Natafuta miti ya matunda yafuatayo:

CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
571
156
Ndugu wana JF, natumai hamjambo!
Naomba mnisaidie wapi naweza kupata miti ya matunda yafuatayo? Nahitaji angalau miti miwili katika kila aina.
Nahitaji mnisaidie kunielekeza nitakapozipata, contacts na if possible na bei zake:

(1)Zabibu (nyeusi na za kijani) - jumla miti minne
(2)Strawberry - miti miwili
(3)Zeituni - miti miwili
(4)Dates (tende) - miti miwili
(5)Apples (tufaa) - miti miwili
(6)Pears - miti miwili
(7)Pomegranate (komamanga) - miti miwili
(8)Mulberry (forosadi) - miti miwili
(9)Tangarine (chenza) - miti miwili
(10)Na miti ya matunda mengine mengi kadiri mtakavyoona yatanifaa, sana sana mimea inayostawi sehemu ya joto - nataka niipande Mtwara.

Nitashukuru.
 
Ungekuwa Morogoro ningekuambia nenda TTSA - Tanzania Tree Seed Agency. Wanaotesha miti na kuuza kwa bei ndogo - miti ina-range kuanzia 1000 na kuendelea depending on the nature of trees. Mingine ni special order - ukiwaambia wanakuoteshea. Wako Kihonda (Dar - Moro - Dodoma Highway). Ofisi zao zinafunguliwa Jumatatu hadi Ijumaa (8:00am - 15:30hrs). It's five to seven minutes driving distance from Msamvu - the main bus stand.
 
Asante kwa msaada wako.
Tatizo la hizi agencies/ taasisi za serikali au wafanyakazi wa serikalini kwa ujumla huwa hawa-respond on time. Unaweza kuwaomba kitu kupitia e-mail au njia yoyote lakini kupata majibu positive ni kasheshe.
Siku nikipita Moro nitaenda kangalia physically.
Thanks very much.
 
tafuta member wa JF aliyepo morogoro anaweza kukusaidia kununua na kukutumia then unamtumia pesa via M-Pesa,ila bora utumie bank account yake ,sometime mpesa huwa inamatatizo kibao(yamenikuta)
 
nina wasiwasi kama TTSA wanauza miche ya matunda. nadhani wenyewe wamefocus zaidi kwenye mbegu za mbao.. ila hebu mtwangie huyu dada VAILET 0787387679 wa TTSA atajibu maswali yako
 
thanks,hata mimi nitamtwangia :)
nina wasiwasi kama TTSA wanauza miche ya matunda. nadhani wenyewe wamefocus zaidi kwenye mbegu za mbao.. ila hebu mtwangie huyu dada VAILET 0787387679 wa TTSA atajibu maswali yako
 
tafuta member wa JF aliyepo morogoro anaweza kukusaidia kununua na kukutumia then unamtumia pesa via M-Pesa,ila bora utumie bank account yake ,sometime mpesa huwa inamatatizo kibao(yamenikuta)

Nashukuru sana Newmzalendo.
Nitajaribu kutafuta mtu ili anisaidie kwa hilo, maana huku Mtwara ni kwenye mkia kabisa wa nchi - everything is BEHIND! Pia nitajaribu kumtwangia huyo Vailet niliyepewa namba yake hapo juu.

Thanks very much!!
 
Nilikuwa Morogoro pale SUA week jana kuchukua miche ya embe, mingi ya miti uitafutayo ipo pale, nitajaribu kumuuliza vicent ili kama miche yote anaweza kuipata itakuwa rahisi zaidi. Zeituni niliziona,komamanga, na karanga miti zile mnazotafuna mkiwa ktk ndege hewani, na vikorokor kibao.
 
Back
Top Bottom