1,000 lakini maisha magumu kichizi!! Watoto hata hawaendi shule. Nakutakia mafanikio mkuu tutakuwa tunajuliana hali mara tukianza hii kitu. Mimi nataka kufugia Kigoma.
Nataka niwe nawachezea:
Niwe nachanganya mbegu bora ya Boran 9pure breed) na mbegu bora ya Ankole (pure breed)
Mbegu bora ya Freishian (puer breed) na mbegu bora ya Ankole (pure breed).
Halafu hizo products niwe nauza kwa ajili ya nyama, zingine natenga kwa ajili ya maziwa.
Maziwa YOTE yatakayokuwa yanatokana na hawa Ankole (ambayo huwa ni kiasi kidogo sana 1- 2 litre per cow in 24 hours) itakuwa inatumika kwa kulipa wafanyakazi, chakula cha wafanyakazi na matunzo ya ng'ombe hao. Mimi faida yangu itakuwa ni kuwavuna tu kila mwaka mara moja. Nikiuza 50 cows kila mwaka sikosi 15,000,000 - 20,000,000 ambayo naweza kusomesha watoto wangu watatu na kuwawekea miradi endelevu kama mashamba yenye ukubwa wa ekari kadhaa za maembe ya kisasa kwa ajili ya kumuuzia Bakhresa (AZAM) ili na wao kutokana na exposure (through formal and informal education) yao waweze kuweka vitu vingine kama hotels, hospitals au viwanda kama watahitaji! Au wakuu haiwezekani? Japo si rahisi kiasi hicho lkn IT IS POSSIBLE!
Kuna mzee mmoja ana ekari 300 za maembe (aliniambia ekari 1 ina uwezo wa kumpatia mkulima 15,000,000 kwa mwaka).
Ikiwa ni 10,000,000 kila ekari na na ekari 300 (tufanye 200 out of 300 nd'o ziwe productive).
Ina maanisha anaweza kutengeneza AT LEAST 10,000,000 x 200 = 2,000,000,000 Tshs per year!
Everything is possible if one is patient (not a patient) and determined!
Japo mimi labda naweza nisifanikishe hivyo kwa kipindi nilichopanga, mkiona mawazo yanalipa YOU BUY THE IDEAS
"People can help a man think, but they can't think for him/ her!"