juliano norman
Member
- Dec 17, 2015
- 41
- 4
kwa jina naitwa juliano norman(24),ni mkazi wa mtwara,mimi ni wa kwanza ndani ya familia yetu na kufuatiwa na ndugu zangu wawili,mwaka 2005 tulifiwa na mama yetu na kuachwa na baba tu,maisha yalikuwa magumu zaidi kwani jamaa wa upande wa mama walitutenga,wakati mama katutoka mwaka 2007 nilijiunga na shule ya sekondari mtangalanga iliyopo km 3 kutoka newala mjini,nilisoma japokuwa uwezo wa kulipa michango ulikuwa mgumu kwani kipato kilikuwa hafifu hivyo mara kwa mara nilirudishwa nyumbani,2010 nihitimu elimu ya kidato cha nne na kupata ufaulu wa D 4,kwa kweli sikuridhishwa na ufaulu wangu hivyo nikaamua 2014 nirudie mtihani wa kidato cha nne kwa masomo tano na kupata c,c,b,d na d,wakati najipanga niende form 5 baba alianza kuumwa ugonjwa wa kisukari na ilipofika 26/05/2015 baba akafariki na kutuacha yatima tusiokuwa na mlezi na ndipo ndoto za shule zikayeyuka,leo hii nipo mbele yetu kutafuta ufadhili wa kunisomesha au kunichangia ada au kwa wakazi wa mtwara mjini kama una kazi yoyote nipatie ili nipate ada.