Nimefurahishwa na mwenendo wa michango ya wadau katik hii thread wameonekana kukerwa na PERRY aliyetoa jibu la dhihaka katik ishu sensitive kama ya mtoa mada.
Kimsingi katika jamii hii hakuna ambaye hajaguswa na athari za HIV/AIDS, anaweza kuwa ama mwenza, mtoto, mzazi,ndugu, jirani au jamaa umempoteza au ana maambukizi au anaugua.
Na si kila anayepata eti ni mzinzi SI kWELI na saiv thanks to ARVs watu wanaathirika bt wanatumia dawa na kuishi miaka mingi had wanalea na kusomesha watoto had wanajitegemea.
Mama wa rafiki yangu mume wake alifariki miaka 13 iliyopota lakini mama aliendelea kutumia dawa na sasa watoto waliokuwa wadogo sasa hiv wako vyuo vikuu na bado yuko kazini akiendelea kuwahudumia. So plz huna sababu ya kumnyanyapa muathirika eti kw sababu tu ni muathirika.