Natafuta mganga wa jadi

hiyo salamu tu aliyoanza nayo kwenye post ake nshajua dini yake huwa wanaamini sn hizo mambo watu wa dini hiyo kuliko hata kufanya kazi.Ukikwama kabisa mtafte MZIZI MKAVU manake ye anajua tiba ya kila tatizo

Mzizimkavu naweza mpata wapi mkuu.
 
unaweza kufikia Roho ya mtu aliyekufa, Roho ya kiumbe mbinguni kuzimu kwa kupitia Mganga "mwanadamu". Tukienda huko tunaamini mwisho na si njia.
Aaah kwenda zako... uongo huo
 
Aaah kwenda zako... uongo huo

mkuu, mahusiano ya nguvu za giza na nuru sina uhakika kama wanadamu tunastahili kuyafahamu; yamefichwa sana, ila bado njia ipo wazi kumfikia Mungu kupitia kwa Shetani na kinyume chake, japo angalau kwa ngazi ya matendo.
 
Mkuu Tyta namtafuta huyu kwa ajili ya hiyo namba 3....

kwa ukaguzi wa hapo chini...sijui kama utafanikiwa...

xx.PNG
 
Sabalkheri Mabibi na Mabwana wa Jamiiforums.
Nimekuwa msomaji wa tovuti hii kwa kiasi cha muda na sasa nimeonelea vyema kujiunga nanyi.
Natafuta mganga mzuri wa jadi awezae kazi na sio mwenye maneno matupu, najua humu wapo watu kadha wa kadha waliowahi pata mitihani ya maisha na kwenda kuongea na mizimu na kupata ufumbuzi wa jambo husika.
Mimi ni mjasiriamali na napatikana morogoro na kusafiri naweza.
Kwa yoyote alie na mawasiliano na mganga mzuri tafadhali nitumie mawasiliano yake kwa PM. ukinisaidia na nikapata ufumbuzi nitakupatia zawadi.
Ni hayo tu kwa leo.

Wote mnavyoongea kama vile wacha wa mungu maisha yenu yote msaidien mwenzenu na sio kujifanya wacha wa mungu hiyo ipo wazi kwa wa afrika asilimia 80 ya waafrika kila mtu ana mganga wake
 
Ungeandika tu ni nini kinakusumbua, huenda kupitia mawazo ya watu humu ndani ungepokea msaada mkubwa. Achana na mambo ya Waganga, hao kuku, mbuzi, ng'ombe au chale utakazochanjwa tambua damu itakayotoka hapo ndio Agano linapoanzia na hiyo mizimu, hio mifugo unayoitoa ni sadaka. Utaendelea kuwa chini ya shetani mpaka pale utakaporuhusu Yesu abadilishe maisha yako, Okoka ndugu yangu na umshike Yesu kisawasawa.
 
Kila mtu ana haki ya kuamini kile ambacho anaona sahihi kwake...who are you to judge him? Nyie ni wasafi kiasi gani hadi mhukumu mapema hivi?

Mungu ametoa vipawa kwa watu wake ili watibie wwnzao kupitia mitishamba n.k ndugu ameona atapata msaada huko then mwacheni akapate salama yake. Kwani inaaminika imani yako tu ndo itakuponya, hivyo imani yako iko kwa sangoma. Mwacheni aende.

Mungu akujalie upone kupitia tiba za asili ndugu.

Kila la kheri!!

kwani wewe aliekwambia yeye anagonjeka nan?? amekuambia ni mjasiriamali sawa hajataja kitu amelaania amtegemeae mwanadam na kumfanya kua kinga yake na moyon mwake lazma amemuacha bwana kusulumalaa
 
Kila mtu ana haki ya kuamini kile ambacho anaona sahihi kwake...who are you to judge him? Nyie ni wasafi kiasi gani hadi mhukumu mapema hivi?

Mungu ametoa vipawa kwa watu wake ili watibie wwnzao kupitia mitishamba n.k ndugu ameona atapata msaada huko then mwacheni akapate salama yake. Kwani inaaminika imani yako tu ndo itakuponya, hivyo imani yako iko kwa sangoma. Mwacheni aende.

Mungu akujalie upone kupitia tiba za asili ndugu.

Kila la kheri!!

Nimekukubali sana kwa ushauri ulio utoa mkuu, upo vizuri na hongera sana.
 
Nenda kwa sheikh yeyote aliye karibu yako.
Au nenda msikitini kwa maelezo zaidi.
 
Ngoja niwasiliane na jamaa yangu anayeishi Dodoma atutafutie namba ya mzee Kingunge
 
Unajua smts inabidi tujiulize ni tajiri yupi anaeweza kujitokeza hadharani na kujigamba kuwa hajawahi kutenda dhambi(kumjibu wa dini zilizoletwa na meri) ktk utaftaji wake? mi naamini hayupo na hatakuwepo kamwe zaidi ya kugubikwa na sintofahamu na mizengwe mingi ya makafara!
 
Back
Top Bottom