Natafuta mkopo nimalizie ada ya chuo, nimekwama

tzhumoally

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
412
156
Wakuu mimi ni mwanafunzi nasoma chuo cha ardhi morogoro katika fani ya geomatics(land surveying),

Najisomesha mwenyewe kutokana na mitihani ya maisha niliopata hapo nyuma, tunaanza mitihani tarehe 20 mwezi huu,hapa tumepewa mpaka tarehe 17 mwezi huu tuwe tumemaliza ada, otherwise hatutoruhusiwa kufanya mitihani.

Naomba kama kuna msamaria mwema naomba anisaidie mkopo kwa masharti ya kuwacha vyeti vyangu kama dhamana kwa muda wa miezi minne mpaka mwezi wa 10 nitakua nimeshahangaika kuzipata, cheti changu cha form four nina div 111 ya points 14 nilipata penalt ya civics, na form6 pcm nina div111 ya points 12 nilipata penalt ya GS. nadaiwa 637,500 ila nahitaji laki 7 ili niweze kumalizia hii semister.namba yangu ya simu ni 0673500181
 
Attachments

  • IMG-20160614-WA0020.jpg
    IMG-20160614-WA0020.jpg
    56.2 KB · Views: 81
  • IMG-20160614-WA0027.jpg
    IMG-20160614-WA0027.jpg
    44 KB · Views: 104
  • IMG-20160614-WA0028.jpg
    IMG-20160614-WA0028.jpg
    43.3 KB · Views: 97
  • IMG-20160614-WA0018.jpg
    IMG-20160614-WA0018.jpg
    33.4 KB · Views: 76
Nenda sijui Bank gani wale wanaweza kukusaidia, tatizo ni kwamba huo muda ni mfupi sana. Mpwa hebu sema kabis ani bei gani unatakiwa??
 
mimi niliwahi kuacha vyeti vyangu kwa MENEJA WA CRDB miaka hiyooooooooooo alinielewa sana , tafuta taasisi za kifedha kaziache huko .ila angalizo wakati huu wa magufuli fedha ni ngumu ,wasije kuchania vyeti vyako.
 
Mkuu hii thread yako ungehamishia kule kwenye jukwaa la habari na hoja mchanganyiko au jukwaa la elimu. Utapata wasamaria wema watakaokusaidia japo kejeli na matusi hayatakosekana
 
tzhumoally hebu waone FINCA Microfinance Bank wa office maeneo ya Mwmbechai Magomeni huwa wanatoa mikopo ya ada ya wanafunzi kuanzia Primary hadi Chuo kikuu. Watajua wanakusaidiaje.

Pole bhana
 
Mkuu hukuandika unahitaji sh ngapi,japo mi sina uwezo wakukusaidia lakini hata kwa wenye uwezo na nia hawaelewi unahitaji pesa ngapi.Ni vema ungesema
 
mimi niliwahi kuacha vyeti vyangu kwa MENEJA WA CRDB miaka hiyooooooooooo alinielewa sana , tafuta taasisi za kifedha kaziache huko .ila angalizo wakati huu wa magufuli fedha ni ngumu ,wasije kuchania vyeti vyako.
sawa mkuu nitajaribu njia hio nione itakua vipi na mungu akipenda ilifika mwezi wa kumi nitakua nimeshapata kuzilipa
 
tzhumoally hebu waone FINCA Microfinance Bank wa office maeneo ya Mwmbechai Magomeni huwa wanatoa mikopo ya ada ya wanafunzi kuanzia Primary hadi Chuo kikuu. Watajua wanakusaidiaje.

Pole bhana
nitajaribu kufika hapo mwembechai nifatilie japokua nipo ardhi institute ya morogoro ila nitajaribu kwenda dar hio jumatatu mungu akipenda
 
nitajaribu kufika hapo mwembechai nifatilie japokua nipo ardhi institute ya morogoro ila nitajaribu kwenda dar hio jumatatu mungu akipenda

Mkuu hauhitaji kusafiri hadi Dar, FINCA Bank wapo pia Morogoro Boma Road wamepakana na Hospital ya Agha Khan. Kwenye lile gorofa refu la Omary Awadh.

Wewe nenda hapo ili ujue mapema kama unapata ama la. Mimi ninachojua wanatoa Mikopo kwa wanafunzi na wamiliki wa shule na vyuo.
 
kama ni hivyo itanirahisishia,agakhan naijua kwahio nitapajua tu mungu akipenda,nitakupa mrejesho mkuu
 
Back
Top Bottom