Natafuta mtaalam wa Gia box

Natafuta mtaalam wa Gia box

george tiru

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2018
Posts
200
Reaction score
147
Naombwa kujua tatizo ni nini hasa, nina gari gari chaser hasa asubuhi ukitaka toka ukiweka D au R
inachukua kama dk 5 ndio inaanza kuondoka, nimebadilisha ATF lakini bdo tatizo linaendellea, mwenye experience nazo anipe angalau cha kufanya.
 
Naombwa kujua tatizo ni nini hasa , nina gari gari chaser hasa asubuhi ukitaka toka ukiweka D au R

Nilikuwa na tatizo kama lako, kinachotokea ni kwamba zile oil seal ndani ya gearbox zinakuwa zimekauka kutokana na uchakavu, hivyo unapoweka gear oil pressure inapotea kwenye zile loose seals na inachukua muda mafuata ku-accumulate kwenye njia zake na kutengeneza pressure ya kutosha ili kuondoa gari.

Kutengeneza ni ghali na inaweza isipone maana ni a very intricate system, simple solution ni kanunue used gear box toka japan / dubai pale lindi na shaurimoyo, ni very cheap, kwa gari yako hilo litoyota hata laki 2 unusu hadi tatu utapata. Mi nilihangaika sana na kutumia gharama kubwa, in the end solution ikwa ni kubadilisha gear box.
 
aisee nshukuru kwa ushauri wako, kumbe gear box yake si ghali sana, maana kuna fundi kaniambia kushusha na kufunga laki 3, kumbe naeza nunua ingine tuna kufunga, ahsante.
 
Kushusha, kusuka na kufunga inaweza fika hata laki 5, sasa angalia unafuu
 
Naombwa kujua tatizo ni nini hasa , nina gari gari chaser hasa asubuhi ukitaka toka ukiweka D au R
inachukua kama dk 5 ndio inaanza kuondoka, nimebadilisha ATF lakini bdo tatizo linaendellea, mwenye experience nazo anipe angalau cha kufanya.

Gearbox automatically ni kununua mpya tu kama Fundi ata rule out shida Siyo wiring!! Asikudanganye mtu anatengeneza gearbox AT itakufa next week!
 
Naombwa kujua tatizo ni nini hasa , nina gari gari chaser hasa asubuhi ukitaka toka ukiweka D au R
inachukua kama dk 5 ndio inaanza kuondoka, nimebadilisha ATF lakini bdo tatizo linaendellea, mwenye experience nazo anipe angalau cha kufanya.
kanunue lingine Milion 3 chaser,crester
 
Naombwa kujua tatizo ni nini hasa , nina gari gari chaser hasa asubuhi ukitaka toka ukiweka D au R
inachukua kama dk 5 ndio inaanza kuondoka, nimebadilisha ATF lakini bdo tatizo linaendellea, mwenye experience nazo anipe angalau cha kufanya.
Badili gearbox kama alivyoshauri FRANCIS DA DON ,kwa uzoefu wangu gearbox ikishaanza kusumbua kupona ni nadra sana...
 
Kama upo dar nenda pale toyota duka lao lipo karibia na kituo cha mwendo kasi karia koo msimbazi A kanunue hydraulic ya gear box namba 4 usinunue gearbox mpya kwanza baada ya hapo uje kwenye uzi huu kunishukuru 100% tatizo sio gearbox ni hydraulic unayotumia ndo tatizo

(Hydraulic ipo kwenye mkebe ujazo wake ni lita 4 bei ni 94600+ itapendeza kama ukichukua na oilfilter yao inauzwa 15000 engine oil tumia ya castol 65000 lita 5 w40)

Baada ya hapo chombo yako ni mpya kabisa trust me gearbox yako n nzima kabisa iyo hyraulic ya toyota namba 4 ndo special inatembea kilomita 20000
 
mfobi,
You have a point.

Kuna watu wanaweka hadi za kupima.

Unazungumzia duka lipi? Kisangani Autospares.
 
mfobi,
Sasa kama seal zimekauka, nini mantiki ya kubadili hydraulic oil? Na hata kama hiyo oil ni nzito kiasi hicho, ikishatumika na ikawa nyepesi tatizo litarudi tena, hivyo temporary solution tu
 
Duka la toyota wenyewe ukipita njia ya mwendo kasi baada ya kupiga kona kutoka kituo cha fire uwelekeeo wa kwenda kariaoo utakapozikuta taa za mwanzo upande wa kushoto utaona duka kubwa limeandikwa toyota na nembo yao ndo hapohapo
 
Mzigo huo hapo maduka mengine kwa kariakoo wanauza 90000-120000 ila uhakika zaidi ni kwa toyota wenyewe oil kwa saizi ni tatizo makanjanja wanekua wengi
Screenshot_20190820-213035.jpeg
 
Duka la toyota wenyewe ukipita njia ya mwendo kasi baada ya kupiga kona kutoka kituo cha fire uwelekeeo wa kwenda kariaoo utakapozikuta taa za mwanzo upande wa kushoto utaona duka kubwa limeandikwa toyota na nembo yao ndo hapohapo
Ndiyo hilo. Linaitwa Kisangani Auto spares. Kuna spare halisi sio fake.
 
Hio gari itakua na shida kwenye solenoid za kwenye gia box maana hapo ndo kunapofanya either gia ziwahi au zichelewe ku engage..kabla ya yote hakikisha unatumia ATF recommended i.e dexron ii/iii au iv
 
Ofcourse kabla ya kubadilisha inabidi a rule out matatizo kama hayo kwanza, lakini kwa jinsi alivyoelezea haiwezi ikawa solenoid, maana solenoid ikifa imekufa, na sio ichelewe kuengage gear
 
Mkuu mimi kuna gari ina shida ya design hio hio hata ukisema u google delaying shift husababishwa na shift solenoid ingawa mleta mada hajasema utakuta hio gari ukikanyaga mafuta sana inaanza kusogea taratibu taratibu
 
Back
Top Bottom