Je, unaweza tumia oil ya gear box kwa ajili ya power sterling (mfumo wa usukani)?

geranteeh

JF-Expert Member
May 21, 2015
266
618
Watu wengi huwa tunatumia magari bila ya elimu hasa kwenye kuyahudumia na kwa bahati mbaya kwa Tanzania ni wachache sana hujitolea kuandika elimu mbalimbali kuhusu magari kwani wengi hutegemea elimu hiyo tuipate kwa mafundi na mafundi wamekuwa labda ni wachoyo kwa kuhofia watapoteza wateja kwani watanzania wengi ni wajuaji ama labda hawana elimu ya uandishi au hawana muda huo. Kupitia channel yangu ya telegram ntakupatia elimu hiyo bure lakini pia Jamii forum na sehemu nyingine ambazo watu watakua wame share.

Leo naomba kukupa jibu ambalo watu wengi hutamani kufanya ila tu hawana elimu nalo au pengine wanatishwa na mafundi na wataalamu wengine wa magari. Huwa tunazingatia kubadilisha oil ya gearbox (Transmission fluid) na oil ya engine lakin hatizingatii sana hii ya power sterling. Leo utapata madarasa matatu kwa wakati mmoja na kama ulijua nimemaliza basi Karibu.

Je Kuna ulazima wa kumwaga kimiminika cha power Steering?

Hapa kumbuka tunazungumzia gari zenye Hydraulic power steering system ambazo ni lazima ziwe na power steering pump ambapo mfumo mzima huuatokeo yake hutupa ulaini wa usukani wako pindi unapoendesha gari yako.

Kazi kubwa ya hivi vimiminika ni kuzoa chembe chembe mbali mbali ziwe zenye asili ya chuma mbao ama vumbi ambavyo pia hadi viingie kwenye mfumo ni ngumu na inachukua muda sana na ndo maana unakuta kuna muda maalumu wa kubadili oil ya gari au kimiminika cha gear box lakini si kwa kimiminika hiki cha usukani lakini wataalamu wanashauri ubadilishe baada ya mwendo mrefu japo haijawekwa kitaalam ni km ngapi au miaka mingapi.

Sasa hapa kwenye kubadilisha ndo linapokuja swali la je ninaweza tumia oil ya gearbox (Transmission fluid) kama mbadala?

NI NINI TOFAUTI YA OIL YA GEARBOX NA KIMIMINIKA CHA USUKANI?

Hapa naongelea ATF au AF ambazo tunatumia kwenye magari yetu na sana hapa naongelea hizi automatic cars.

Kwanza kwa rangi ni nyekundu ambapo inapotumika huwa inatoa harufu fulani nzuri sana wakati kimiminika cha usukani inakua nyeupe au inakuja na rangi kama ya pink lakin pia kikitumika inakua na harufu fulani ya kama kitu kimeungua.

Achana na rangi na harufu kwenye matumizi kama nilivoongelea kazi ya oil ya engine basi na kwenye oil ya gearbox yako (ATF) kuna material ambayo yamewekwa ili kupunguza msuguano pindi inapokua inafanya kazi ndani ya gearbox na pia kwenye Fluid ya Power steering kuna viambata ambavyo vina kazi hiyo hiyo lakin kwa upande wa power steering sasa hivi viambata vilivyopo kwenye ATF endapo vitakwenda kutumika kwenye Power sterling basi ni swala la muda utaweza kuharibu pump ya power steering pamoja na valve za kwenye power steering. Kiufupi kinachoweza kukuharibia power steering system si kile kimiminika bali ni vile viambata ambavyo vimewekwa kwenye Oil ya gearbox na ndo maana pindi utakapoweka ATF kwenye Power steering vitafanya kazi ila ni swala la muda kuharibu system yako nzima ya Power steering nadhani kidogo hapo utakuwa umeelewa. So kwa magari ya Kisasa unatakiwa utumia PS fluid husika kwa gari yako. Kiufupi si kwamba napambana na maendeleo ya ulimwengu lakini nachukia sana gari za kisasa tunatumia sababu hatuna namna ila ni muumini mkubwa sana wa Old Model hapa naongelea 80's na 90's cars unajua kwanini?

