Natafuta mtu wa kufanyanae biashara

Natafuta mtu wa kufanyanae biashara

muksinihamisi

Member
Joined
May 1, 2020
Posts
14
Reaction score
6
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 22 nimemaliza elimu ya secondary mwaka 2017 nashukuru nilipata ufaulu mzuri ila sikuweza kuchaguliwa hvyo kutokana na uchumi sikuweza kuendelea na masomo bali nikajiingiza kwenye ujasiliamali na kuweza kupata ujuzi wa kutengeneza bidhaa mbalimbali za viwandani kma vile sabuni za miche aina zote ikiwemo medicated soap aina tofauti tofaut,sabuni za maji aina zote, kama vile za kudekia (tiles cleaner) handwash,jik,shampoo nk.

Pia,utengenezaji wa mafuta ya mgando,lotion nk.Nimeshindwa kukuza hii idea kutokana na capital.Hvyo ninaomba mtu ambaye tutaweza kushare idea na kuikuza wenda tukafanys kitu kikubwa zaidi.
 
Umefanya uchambuzi wowote upande wa soko?

Nimeuliza swali hili sababu kila mwenye pesa za kuwekeza sehemu atakuuliza.

Wote tunajua kuna biashara kibao zinafilisika huku wakiwa wanazalisha bidhaa nzuri tu ila unakuta hawakupika uwepo wa soko la kutosha na kutumia nguvu kidogo sokoni.

Kumbuka kuzalisha inapaswa kuwa hatua ya pili baada ya kuona soko lipo vizuri. Ndio maana unakuta mtu kafanya biashara ya bidhaa flani miaka kadhaa akaona inalipa na soko lipo akapiga tathmini akizaliaha mwenyewe inalipa zaidi basi akaanza kuzalisha.

Courtesy of miamiatz
 
Back
Top Bottom