Natafuta mwanamke wa kuzaa naye. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta mwanamke wa kuzaa naye.

Discussion in 'Love Connect' started by RUBERTS, May 18, 2012.

 1. RUBERTS

  RUBERTS Senior Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 41. Ninaye mtoto mmoja wa kike ana umri wa miaka 10. Tatizo ni kwamba mke wangu hashiki mimba nyingine. Tumeishaangaika vya kutosha kwa madaktari wa kawaida na waataalamu wa masuala ya wanawake (Gynoclogists) lakini naona hakuna uwezekano tena. Nimevumilia sana sasa naona nakata tamaa. Mimi nahitaji mtoto mwingine japo mmoja, lakini mke wangu hataki nizae nje ya ndoa. Sifa za mwanamke ninayemtaka ni hizi: Awe na kazi na elimu anglau form six, anaweza akawa na mtoto lakini si zaidi ya mmoja, awe mzuri na mweupe, dini siyo muhimu sana ila mimi ni mkristo, awe na uelewa wa kutosha wa maisha, asiwe na ugonjwa wa aina yoyote, awe mchangamfu, asiwe after money. Mtoto akizaliwa awe tayari kupima DNA ili kujihakikishia kuwa mtoto ni wangu. Maana matapeli wako wengi.
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280
  hayo mambo ya kuwa na watoto kisiri siri mabaya ukifa ghafla itakuwaje? Si mwanzo wa watoto kuoana huu?

  Ila nakutakia mafanikio mema........
   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Acha tamaa, acha uzinzi. Ulisema utakuwa mwaminifu kwa shida na raha mpaka kifo kiwatenganishe!! Una watoto wawili (mmoja ni wa mkeo, sawa) umesema unawapenda sana, sasa unatafuta mtoto mwingine wa nini. Acha uzinzi, tamaa za ngono. I dont buy your idea at all. Tena unasema unataka uzae kwa siri, hopeless!!!
   
 4. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  hyo e-mail yako badilisha huendani nayo wewe sio Mr trusted.
   
 5. uttoh2002

  uttoh2002 JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,680
  Likes Received: 2,738
  Trophy Points: 280
  Hopeless and stupidy Man, what a shame? Watoto wanaliwa mpaka Uharibu Amani ya Ndoa yako? Mkeo Naye akitafuta mwingine? Uzinzi huo hauna maana wala sababu.
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,246
  Trophy Points: 280
  Unatafuta ngono za bure tu wewe! Mie najitolea kuzaa na wewe ila kwa ivf.
  Unatafuta wa kuzaa nae, elimu yake na uzuri wake unahusikaje hapo? Asiwe na mtoto zaidi ya mmoja ili iweje? Una mpango wa kuhudumia familia yake yote?
   
 7. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Chukuwa na watoto wa dada yako uishi nao na kuwasomesha hao nao ni watoto. Mbona Clinto ana mtoto mmoja tuu kama wewe na bado ni mtu wa furaha tuu?
   
 8. Maty

  Maty JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 2,170
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Yaani ni kama umeiba mawazo yangu, we unatafuta mtoto halafu unaanza kuweka mavigezo kibaaaaaaaaaaaao mara form six mara awe mweupe na mzuri oh asiwe after money we vipi wewe bana? Sema unatafuta mwanamke mrembo mweupe na ili uwe unazini nae kirahisi ndio utaka kumbebesha hilo limimba pambafu kabisa wewe mkeo ana hasara.
   
 9. LD

  LD JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Akili ya mwanaume inawaza hivi? Mwanaume aliyeumbwa kwanza kabla ya mwanamke? Haya labda utampata.
   
 10. y

  yaliyomo yamo Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duuh! Yaleo kali kweli akili ni nywele
   
 11. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,019
  Likes Received: 8,498
  Trophy Points: 280
  Phew....!!
   
 12. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Asante Uttoh 2002, Eti jianaume jizima linafikiria mavi (samahani kwa neno kali) kichwani!! Shame up on him. Watoto ni malori kuwa sasa naanza kuzalisha mali utajiri unanukia, linafikiria kuvunja ndoa eti watoto!! Watoto unajua watakuwa wa aina gani kama si vibaka wa kuchoma na moto mitaani mpaka wavunje ndoa. Jitu halina huruma na mama liliyemtoa kwa wazazi wake, je mwenzio akifanya hivyo utafurahi, shenzi.
   
 13. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  HIVI UKIWA NA MIKA SABA BILA HATA MTOTO. NA UKAGUNDUA SHIDA IPO KWA MWANAMKE. WEWE KAMA GREAT THINKER UTASHAURI MWANAUME ACHUKUE HATUA GANI???. tUSIONGEE TU KUFURAHISHA JAMIII. JE MUME AKUBALI KUISHI MAISHA YAKE YOTE BILA MTOTO???
   
 14. CUTE

  CUTE JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 1,237
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  alafu mke wake wa ndoa hataki asa kwanini umkaidi mkeo jamani..............wanaume nyie na sio kwamba mke hazai ashakuzali mmoja na bado angekuzalia sema mipango ya mungu ndio ivo tena sasa ww badala ya kukituliza ndani unataaka ukagawe mbegu nje lol!
   
 15. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  jaribu kutafuta anayejitosheleza kwa kipato, ukichukua hawa wanawake wachumia tumbo ndoa yako itakuwa mashakani sana maana atakufuata kila siku nyumbani kwa kisingizio cha mtoto.
   
 16. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yeye anatafuta mtoto, atulize ndani atampata?
   
 17. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kama uwezo unao kama unavyo sema siongeza mke.
   
 18. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  Yes, ishi bila mtoto, mtoto ni oxygen? Uliahidi nini kanisani? Ahadi ni nini? Usichopenda kufanyiwa usimfanyie mwenzio.
   
 19. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tusikurupuke. Madumuni mojawapo ya ndoa ni watoto, Kama hawapo amani hiyo unayozungumzia haipo kabisa. Ila kuna watu wanavumilia tu na maumivu moyoni. Wanawake wengi wanauchezea ujana wao na kusababisha tatizo la kutopata mimba.
   
 20. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Please take my advice - Kama mmeishi muda mrefu na mkeo tunaamini mlifunga ndoa takatifu, hii ina maana ni vizuri mkaishi kwa misingi ya dini yenu. Kama mkeo alishakukataza kuzaa nje ya ndoa yuko sahihi kabisa, ukikiuka hilo na mkeo akagundua hakika ndoa yenu itakuwa hatarini lakini utakuwa umemkosea mungu sana.

  Lakini pia, wako watoto wengi sana hawana wazazi (yatima), kuna wengine ambao walitupwa wazazi wao hawafahamiki - kwahiyo ningekushauri kushauriana na mkeo suala la ku-adopt mtoto. Lakini la muhimu zaidi mkeo aridhike, akisharidhika mnaweza kufanya hivyo. Mtapata thawabu kwa mungu wengu, lakini pia ndoa yenu itakuwa na amani zaidi kwani huyo atakuwa mtoto wa kwenu. Ingawa itakuwa muhimu kufuata taratibu zote za ku-adopt huyo mtoto.

  Mwisho, hiyo email address yako imekuwa ya kihuni pia.
   
Loading...