Gari za miaka ya kuanzia miaka ya mwanzoni na 90s kurudi nyuma ni tofauti katika utengenezaji na gari za miaka ya katikati kuja juu. Naomba nikupe mfano ambao nimeushuhudia na ninaendelea kushuhudia.
Nina rafiki yangu ana toyota Limited ambayo ilipasuka kidogo kwenye system ya power steering mwaka 2016 fundi wake akamshauri akati anajipanga basi atumie Oil ya gearbox au oil ya kupima kwenye power steering mpaka atakapokua vema atabadilisha then ataendelea kutumia PS fluid unajua ni nn kimetokea????

Mpaka leo hii mwaka 2023 anatumia oil ya gearbox au oil za kupima kwenye steering power kila inapopungua anaongezea tu kidogo every week.

Mfano wangu unamaanisha kwamba kwa gari za zamani yani miaka ya kati mwa tisini kushuka chini haichagui chakuweka kati ya PS fluid au ATF kwenye power steering system kwasababu hazina complicated system ambayo ina vitu vinavoweza kuharibika kwenye mfumo wa Power steering endapo utaweka ATF kiufupi zimeundwa na material ghafi ambayo yanaweza kuzoea ATF kwenye system yake na ndo maana rafiki yangu kaitumia zaid ya miaka nane na mwenye kuhitaji ushahidi anaweza nitafuta am here to prove it.

Kwa gari za kisasa yani gari za miaka ya katikati ya tisini kuja juu sikushauri ufanye hiki kitu kwani matokeo yake nimeshayaeleza hapo juu kwasababu kuna components zimeongezwa kwenye system ya power steering zinazoikataa ATF yani ukiweka tu utaharibu ndgu yangu.

Thats why napenda sana old cars haziko complicated na vifaa vinaingiliana kwa mfano Limited, Corola 110, Corola 111 na corona kuna vifaa vingi vinaingiliana tofauti na gari za kisasa mfano mazda demio Generation ya kwanza ya pili na ya tatu haziingiliani vifaa hata kama ile ya pili na ya tatu kimwonekano kama zinafanana lakin imagine hata bearing haziingiliani.

Gari za kisasa zimetengenezwa kibiashara zaidi kuwapa guarantee watengenezaji ya kuingiza pesa katika uuzaji wa spea kwa wingi.

Kwa kumaliza ningependa kusisitiza tu jitahidi kuisoma instruction menu ya gari yako kwamba ni nini inataka kutumika na ni nini haihitaji kumbuka kila gari inayo na kama hamna basi tumia muda wako wa ziada kuangalia youtube videos na articles mbalimbali kuhusu gari yako na hakika utapata taarifa husika kwani dunia imekua kijiji. Usikubali kudanganywa au kuambiwa hiki na kile na hata hiki ninachokuandikia hapa kila siku unaweza kukihakikisha kwenye official websites za wataalamu wa magari. Mpaka wakati mwingine ni mimi katika ujenzi wa taifa.

Makala hii imeandikwa na Hamis Mgaya

IMG-20230607-WA0004.jpg
 
Asante kwa elimu,endelea kutupa madini mkuu

But You can make it summarized next time
Asante mkuu tatizo niki summarize ntatumia sana lugha ya ki professional na watu wengi hawataelewa ila nkitumia lugha hii ya maelezo wengi wataelewa si unajua kiswahili kilivo kinazunguka
 
Additives zilizomo ndani ya transmission fluid ni tofauti na additives zilizomo ndani ya power steering fluid...hivo sasa kutokana na utofauti wa additives hizi, seals/ valves za steering pump hazipo designed kutumia additives zilizomo ndani ya transmission fluid, na kama ukiweka transmission fluid ndani ya steering system kama alternative ya steering power fluid, basi utaua seals na valves za steering fluid pump prematurely..

Ni kama matumizi ya msfuta ya drake kwenye system ya dot 3 ukaweka dot 4 au system ya dot 4 ukaweka dot 3. Utaona matokeo yake baada ya muda..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Additives zilizomo ndani ya transmission fluid ni tofauti na additives zilizomo ndani ya power steering fluid...hivo sasa kutokana na utofauti wa additives hizi, seals/ valves za steering pump hazipo designed kutumia additives zilizomo ndani ya transmission fluid, na kama ukiweka transmission fluid ndani ya steering system kama alternative ya steering power fluid, basi utaua seals na valves za steering fluid pump prematurely..

Ni kama matumizi ya msfuta ya drake kwenye system ya dot 3 ukaweka dot 4 au system ya dot 4 ukaweka dot 3. Utaona matokeo yake baada ya muda..

Sent using Jamii Forums mobile app
Sure ila kuipata dot 3 kipengele kweli kaka
 
Back
Top Bottom