Natafuta Mdada wa kuzaa naye mtoto

Natafuta Mdada wa kuzaa naye mtoto

Ray M

Senior Member
Joined
Sep 23, 2012
Posts
182
Reaction score
61
Jamani kama kichwa cha habari kinavyojieleza ninahitaji kupata mtoto na nimeonelea nitafute mwanamke/mdada ambaye yuko tayari kwa hilo kisha tukubaliane terms & conditions.

Ningependa mhusika awe na sifa zifuatazo
1) Awe na shughuli halali inayomwingizia kipato
2) Dini yeyote, kabila lolote. Ila asiwe extremist
3) awe tayari kuzaa bila kuhusisha mambo ya kuoana.
4) Umri kuanzia miaka 25 mpaka 32.

Terms & Conditions
*** Vipimo vyote vya afya vitachukuliwa ili kujiridhisha kuhusu usalama wetu na wa mtoto wetu pia.
1) Nitagharamia kwa 100% matunzo yote ya mtoto kuanzia mimba, kuzaa mpaka malezi. pale nitakapokwama ndipo atakuwa ananisaidia.
2) Awe tayari kuruhusu vipimo vya DNA in case any doubt arise.
3) Kwenye kadi ya Klinik nitambulike kama baba wa mtoto tangu mwanzoni kabisa
4) No ndoa attached, atakuwa huru kuolewa iwapo atapenda, na mimi pia nitakuwa huru na maisha yangu.
5) mengine tutayajadili kadri muda utakavyoruhusu.

Kuhusu mimi
1) Kijana Mtanzania miaka 26
2) Mpole, mtanashati
3) Mrefu, mwembamba, mweusi
4) Nimeajiriwa na pia ninamiliki biashara zangu
5) Ninataka niweze kupata mtoto mapema

Asanteni na Karibuni
Ray
 
"5) Ninataka niweze kupata mtoto mapema"

Wale wanaopataga watoto mapema zile ni bahati mbaya bro hawapangagi ivyoo...
 
Miaka 26 ni umri unakuruhusu kuoa kabisa ikizingatia unasema una kazi na biashara zako. Nakushauri uoe ili mtoto atakaye zaliwa apate malezi mazuri ya wazazi wote.
 
Miaka 26 ni umri unakuruhusu kuoa kabisa ikizingatia unasema una kazi na biashara zako. Nakushauri uoe ili mtoto atakaye zaliwa apate malezi mazuri ya wazazi wote.

Tatizo ni kumpata mwanamke mwenye vigezo vyote vya kuwa mke, huko mbeleni nikimpata basi tutaoana.
 
"5) Ninataka niweze kupata mtoto mapema"

Wale wanaopataga watoto mapema zile ni bahati mbaya bro hawapangagi ivyoo...

Mimi ninataka nimpate kwa kukusudia
 
Mimi ninataka nimpate kwa kukusudia

Labda ni kwanini unataka ivyoo... unajua kama umelelewa na mzazi mmoja kwa bahati mbaya na malezi yako yakawa sio mazuri.. iyo laana usiipeleke kwa mtoto wako... Jipange upete umpendaye na mzae na kulea vyema..
 
Yaani huyu hata hajui maisha ninini Mungu wangu. embu msaidieni, anyway kama shida ni mtoto anaweza akaenda kuadopt kwenye vituo wako wachanga kibao aache ununda hapa

Nataka mtoto ambaye ni damu yangu
 
Labda ni kwanini unataka ivyoo... unajua kama umelelewa na mzazi mmoja kwa bahati mbaya na malezi yako yakawa sio mazuri.. iyo laana usiipeleke kwa mtoto wako... Jipange upete umpendaye na mzae na kulea vyema..

kumpata nimpendae kwa dunia ya sasa itanichukua muda. nataka nitimize ndoto yangu ya kupata mtoto mapema hayo ya ndoa yatafuatia. nimelelewa na wazazi wote na mwanangu pia atapata malezi ya pande zote
 
Aliyekwambia wewe ni damu ya babako ni nani? na Unamwamini?

hiyo ni mada inayojitegemea, lakini cha msingi yeye ninamtambua kama baba yangu na nimefanana naye, kama humuamini mama yako pole sana
 
Mkuu RAY M natumai umeeleweka na atakayekuwa tayari kuambatana nawe basi atawasiliana nawe,nakutakia kila lenye heri katika kufanikisha mpango wako huo ila mwombe Mungu akupe afya njema ya kuweza kumjaza huyo mwanamke mimba maana wengine huishia kuweka mbegu shambani lakini mazao wasiyapate.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom