Natafuta Mke

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,458
29,151
Jamani eee!!,
Nimefikiria sana kwa undani nimeona nije humu jamvini kutangaza kwamba sasa natafuta Mchumba ili aje awe mke wangu mungu akipenda, maana maisha ya ukapera na ubachela yamenichosha sasa.

Vigezo;
Awe mrembo,
Mchapa kazi,
Asiwe mnywaji wa pombe,
Asiwe mpenda kujirusha,
Asiwe muongeaji sana,
Kabila lolote kasoro Mzaramo, Mkinga, ****** na Mmachame,
Sio mnene sana but angalau uwani kajazia,
Elimu kuanzia Form6, na awe tayari kujiendeleza zaidi,
Asiwe mkorofi wala mgomvi,
Dini yoyote, ila tu aamini Mungu ni mmoja Muhammad ni moja ya mitume wake,
Kazi sio lazima sana, ila kama anayo iwe ya halali,
Umri usizidi miaka 27,
Awe hajawahi kuolewa akaachika,
Msafi wa nje na ndani,
Mpenda na mheshimu ndugu zake na zangu,
Mwenye upendo wa kweli sio wa 'kifedha' zaidi,
Awe tayari kupima hospitali.


Wasifu wangu,
Elimu Degree moja,
Muislam,
Mwajiriwa sekta binafsi,
Mpole,
Mrefu kias (1.8m),


Kwa alie tayari tujuane zaidi kwenye ''Private Message''
 
Umekosea njia,hapa sio mahala pake,peleka Love Conect!
 
Ebo, Mod vipi?
mbona mnachakachua msg yangu? si nitapata mtu ambae sie sasa? watu tuko sirias bwana.
Mi sikuweka nyota nyota, nimesema katika makabila ambayo nisingegenda kuo ni m-kwere, kwani ni tusi?
 
Hilo kabila lililowekewa nyota lime2mika sana kumdhihaki mkuu wa nchi ndio maana mitambo imedetect hapo.
 
Umekosea njia,hapa sio mahala pake,peleka Love Conect!
Sawa,lakini hao wanaopitaga huko Love Conect si na hapa pia wanapitaga?Wacha nsikilizie kwanza hapa, nkiona sio naweza kuhamishia huko unakosema
 
Kabila la mtu halinyimi sifa ya kuwa mke bora!
Ni vile tu natumia simu ambayo haina uwezo wa kuweka link,but ningekuwekea uone majibu aliyopata yule jamaa ambae alitaka kuoa mmachame!!,Haya makabila mengine nina sababu zangu nyingine tofauti
 
Ni vile tu natumia simu ambayo haina uwezo wa kuweka link,but ningekuwekea uone majibu aliyopata yule jamaa ambae alitaka kuoa mmachame!!,Haya makabila mengine nina sababu zangu nyingine tofauti
Nimeifuatilia ile link, but still si 7bu ya kugeneralize. Otherwize All The Best
 
Loh! kwa vigezo hivyo bora ukamchukue Muhimbili ulee mwenyewe. mitaani hapatikani.
Dunia kubwa lakini,pia si lazima sana awe mwanajamii wa hapa,hata kama kuna anaemjua mtu/ndugu/rafiki/jirani/ n.k. mwenye sifa hizi anaweza tu kuniunganisha nae.
 
Jamani eee!!,Nimefikiria sana kwa undani nimeona nije humu jamvini kutangaza kwamba sasa natafuta Mchumba ili aje awe mke wangu mungu akipenda, maana maisha ya ukapera na ubachela yamenichosha sasa.Vigezo;Awe mrembo,Mchapa kazi,Asiwe mnywaji wa pombe,Asiwe mpenda kujirusha,Asiwe muongeaji sana,Kabila lolote kasoro Mzaramo, Mkinga, ****** na Mmachame,Sio mnene sana but angalau uwani kajazia,Elimu kuanzia Form6, na awe tayari kujiendeleza zaidi,Asiwe mkorofi wala mgomvi,Dini yoyote, ila tu aamini Mungu ni mmoja Muhammad ni moja ya mitume wake,Kazi sio lazima sana, ila kama anayo iwe ya halali,Umri usizidi miaka 27,Awe hajawahi kuolewa akaachika,Msafi wa nje na ndani,Mpenda na mheshimu ndugu zake na zangu,Mwenye upendo wa kweli sio wa 'kifedha' zaidi,Awe tayari kupima hospitali.Wasifu wangu,Elimu Degree moja,Muislam,Mwajiriwa sekta binafsi,Mpole,Mrefu kias (1.8m),Kwa alie tayari tujuane zaidi kwenye ''Private Message''
wish u the best inshaallah!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom