Mdogo wangu nataka nikushauri kidogo, Mimi pia ni Creativity kama wewe! Niko na ma ideas kibao na nayatekeleza moja baada ya jingine, achana na Mawazo ya wajinga ya kukukatisha tamaa, kwani sio kila mtu anaweza Ku create kitu hata kichwani Tu, wengi hawana kipaji hicho wanasubiri mshahara mwisho wa Mwezi mpaka kufa kwao.
Ukiwa unafikiria kutengeneza kitu kichwani usikatishwe tamaa na umasikini Wako au kukosekana kwa capital, wewe tengeneza idea yako kichwani then iamishie kwenye Makaratashi (Business plan), then tokea hapo ndo unaweza kuruhusu wazo la wapi ntapata Capital ndo litawale! Usiogope kuitengeneza kichwani idea yako hata ikiwa kubwa kiasi gani, Wajinga wasikukatishe tamaa coz wao hata Bill Gates angewaambia Mawazo na ndoto zake wangemwambia "Unawaza mambo makubwa ambayo hutaweza kutekeleza"
Duniani Kuna watu wenye pesa (Companies) lakini hawana ideas mpya, halafu Kuna Wabunifu masikini kama wewe lakini hawana Capital, hakuna mfanyabiasha ambaye atakataa kuwekeza biashara itayoleta faida, uzuri idea yako haiitaji mtaji mkubwa hivyo, zaidi ya vitendea kazi na kufanya promotion ya App yako Worldwide, na Social network zimefanya maisha yamekua rahisi.
Tengeneza Business plan Kisha tembelea watu wenye uwezo ama Kampuni kubwa then washawishi wawekeze, ila vipo vitu unaweza kufanya kabla ya kutafuta Msaada wa mtaji, hiyo Computer ya best yako japo anakumaind akiona Una type codes (japo siamini) tumia hiyo kutengeneza hiyo App yako, sidhani kama utashindwa kununua Bundles za internet, achana na Mawazo ya office kwa sasa, nakuhakikishia kama utatengeneza hiyo App yako ikawa inapatikana online, ukachukua na Business plan yako ukawafata Wadau, hawachomoi...
Tatizo letu vijana tunataka msaada hata vitu ambavyo tungeweza kuanza wenyewe, ni ngumu kupata msaada kwa maneno tu, unamshawishi mtu aweke pesa kwenye idea yako, unamweleza idea yako, mpe business plan, mwambie nimetengeza App na ipo online, na uwezo wangu umeishia hapo, nahitaji pesa kwa promotion, Kuandaa mikataba na artist and so and so, kwa nini mtu asiweke pesa???