Natafuta MKOPO

Mgombezi

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
610
178
Wana JF

Ninaamini wote tutakubaliana ya kwamba moja kati ya changamoto inayomkabili mjasiriamali ni chanzo cha fedha katika kuanzisha au kuendeleza biashara yake.

Kuna malengo nimeweka kwa mwaka huu katika kuendelezaji mradi wangu, sasa ili niweze kufikia hilo lengo nahitaji kuangalia vyanzo vingine vya fedha.

Hivyo basi natafutufa mkopo wa masharti nafuu wa Tsh. 5,000,000/= kwa kuanzia, kama kuna mwanaJF ambae anaweza kunisaidia katika hili tunaweza kuwasiliana.

Naomba kuwasilisha!
 
njooo huku kwenye vyombo vya fedha upatiwe mkopo fasta...............kama una biashara nenda ACCESSBANK wanatoa mkopo haraka na kwa masharti nafuu kabisa
 
njooo huku kwenye vyombo vya fedha upatiwe mkopo fasta...............kama una biashara nenda ACCESSBANK wanatoa mkopo haraka na kwa masharti nafuu kabisa
Kweli hiyo bank wanatoa mikopo fasta, kuna riba pale hadi basi.
 
njooo huku kwenye vyombo vya fedha upatiwe mkopo fasta...............kama una biashara nenda ACCESSBANK wanatoa mkopo haraka na kwa masharti nafuu kabisa

accesbank iko dar tu,mbona mikoani amna na kwa watumishi vipi,pia stambincbank nayo ni nzuri,
 
Mgombezi,
unayo Account NMB?if yes nenda NMB wanatoa mikopo kwa wajasiriamali na huwa na intrest nzuri.ila hawatoi mikopo kwa ajili ya vyombo vya usafiri e.g dala dala,boda boda etc.
kuna mtu wangu wa karibu anawatumia and they are helpful to wajasiliamali.
Kama umeajiriwa nenda CRDB peleka payslip wao watakupa mkopo fasta tu
 
njooo huku kwenye vyombo vya fedha upatiwe mkopo fasta...............kama una biashara nenda ACCESSBANK wanatoa mkopo haraka na kwa masharti nafuu kabisa

Asante Jile79, bali huko ni wapi?
 
kwenye msafara wa mamaba na kenge tumo... nasikizia sana hivyo vyanzo vya mikopo...!!:evil::evil:
 
Ni kweli CRDB wanatoa mikopo kwa wafanyakazi ila si rahisi kama ilivyoandikwa hapa. Inampasa mwajiri wako kusaini mkataba au MOU na CRDB ili uweze kuanza kukopeshwa kama mfanyakazi. Mie mwenyewe nishawahi jaribu kuomba mkopo kama huo mwaka huu (2011) hata hivyo sikufanikiwa kwakua mwajiri alikataa kusaini MOU.

Tuhabarishe kama taratibu zimebadilika
 
Mie natafuta mkopo kwa wafanyakazi .... net ni kama 3.5M kwa mwezi ila mwajiri hasaidii wafanyakazi kuomba mikopo bank (kusaini MOU)... Nitashukuru kama kuna mtu atatoa taarifa ni wapi wanatoa mikopo kama hyo...
 
Back
Top Bottom