Natafuta Mchumba/Mume.

PAMELA MS nakuombea kwa mwenyezi Mungu ili uweze kumpata mtu ambaye hasa mtaendana naye. Unajua watu wengi sana hukurupuka katika maamuzi ya kumchagua mtu ambaye anatakiwa aishi naye kama mke na mme. Ndoa ni taasisi ya kwanza kabisa kuasisiwa kwa ajili ya wanadamu, tena muasisi akiwa ni Mungu mwenyewe. Lakini, Shetani kwa kufahamu nini hasa kilikusudiwa katika ndoa, ameuharibu mpango huo mtakatifu wa Mungu. Lakini jambo kubwa la kukumbuka ni kwamba kila binadamu anapoumbwa, anaumbwa na yule atakayekuwa mke/mme wake, rejea kile ambacho Mungu alikifanya kwa Adamu kwa kumuumba Hawa kwa ajili yake. Kwa hiyo hakikisha unamuomba Mungu ili aweze kukupatia mtu ambaye hasa aliumbwa kwa ajili yako.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Asante sana kaka,hakika nimeuelewa ujumbe wako uliojaa busara na elimu ya kutosha,naamini mpango wa mungu ni mwema kwa kila binadamu na ni lazima utimie kwa kila mmoja ndio maana naamini wakati wangu nao ukifika upango wake utatimia na atanikutanisha na aliyemuumba kwa ajili yangu,
Ubarikiwe sana kaka.
 
Ubarikiwe pia.
 
Hongera mwaya kwa kukupata ujasiri huu wa kueleza kile unachokitaka, usiwajali hao wanaojibu km wanatumia kichwa cha chini kufikiria,mungu akujalie umpate mkweli umtakaye.
 
Ndugu yangu Mende, ile kauli ya kusema Mende kaangusha kabati ni usemi tu...Na wewe kusema Love+Money=Ndoa nao ni usemi tu. Tabia ya mtu hairekebishiki kama kweli unaona huyu dada si riziki.Kwani wahehe bado wanakula mbwa?Makonde wanakula watu?...labda konokono kwani mimi nimeshawahi kula."mad fish"

what is uchaga bwana kwanini uogope kivuli chako mwenyewe?Kuna mtu mmoja pale Morogoro, karibu na Motel d'Job anapenda hela kiasi cha kutoa roho ya mtu..mimi mwenyewe kuliko mchaga...kwani hujui kuwa "money is the media of exchange"? Kwa ujumla sote tunapenda hela na si suala la wachaga peke yao.

Vigezo vya elimu vya huyu dada mie navikubali kwani nani anataka aolewe na mtu asiye na elimu, au kazi? sisi wanaume tunahitaji wake wenye elimu, wenye hela, wasomi waliostaarabika, wenye magari ingawa hatuna ubavu wa kuhoji wameyatoa wapi hata kama wamehongwa. Binafsi napingana na wewe "KWANI UNATUFUNDISHA WOGA"ambao madhara yake ni kutuweka kitimoto cha kuonekana hatujiamini, NAMAANISHA SISI WANAUME TUTADHARAULIWA.

Usione natetea sana hoja ya huyu dada kwani hata anyway...SIMFAHAMU, SIMJUI, SIJAWAHI MWONA ILA NIMEHESHIMU SANA POST YAKE...kwanza mbona hivyo vigezo vichache sana.

Yeye alichotaka ni elimu tu ya Diploma, kwa maelezo yake hapo juu ana Shahada ya Kwanza, hata kama hajasema amejidhatiti kwenye fani gani... hivyo anahitaji mwanaume mwenye elimu . Pili mtu aliye na kazi.."kazi ni kazi" hakutaja aina ya kazi, Awe hajaoa hata kama ana mtoto sawa tu (ona anavyojali hata mtoto wa mwenzake) Awe mkristo, asiwe mvutaji sigara,...mi nadhani hata na pombe asiwe anakunywa...eti dada yangu awe mnywa pombe?..jibu tu utuondolee mashaka.

Kingine si shahada inayotakiwa, ni mapenzi ya kweli. Unaweza tu kuwa na stashahada, astashahada, au hata shahada yenyewe na bado ukapendwa au ukachemsha, "HIVYO JENGA MAZINGIRA YA KUJIAMINI KWANZA"

Na kwa wale mliooa "KAMA MIMI" tuwe wawazi inapokuwa ni suala la kumshauri mtu kama huyu badala ya kumponda jukwaani..hili ni jukwaa la heshima, lina watu wa rika mbalimbali, elimu mbalimbali, kazi mbalimbali,humu ndani pia kuna watu wenye matatizo yao mbalimbali wanahitaji ufumbuzi na WAMETUAMINI WANA JAMII kuwa tunaweza kuwashauri vyema, hivyo tusiwavunje moyo kwa kuwatukana au kuwabeza...tuwashauri tu mungu atatulipa siku moja.

Mwisho narudia ule usemi wangu kuwa NAWAKUBALI WANAJAMII WOTE , ILA NINACHOCHUJA HAPA NI HAYA MAWAZO TOFAUTI TOFAUTI TULIYO NAYO NA TUNAYOYATOA.
 
Ushauri wako kwa Pamela ni mzuri sana unajua unapomtia mtu moyo naye anaanza kujithamini na kujitathmini.....Hofu yangu asije angukia mikononi mwa WAHUNI ingawa hilo linaweza kuwa pevu kwa hapo alipofikia.

Kingine ameweka mezani kwa kutuamini...

Pamela Ukipata mume wako umtakaye usisahau kutujulisha ili usiendelee kufuatiliwa...Utujulisheili tumshukuru Mungu pamoja.
 
Na iwe hivyo(amina).

Asante sana kaka kwa kunisaidia kuwaelewesha ambao wanakua hawajanielewa,

Baada ya kuhitimisha hili naahidi nitarudi kuleta feedback na tutamshukuru mungu kwa pamoja!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom