Natafuta mtu wa kunishika mkono

imekaa kimkakati sana kwakua ni ke bas Kuna msaada utaupata ila ungekua Me bado ngoma ingekua ngum sana
 
Kwa vile ni demu watu watakusaidia ,ila ungekuwa dume wangekuambia urudi Kijijin ukalime [emoji848]
 
Kuna watu wanaenda kujikaanga apo [emoji115][emoji115][emoji115]
 
Struggle is real utapata wa kukushika mkono
 
Kwanin moderator wamefunga pm zako
 
Nimekumbuka Uzi wako ulioomba ushauri kuwa uwaambie rafiki zako kuwa umepoteza kazi.

Na ukawe ushuhuda mahali hapa kwa kuwa unalopita nalo wewe tayari ni mshindi.
 
Habari chukua hii business idea kupitia hiyo 200k uliyonayo

Kanunue ulezi 5kg = 10000

Mchele 2kg = 6000

Karanga 1.5 = 8000

Mahindi 2.5 kg = 5000

Mbegu za maboga 1kg = 4000

Ukishavipa vyote vitayalishe kwa kuviosha vizuri na uvianike, karanga na mbegu za maboga zikaange vikishakauka vizuri kavisage.

Kusaga = 2000

Jiko la mkaa =10000

Mkaa = 5000

Sukari 2kg = 4000

Blueband = 8000 ile kubwa

Chupa za chai zile kubwa 3 karikoo= 60000

Vikombe vya robo lita 20 = 10000

Sufuria kubwa 1= 25000 kariakoo

Pilipili manga = 5000

Total 157500

Pika uji kwakuwa unapatikana kinondoni uza kinondoni studio mpaka mkwajuni kila siku jioni

Kikombe kimoja uza 500

Kwa siku ukitengeneza vikombe 60 vya uji utakuwa unapata 30000

Ni biashara ambayo inafaida sana uji wako ukizoeleka unaajiri ata na wadada wenzio

Ukiifanya hii biashara na mtaji wako ukakatika nitakurudishia pesa yako 200k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…