Natafuta mtu wa kunifadhili masomo yangu

Natafuta mtu wa kunifadhili masomo yangu

kalachai

Member
Joined
Jul 4, 2021
Posts
76
Reaction score
110
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 23.

Shikamooni wa kubwa rikaa yangu habari zenu natumain wote ni wazima na mnaendelea vyema na jukumu la kulijenga taifa letu lenye kubarikiwa na Mungu TANZANIA

Kama nilivyoeleza hapo juu ndugu zangu nimeona nililete hili kwenu kwa yeyote ataeguswa naomba anisaidie nimekwama kuendelea na masomo kwasabu ya kiuchumi mimi nilikuwa nasoma fani ya Clinical Medicine nimemaliza mwaka wa kwanza lakini niliacha kuendelea na masomo kwa sababu ya pesa.

Pia chuo nilichosoma ni cha private aliyekuwa anajichanga changa ili nisome kwa sasa hana pesa ni kwamba ameporomoka kiuchumi na nina mpango wa kutafuta chuo cha Government mwaka wa kwanza pamoja na kusoma kwa shida sana nilijitahidi nisipate sup, repeat module wala disco ili niendelee kumconvice mfadhili wangu aendelee kunilipia. Mungu alinisaidia nikapata GPA ya 3.0

Asanteni na Mungu awabariki
 
Niongee kitu hapa ,hii familia im3shakua kua kubwa ni suala la wewe kujulikana uko wapi aidha kupitia Mods au jf member mwenzako ambaye yuko karibu nawe.

Baaada ya kuwabaini hapo ,hebu tulione hili wazazi wenzangu kwa kuangalia kila mmoja kwenye muamala wake wa siku moja ile mia mbili hamsini iliobaki 250Tsh tujitolee kuichanga tukiwa watu laki moja humu100000 mdogo wetu atasoma kwa faraja kabisa
 
Pole sana.

Msomi wa Clinical Medicine.. (Japo sioni mahali uliyosema ni level ipi.. Certificate, diploma, advanced diploma au degree)..

Naomba nikushauri uandike vizuri aya zako ili tuzielewe.. Ainisha hitaji lako vizuri kwa mchanganuo.

Nakuombea mema hitaji lako na litimie.
 
Kama ni mkristo nakushauri kaongee na mchungaji wako akupe nafasi waumini wakuchangie..kama ni mwislamu nenda msikitini..

Humu wengi tuna comment tu ila swala la kumchangia mtu ni ngumu. Maana hatuna uhakika kama kweli ana shida ama ni msanii
 
Kama ni mkristo nakushauri kaongee na mchungaji wako akupe nafasi waumini wakuchangie..kama ni mwislamu nenda msikitini..

Humu wengi tuna comment tu ila swala la kumchangia mtu ni ngumu. Maana hatuna uhakika kama kweli ana shida ama ni msanii
Sawa mkuu asante kwa ushauri wako
 
Kama vipi waweza tafuta kazi ukapiga ukitunza hela ya kujisomesha.watu Kama wanakusaidia kumbuka watalipa hela chuoni na wewe lazima uwe umesajiliwa.inatakiwa Ada ijulikane ni Bei na mahitaji mengine pia ni kiasi gani
 
Back
Top Bottom